cyrustheruler
JF-Expert Member
- Jul 20, 2015
- 2,044
- 1,869
Kwanza niwashukuru watu wa huku ndani kwa michango na utatuzi wa hoja zinazoletwa humu ndani.
Leo naomba kuwashirikisha juu ya hili jambo sijui ni imani au ni kweli juu ya matukio yaliyokuwa yakigonga vichwa vyetu zamani za utoto wetu juu ya visa vya watu waliokuwa wakinyonya damu watu huko vijijini kwetu walikuwa wakiitwa ''msekwa"sijui maeneo mengine walikuwa wakiitwa nani pengine tufahamisheni ukweli hasa wa mambo yale na pengine tuweze kuelewa hasa ni nini kilichokuwa kikifanyika.
Maana tukiona gari la ''bandawazi"watoto walikuwa hawakai eneo hilo au ''110"landrover nyekundu na ya kuwa wanyonyadamu hao walikuwa wakiteka watu na kuwanyonya damu yote na kuwapiga Mihuri,wengine walisema kuwa watu wale walikuwa watu waliotumwa na serikali kukusanya damu kama ndivyo tujulisheni na kama sivyo tujulisheni.Kiukweli ilikuwa ni hofu sana katika habari zile.
Je nini lilikuwa lengo la shughuli zile kama ilikuwa kweli?
Nitashukuru sana kwa ufafanuzi wowote utakaopatikana hapa.
Nawasilisha.