Imani ya Wanavijiji juu ya CHADEMA yaongezeka kwa kasi; Bendera za CDM kila mahali si tishio tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imani ya Wanavijiji juu ya CHADEMA yaongezeka kwa kasi; Bendera za CDM kila mahali si tishio tena

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ta Muganyizi, May 17, 2011.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kabla ya kampeni za uchaguzi za mwaka 2010 na kurudi nyuma wanajamvi mtakuwa mashahidi jinsi bendera za CCM pekee zilivyokuwa zimeshamiri vijijini. Kipindi hicho ilikuwa ni tishio au mtu asingekaa na amani pale ambapo angetundika bendera ya chama cha upinzani nyumbani kwake kijijini. Angeandamwa na viongozi wa ccm na kuzushiwa mambo mengi ya ajabu.

  Lakini sasa hali ni tofauti. Ukipita maeneo mengi vijijini unazikuta bendera za Chadema zikipepea hadi unajiuliza confidence hii wamepata wapi? Kumbe matendo ya CCM yamewafanya hata wale waliokuwa wababe wa chama kuona aibu ndani ya jamii zao. Mzee Aliyetundika bendera ya CCM kwake sasa hivi haheshimiwi kama hapo zamani. Bali anachekwa na vijana na baadhi ya watu wazima wenzie.

  Nikitoa mfano kwa vijiji vya Shinyanga, Mwanza, Chato na Biharamulo na wilaya nyingine za Mkoa wa Kagera kwa mfano na hata vijiji vingi njiani ukisafiri kwa basi kutoka Dar kwenda Mwanza ambamo nimekuwa nikifanya shughuli zangu utaona mabadiliko ya hali ya juu. Kipindi cha nyuma ilikuwa ni vigumu vijiwe vya vijana ambao ni mafundi baiskeli au majiko au wale wa mikokoteni kukuta wametundika bendera ya Chama cha upinzani. Hata wale waendesha pikipiki walitundika bendera za CCM wakiamini kuwa Trafic asingewasumbua, vivyo hivyo na mabasi(hawa bado waoga). Kwa sasa hivi watu wanajiamini na Chadema, bendera zinatundikwa popote, waendesha baiskeli, pikipiki, vijiwe vya vijana na maeneo mengi ambayo zamani walikuwa wakiona kuwa ni tishio kutundika bendera ya CDM, kwa sasa wanaona ni ujasiri na heshima ndani ya jamii kutundika bendera hizo na kuonesha msimamo wao wazi kuwa wameschoshwa na ccm.

  Waliokuwa wababe wa ccm vijijini wanaona aibu. Wakitoa sauti wanaulizwa, Richimond, Magamba ambayo hayajavuliwa, Kagoda, Epa, wanakaa kimyaaaa. Kilichonifurahisha ni kijiji kimoja biharamulo ambapo walikuwa na gazeti la Mwanahalisi la Wiki tatu zilizopita nyuma na jingine mwezi mmoja na nusu wakiwa wamekaa eneo la kinywaji cha kienyeji wakiwazodoa viongozi wa CCM kwa chama chao kushindwa kujibu yote. Zoezi hili liliongozwa na mwalimu mmoja mstaafu aliyeamua kurudi kijijini kwao kuungana na wananchi katika kulisukuma gurudumu la maendeleo.

  Baada ya ticha huyo kutoa reference hizo, ofa ya vinywaji ilimuandama ticha na kumfanya mzee mwenzakewa ccm aone aibu.

  Yote haya wanavijiji na wananchi wengine mijini wanayafanya wakijiamini maana wanajua wana mtetezi asiyemuoga CDM ambaye atasema chochote kilicho kiovu.

  Kwa hali hii nikaona strategy moojawapo ya kuiandaa CDM kuongoza nchi ni kuwa na intelijensia wa uhakika kila wilaya au kata ili fursa za kukiimarisha chama zinazoonekana tuzitumie. Mfano CDM ni chama ambacho ni kipya na kimewajengea imani wananchi lakini huku kijijini bendera zetu zinaonekana kuchoka kama za ccm na pia ni chache. Wengi wanataka waonekane mashujaa na wenye uchungu na nchi kwa kutundika bendera maeneo yao lakini hazipatikani na zilizopo zimechakaa. Bendera ina psychological advantage yake katika jamii kitu ambacho nikikieleza hapa ccm wata ki - renew na kusumbua tena. CCM wameteka akili za wanavijiji tangu utoto sababu ya bendera. Akitokea mpinzani wanakuwa hawaelewi. Sasa kama wazee wa heshima wametundika hizo bendera za CDM vijijini, vijana wanaokua wataona ni kitu chema maana wazazi wao wanakiamini.

