Imani ya chama chao hii hapa,wanaitekeleza au uongo mtupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imani ya chama chao hii hapa,wanaitekeleza au uongo mtupu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by AMARIDONG, Sep 15, 2010.

 1. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  IMANI YA CCM
  • Binadamu wote ni Sawa
  • Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake
  • Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru
  AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI
  (1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja
  (2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote
  (3) Nitajitolera nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.
  (4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.
  (5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
  (6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.
  (7) Nitashjirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.
  (8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.
  (9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hii ilikuwa imani ya ccm ya Nyerere. Baada ya hapo imani ziliendelea kubadilika kadri viongozi wake walivyobadilika.
  Sasa tuna sisi m ya msanii kikwete wao wanaita sisi m maslahi na imani yake ya kwanza ni kwamba anayeweza kuiba sana na kumgawia kidogo kwa njia ya kampeni ndiye atakuwa rafiki yake mkubwa.
  Sisi m ya leo ni tofauti kabisa na ile ya mwaka 1977. Kama ingelikuwa ni sisi m ile ile nisingeshindwa kujiunga na sisi m.
   
Loading...