Imamu kortini kwa wizi wa nyaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imamu kortini kwa wizi wa nyaya

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Dec 27, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Imamu kortini kwa wizi wa nyaya


  Na Yusuph Mussa, Lushoto

  IMAMU wa mwalimu wa dini wa Kijiji cha Mkuzi, Kata ya Kwai wilayani Lushoto Bw. Amir Kijangwa (47) amefikishwa mahakamani akituhumiwa kuiba Nyaya za umeme zenye uzito wa kilo 19 huku zikiwa na thamani ya sh. 285,000.Akisoma
  mashtaka hayo mwishoni mwa wiki kwenye Mahakama ya Wilaya ya Lushoto, Mwendesha Mashtaka, Bw. Evarist Mwamengo alisema Desemba 18, mwaka huu saa moja asubuhi Bw. Kijangwa alikamatwa na kiroba cha nyaya hizo nyumbani kwake.

  Hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo, Bw. Yona Wilson alitoa dhamana kwa mtuhumiwa huyo, mara baada ya Bw. Kijangwa kukataa kosa lake na kesi inatarajiwa kutajwa tena Januari 4, mwakani.

  Wakatu huo huo, Meneja wa TANESCO Wilaya ya Lushoto Bw. Said Mhando amesema wimbi la wizi wa nyaya za umeme limezidi kuongezeka baada ya watu wasiofahamika kuiba nyaya usiku wa kuamkia Desemba 20, mwaka huu.

  Bw. Mhando alisema nyaya hizo zenye urefu wa mita 800 na thamani ya sh. milioni mbili ni muendelezo wa matukio hayo yaliyoanza Septemba, mwaka huu na kuwa hadi sasa yameshatokea matukio saba yaliyosababisha wikiwa nyaya zenye urefu wa mita 2,740 zenye thamani ya sh. milioni 6.8.

  "Wananchi lazima waelewe TANESCO au Jeshi la Polisi hawana uwezo wa kulinda miundombinu ya umeme, na jukumu hilo ni la wananchi wenyewe kwa kuwa matokeo yake ni kukosekana huduma ya umeme.

  "Lakini pia shirika linapata hasara kwa kuweka miundombinu mipya maeneo ya wizi na kuacha kuwawekea wananchi wengine wapya, lakini pia wafanyakazi wanaacha kufanya kazi mpya na kuziba mapengo ya wizi, matokeo wananchi wanalalamikia huduma inachelewa kwao," alisema Bw. Mhando.

  [​IMG]
   
 2. October

  October JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kaasi kweli Kweli!!
  Anapeleka wapi hizo nyaya za wizi huyu Imamm?
   
 3. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
  masjid
   
 4. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2010
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Unawachokoza???
   
 5. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,766
  Trophy Points: 280
  Mwizi ni mwizi tu hata awe imam.................. LAKINI NADHANI KILICHOMSHAWISHI KUIBA NI SHIDA ZAKE NA SI DINI YAKE............
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,135
  Trophy Points: 280
  Uwoo ndg zangu washambaa saasa inakuaje tena huko kaya jamani, huyu imamu si ndio mkwewe Malaria Sugu huyu..
   
 7. P

  Percival JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,567
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Nani si mwizi hapa ?
   
 8. Antonov 225

  Antonov 225 JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  watu wote huwa tunakosa jamani, na tukikosa tunapata nafasi ya kutubu. Yesu alikuja dunia na ujumbe wa "Tubani na Kuiamini Injili" kwa hili tunatambua kila mtu anadhambi na ana nafasi wakati wowote kupewa nafasi ya kutubu na kumrudia MUUMBA Mbingu na nchi.
   
Loading...