  Wasomi wako kibao walioamua kufanya kazi vijijini na ni vijana hivyo watumieni ( me inclusive) ila kwa kuchunguzana kwanza na kupeana viapo tusije tukawa na watu kama NAPE.

  CDM iandae intelijensia mapema wakati wakijiandaa kuchukua nchi. Mijini sawa ila harakaharaka nitumieni bendera hizo mpya na kubwa ili kabla hamjaja huku mkute watu wanawatambua vya kutosha. Zinatakiwa bendera mpya za CDM sio zilizochakaa kama za CCM maana chama tayari kimechakaa hadi Maralia Sugu amekubali.
   
 2. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  CCM hoiiii! ... CHADEMA haiiii!
   
 3. M

  Mmongolilomo Senior Member

  #3
  May 17, 2011
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kuwa na bendera haitoshi wawatambue waimarishe wajumbe wa mashina na vitongoji. Kwa kuwa watakuwa na damu ya CDM na mapenzi pia watakuwa walinzi wa kura bila ya gharama yeyote kwa maana hawatahongeka. Muda ndio huu wa kuimarisha CDM km chama na si porojo.
   
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mungu saidia CHADEMA na pia taifa hili nimekuwa katika harakati kubwa sana na pia sasa Kilio chao Mungu amekisikia Kabisa
   
 5. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kujiamini ni kitu muhimu kwa mwanadamu,kwa kulitambua hilo cdm na viongozi wote wakaamua kuwapa hilo wananchi mapema pasi na kusubili uchaguziufike.tuko pamoja kubwa kwa hilo mpaka nchi yetu ikombolewe.amina mungu yu pamoja nasi.
   
 6. Kyaiyembe

  Kyaiyembe JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2014
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2014
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,029
  Likes Received: 3,052
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mzee uandishi wako umespit venom na kudhihirisha ukweli,wewe pia ni jasiri kamanda ila nilitegemea na wewe ulambe mtaa1 mara hii
   
 8. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #8
  Dec 17, 2014
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Mleta mada lakini pia tuseme kuwa wanaharakati wasomi vijana watumie fursa wazi ya CDM kupitishia harakati zao. Yaani badala ya sisi kusubiri CDM itutumie, sisi tuitumie CDM...
   
 9. L

  Lwesye JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2014
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 5,297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Uliona mbali haya shime wote kila mtu anapotokea kuhamasisha wananchi wajitambue hakuna kuibeba CCM
   
 10. C

  Camp 05 JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2014
  Joined: Apr 27, 2013
  Messages: 875
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 80
  post hii iende mbali zaidi ya hapo,viva CDM
   
 11. mjukuum

  mjukuum JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2014
  Joined: Dec 8, 2014
  Messages: 4,999
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  Picha plz
   
 12. L

  Lugulu JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2014
  Joined: Mar 27, 2013
  Messages: 448
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  Kutoka jimbon Buchosa ni kwamba Nyehunge ambapo ndo makao makuu ya jimbo, Kalebezo, Magulukenda na kwingineko CCM imepata kipigo cha mbwa mwizi...
   
 13. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2014
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Pipoz...!
   
 14. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2014
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Ukweli ndio huu.Matendo ya ccm kwa miaka yote waliyotunyonya na kutufanya masikini sana yatawajeukia wao kwa asilimia zile zile. Hii ni kanuni ya maisha. Universal law. Haina ubishi hii.
   
 15. Van persie

  Van persie JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2014
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 916
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 60
  Watu wamewachoka majambaz hao. Wanashinda kwa sababu ya Mapingamiz. Acha mapingamiz uone unavyogaragazwa. wananchi wamewachoka jaman . CCM Majiz Mno. Saiz tunataka uchaguz so Mapingamizi.
   
 16. Hansard

  Hansard JF-Expert Member

  #16
  Dec 18, 2014
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 835
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
 17. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #17
  Dec 18, 2014
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Loh jamani hii thread nilishaisahau kumbe wadau mna documentary......niliiandika 2011!!!
   
 18. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #18
  Dec 18, 2014
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  ahahahaaa......rweye tuonane basi tupange mikakati
   
 19. NYEHUNGE

  NYEHUNGE JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2014
  Joined: Jul 31, 2013
  Messages: 329
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa, kila kona sasa hivi ni sherehe.
   
Loading...