Imani na jaji mkuu wa Tz ilishanitoka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imani na jaji mkuu wa Tz ilishanitoka

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by johnmashilatu, Dec 23, 2010.

 1. j

  johnmashilatu JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  AGIZO la Jaji Mkuu Agustino Ramadhan la kupatiwa dhamana kwa raia wa Afrika Kusini, mwenye asili ya Kiasia Dawid Human (48), aliyehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela na faini ya sh milioni mbili, limefanikisha mfungwa huyo kuachiwa kwa dhamana.
  Dawid, ni Mkuu wa Kitengo cha ulinzi cha kampuni ya Geita Gold Mines (GGM); alikutwa na hatia ya shambulio la aibu hivyo kupewa adhabu hiyo Desemba 10 mwaka huu, baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kujiridhisha kwamba mfungwa huyo alitenda kosa.
  Baada ya hukumu hiyo kutolewa, Dawid alikata rufaa na wakati huo huo Jaji Ramadha, aliagiza mfungwa huyo kupewa dhamana baada ya maombi ya dhamana yake kuwasilishwa kwa jaji huyo.
  Kwa mujibu wa maelekezo ya Jaji Ramadhan, Dawid alipewe dhamana hiyo kwa sababu za kibinadamu hivyo kutakiwa kuwasilisha mahakamani hapo pasi ya kusafiria na mdhamini mmoja aliyesaini mkataba wa dhamana ya sh milioni tano.
  Hata hivyo, Dawid alifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana hiyo na hivi sasa yuko nje. Akizungumzia suala hilo kwa niaba ya Msajili Msaidizi wa Mahakama ya Rufaa, Janeth Masesa, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamaga, alisema Dawid akamilisha masharti ya dhamana yake Desemba 21 mwaka huu.
  Masesa, alisema raia huyo wa kigeni atakuwa nje kwa dhamana hadi hapo rufaa yake itakapoanza kusikilizwa. Hukumu ya Dawid ilitolewa na Jaji Aishiel Sumari wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo. Ilidaiwa kuwa Machi mwaka 2007 katika kijiji cha Mchauru, kilicho kwenye mgodi wa Geita, Dawid, alimshika matiti, sehemu za siri na makalio Adelina kwa nia ya kumnyangÂ’anya kitambulisho baada ya kufukuzwa kazi mgodini hapo.

  Source: Tanzania daima

  My take

  Imani na Jaji mkuu huyo Brigedia jenerali, mwimba kwaya, Agustino Ramadhan ilinitoka siku nyingi hasa alipoongoza jopo la majaji wenzake na kukataa asiwepo mgombea binafsi.

  mimi sio mwanasheria, lakini hizo sababu za kiutu kwanini zitolewe kwa mzungu pekee? au huyo mzungu ndio mtu zaidi ya mama aliyemdhalilisha?

  Nafikiri jaji Agustino ramadhani ambaye pia nasikia ni mwenyekiti wa mahakama ya haki za binadamu ya afrika, anapaswa kuchagua moja. yeye ni Muumini na kule kile kifungu kinachosema, Huwezi......, chagua, kwaya au anzisha kampuni ya ulinzi huko unaweza kufanya vizuri vinginevyo idara ya mahakama chini yako inatia kizunguzungu

  naambiwa kesho unaweza kuagwa (kustafu) mimi nasema umechelewa!, tutakukumbuka kw alipi ulilofanya wakati wa uongozi wako wa idara ya mahakama?, nakumbuka samwel Sitta aliwahi kukupa vidonge vyako kutokana na jinsi mahakama inavyofanya kazi zake.
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Very sad indeed. Sababu za kibinadamu kwa mzungu tu wakati kuna waswahili kibao waliiobambikiwa kesi na wanaotia huruma na wanaostahili kuonyeshwa ubinadamu. Kwa maamuzi haya anamaanisha kwamba jela ni kwa ajili ya waswahili pekee na siyo wazungu.

  Huyu bwana alitakiwa kuwa likizo ya lazima kabla ya kustaafu lakini maeendelea kuwa kazini na kutoa maamuzi tata kama hilo na lile la juzi la kulazimisha kuendelea na kesi ya samaki wa Magufuli wakati Serikali haina imani naye. Sasa hivi anaandaa successor ambaye atahakikisha anam-control na aliye na mashaka ya uadilifu wake kama yeye.
   
 3. D

  Deo JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Well said. I share the same opinion too. Lakini katika hizi teuzi za Kikweti nani aaminike?
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tukitaka nchi yetu ipone haraka kutokana na haya makovu yanayotokana na uteuzi wa watendaji wa juu wasio makini, baada ya mabadiliko ya katiba, ambayo kwa vyovyote vile, itauondoa huu mfumo unaomruhusu rais kufanya uteuzi wa nafasi zote nyeti bila ya kuhojiwa na chombo chochote, watu wote wajiuzuru ili nafasi hizo ziweze kuzibwa kwa kutumia utaratibu mpya utakaokuwa umewekwa chini ya katiba mpya.
   
Loading...