Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,278
- 8,868
Imamu wa Jumuiya ya Sawiyatu Qadiria ambaye ni mkazi wa Tindiga eneo la Unga Ltd, jijini Arusha, Hassan Bashir (33), amemwagiwa kimiminika kinachosadikiwa kuwa tindikali sehemu ya mabegani iliyosambaa maeneo ya mgongoni na shavu la kushoto.
Akitihibitisha taarifa hizi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amesema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 3:45 usiku maeneo ya msitiki huo.
Hata hivyo, Sabas alisema upelelezi kuhusiana na tukio hilo bado unaendelea ikiwa ni pamoja na kutumia kopo lililokuwa na kimiminika hicho ambacho kimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kujua uhalisia wake.
Alisema, uchunguzi wa awali wa polisi pamoja na maelezo ya Imamu Hassan ni kuwa muda si mrefu kabla ya tukio hilo, Hassan, alikuwa anatokea maeneo ya kituo kikuu cha mabasi cha Arusha baada ya kuachana na wenzake wawili, ambao aliwataja kuwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Ismail Olomi na Abdallah Sadila Kaduma ambaye ni mwenyekiti wa ujenzi wa msikiti huo, ambapo walikuwa wanajadili kikao cha Maulid.
Imamu Hassan alisema muda huo wa saa 3:45 alikuwa maeneo ya karibu na kwake Unga Ltd, ndipo alipomuona mtu amesimama kwenye kiambaza cha msikiti, alimsalimia, lakini hakumbuki kama alijibiwa. Wakati akiendelea kuelekea kwake, alihisi kuna mtu anamfuata na alipogeuka ili ajue ni nani, ghafla mtu huyo alimwagia kimiminika kinachosadikiwa kuwa ni tindikali.
Alisema mara baada ya kitendo hicho mtuhumiwa alikimbia na kuelekea kusikojulikana.
Alisema baada ya taarifa hiyo polisi waliokuwa doria maeneo ya karibu walikwenda katika eneo hilo na kukuta kopo dogo ambalo linasadikiwa kuwa lilikuwa na kimiminika kinachosaidikiwa kuwa na tindikali.