Imamu amwagiwa tindikali Arusha

Imamu amwagiwa tindikali Arusha

Status
Not open for further replies.
Sio znz ni Tanganyika Arusha itakuwa ni CDM na wakiristo wamekasirika huyo Sheikh kusamami ujenzi. CDM na wakiristo ni wauwaji sana
 
Sio znz ni Tanganyika Arusha itakuwa ni CDM na wakiristo wamekasirika huyo Sheikh kusamami ujenzi. CDM na wakiristo ni wauwaji sana

CDM na mtu kumwagiwa kimiminika vinahusiana vipi? Inafaa useme ukweli na sio kugesi
 
Sio znz ni Tanganyika Arusha itakuwa ni CDM na wakiristo wamekasirika huyo Sheikh kusamami ujenzi. CDM na wakiristo ni wauwaji sana
Huyu sheikh namfahamu. Katika umri wake wa miaka 33 amemudu kuacha wake 4, hivi sasa ana wake wanne lakini haachi kuparamia wake za watu. Jamaa wameamua kumfanyia kitu mbaya
 
Kws CDM na wakiristo ni jambo la kwaida kuuwa na kunyanyasa kama vile kanisa lilivyo husika na mauwaji ya Ruwanda

Labda useme km uko wanakojitoa mhanga...referenci yako haina kichwa iyo mambo ya kanisa la rwanda ndo unataka useme kanisa lilikuwa na bifu na tutsi au hutu mbona unaongea utumbo mzazi ;ile ilikuwaga ni bifu ya kikabila tu mbona hilo likowazi ? Pia kumbuka rwanda kulikuwa na watusi na hutus at the same time burundi kulikuwa na watusi na wahutu hivyo pia haikuwa vita kati ya nchi na nchi ila ni kabila na kabila..elewa mbambo ww
 
pole Imam,Allah atakupa shifaa in shaAllah.

Na wale wa
naojifanya ugomvi wa mskitin unaohusu michango na ujenz na yakitokea kanisani musikimbize waislamu wamefanya na huko makanisani yapo hayo ya michango kila leo!
 
Waache kugombania misikiti. Huyo shekhe yuko chini ya Bakwata ndio maana wafuasi wa Ponda wamemmwagia tindikali
 
Tanganyika si sehemu salama tena ya kuishi, na juzi tuu walipigana mapanga kwenye uchaguzi mdogo
 
Labda useme km uko wanakojitoa mhanga...referenci yako haina kichwa iyo mambo ya kanisa la rwanda ndo unataka useme kanisa lilikuwa na bifu na tutsi au hutu mbona unaongea utumbo mzazi ;ile ilikuwaga ni bifu ya kikabila tu mbona hilo likowazi ? Pia kumbuka rwanda kulikuwa na watusi na hutus at the same time burundi kulikuwa na watusi na wahutu hivyo pia haikuwa vita kati ya nchi na nchi ila ni kabila na kabila..elewa mbambo ww

Mashirika yote duniani pamoja UN wametoa riport kuwa kaniasa katoliki linahusika ktk mauwaji ya halaiki ya Wanyaruanda ww uko wp au hutaki tu hu ukweli?
 
IMAMU wa Msikiti wa Sawiyatu Qadiria, Hassan Bashir (33) amejeruhiwa vibaya usoni na sehemu ya bega la kushoto baada ya kumwagiwa kimiminika kinachodhaniwa kuwa ni tindikali.
Akizungumza na Tanzania Daima kwenye wodi ya wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru anakopatiwa matibabu, imamu huyo alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya kati ya saa 3:30 na saa 4:00 usiku karibu na Msikiti wa Tindiga, uliopo eneo la Unga Ltd.
Alisema ana maumivu makali sehemu ya uso pamoja na bega la upande wa kushoto.
Sheikh huyo ambaye alikuwa akizungumza kwa shida kutokana na maumivu makali, alisema alikumbwa na mkasa huo muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo na babu yake ambaye pia ni Mwenyekiti wa Msikiti, Ismail Olomi na Mwenyekiti wa Ujenzi, Abdalah Kaduma, juu ya maandalizi ya Maulid yanayotazamiwa kufanyika msikitini hapo.
“Tulipomaliza kuzungumza mimi nikawa naelekea nyumbani kwangu, jirani na hapo msikitini. Wakati ninatembea nikapita kwenye duka la dawa nikaona kuna mtu kavaa koti jeusi nikamsalimu lakini sijui kama aliitikia.
“Wakati nakaribia kuingia kwenye shule ya Madrasa ambayo iko jirani na nyumbani kwangu, nikahisi kama kuna mtu ananifuata nyuma, ile nageuka tu, nikaona mtu ananiziba uso na kunimwagia kitu usoni na kikopo alichokuwa amekibeba kikadondoka chini na yeye akakimbia.
“Kiasi kidogo cha kimiminika hicho kiliingia mdomoni nikasikia uchachu ndipo nikaanza kusikia maumivu makali usoni na kwenye bega la kushoto nikapiga kelele kuomba msaada kwani nilikuwa nasikia kizunguzungu,” alisema Imamu Bashir huku akitokwa machozi.
Alisema kuwa alisaidiwa na mkewe, Zulfa Said, pamoja na majirani na kuwaonyesha lile kopo ambalo baadaye walilikabidhi polisi.
Imamu huyo anahusisha tukio hilo na ugomvi kati yake na mtu mmoja ambaye jina lake kwa sasa linahifadhiwa, ambaye ni Mwislamu mwenye msimamo mkali.
Alisema mtu huyo mwaka jana aliongoza kundi la vijana kuvamia msikiti mdogo wa babu yake ulioko Sombetini, yeye alikwenda kuwaondoa na tangu wakati huo, mtu huyo akaahidi kulipa kisasi.
Imamu Bashir alisema mbaya wake huyo aliwahi kumjeruhi kijana wake wa madrasa, Saban Yunus na kumshitaki Polisi na shauri lao lilimalizika Desemba mwaka jana kwa mtu huyo kuhukumiwa kifungo cha nje.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa wanamshikilia mtu mmoja ambaye hakumtaja jina.
Alisema kopo lililotumika kubebea kimiminika hicho litapelekwa kwa Mkemia Mkuu kwa uchunguzi ili kubaini kitu kilichotumika kumdhuru imamu huyo.
Hili ni tukio la pili kutokea jijini hapa. Julai 14, mwaka jana, Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba, alijeruhiwa kwa kumwagiwa maji yanayohisiwa kuwa tindikali na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake eneo la Kwa Mromboo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom