Imani ina nguvu kiasi gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imani ina nguvu kiasi gani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by vukani, Mar 24, 2010.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35


  Hebu leo tuangalie mfano huu wa imani kwa kusoma habari hii ya mwanamke aliyekuwa akitokwa na damu, katika kitabu cha Marko 5:25-34.

  Nitanukuu
  “Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na mbili na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa na vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya. Aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu nitapona. Mara chemchemi ya damu yake ikakauka , naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule. Mara Yesu, hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu? Wanafunzi wake wakamwambia, Je! Wawaona makutano wanavyokusonga-songa , nawe wasema , Ni nani aliyenigusa? Akatazama pande zote ili amwone yule aliyelitenda neno hilo, Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote. Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.”

  Huyu mwanamke alikuwa na hili tatizo kwa miaka 12, ambayo kwa kweli ni miaka mingi sana kuishi na ugonjwa. Na alijaribu kila njia, akitafuta tiba lakini hakuweza kupona.

  Hata hivyo kitu kimoja kilichonivutia ni kwamba, pamoja na kuhangaika kwa miaka yote hiyo akitafuta tiba lakini hakukata tamaa, na baada ya kusikia habari za Yesu akaona ni vyema ajaribu huenda atapona, na hakika kutokana na imani aliyokuwa nayo akapona. Bwana yesu asifiwe!

  Watu wengi wanadhani kuwa imani ni kama mazingaombe kwamba unaamini tu halafu imani yako inakuletea kila kitu unachohitaji mikononi mwako .
  Hii haiwezekani. Iwapo fikra hasi, au matamshi yako ni ya kukata tamaa na hujiamini, imani haiwezi kufanya kazi kwa mtu wa namna hiyo. Kwa nini?
  Ni kwa sababu Imani sio kitu kinachofanya kazi papo kwa hapo, bali inahitaji mchakato fulani huku ikirutubishwa na fikra chanya.

  Ili imani iweze kufanya kazi ni lazima ipitie katika mchakato ufuatao ndio ufanye kazi:


  Uamuzi: Kumbuka kwamba huyu mwanamke alikuwa amejaribu tiba kadhaa wakiwemo madaktari bingwa na maarufu, hakuweza kupona, lakini aliposikia habari za Yesu akafanya uamuzi katika moyo wake kwamba kupitia Yesu Kristo atapona. Huo ni mchakato wake wa kwanza kabisa kuelekea katika kupona.

  Imani: katika Marko 5:28 yule mwanamke alisema “Nikiyagusa mavazi yake tu nitapona” Ile kauli ya kusema “Nitapona” ni kauli chanya na yenye nguvu na kama tulivyoona kuwa inatoka kwa mwanamke ambaye alikuwa amejaribu tiba kadhaa kwa miaka 12 bila kupona.
  Ni katika Matayo 9:20:22 tunaposoma kuwa alijisemea kauli hiyo kutoka moyoni mwake. Hapo ndipo tunapoona kuwa ni kwa jinsi gani imani inavyokuwa na nguvu hata kwa kujisemea moyoni tu, inatosha kufanya jambo liwe.

  Kutenda: Katika Marko 5:27, tunasoma kuhusu, mwanmke huyo Alivyopenya katika kundi la watu na kwenda kugusa mavazi ya Yesu Kristo.
  Ni kitu gani kilimsukuma hadi akaamua kujipenyeza katikati ya kundi la watu ili tu kugusa mavazi ya Yesu?
  Ni kwa sababu aliamini neno la mungu na ndio sababu ya yeye kuchukuwa uamuzi.
  Kutenda kile unachokiamini ndio njia sahihi ya wewe kuelekea katika kufanikiwa, haitakiwi kusema tu, hiyo haitoshi.

  Ili imani iweze kufanya kazi ni lazima upitie katika mchakato huo ndipo imani iweze kufanya kazi.
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Imani ina uwezo wa kuhamisha milima. Ila hofu ya Mungu lazima iwepo
   
 3. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  soma waebrania 11:1-kuendelea utaona kazi ya imani na nguvu ya imani yote ktk yote ni kwamba imani ndio tunayoitaji kumpendeza mungu na kufanya mambo makuu hapa duniani
   
 4. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Haleluyaa...
  Imani ina nguvu sana na inafanya kazi.
   
 5. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  haswa inapokuwa hai na mwenye nayo asiwe na hofu wala mashaka kama petro kwani kwa imani alitembea juu ya maji alipo ona shaka tu akaanza kuzama ila aliweka historia kuwa mwanadamu wa kwanza kutembea juu ya maji baada ya yesu
   
 6. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Imani ni kuwa na uhakika na mambo yajayo/ unayotarajia, na usiwe na hofu wala mashaka, kila kitu kinakuwa,
  Mwanmke aliyetokwa na damu imani yake ilikuwa juu sana aliona siyo lazima Yesu amguse aliammini akigusa vazi lake tu atapona ndo maana alipona.
   
 7. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kuchukua hatua ndio tatizo kubwa la weni wetu na hivyo imani huishia mioyoni mwetu tu. Tuna imani ya kuendelea lakini hatujachukua hatua maalum za kutufanya tuendelee.
   
 8. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145

  imani inapokosa matendo imekufa
   
 9. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135

  imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana na mambo yasiyoonekana................. angalia hapo kuna points kadhaa ambazo ndio compenent parts za imani:

  1.
  kuwa na hakika (to be certain)

  2.
  ya mambo yatarajiwayo (expected), yaani yale ambayo hayajatokea bado

  3.
  bayana na mambo yasiyoonekana (unseen).............. kubainisha ni kuweka waziwazi.... hivyo hapa ina maana yasiyoonekana kuwa waziwazi.........

  hivyo imani ya kikristo lazima ianze akilini (rejea imani chanzo cake ni kusikia............. ) hata yule mwanamke alisikia kwanza kabla hajaamini na kuamua kumtafuta Yesu............... hivyo hapa tunawaondoa wote wanaoamini kabla hawajasikia.......... hawa watakuwa watarajia miujiza tu na hata washirikina............ hii ni knowledge component.....

  pili imani lazima ihusu mamabo yajayo, yaani yatarajiwayo....... ikihussha yaliyopita haitakuwa imani tena........ yaliyopita ni msingi wa imani pale yanaposikiwa na huifanya hiyo knowledge component

  tatu, imani lazima iyaone waziwazi yale yasiyoonekana (yaani iyaone bayana bayana kana kwamba yamewekwa tayari mbele yake)............. iyo ndiyo imani ya kikrristo...............

  ziko imani nyingi, na zinatofautiaana ......... laki ya kikristo ndiyo hiyo, imani nyingine tofauti nahiyo sip ya kikristo..................

  mbarikiwe nyote.................
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  If you believe , you can fly!
   
 11. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,501
  Likes Received: 1,082
  Trophy Points: 280
  Vipi kuhusu imani zetu za asili jamani zile za chifu kuzikwa na dume la ng"ombe? ili jamii isipate majanga.
   
Loading...