Hapa nanukuu maneno bora mno miongoni mwa maneno ya mwanachuoni huyu,alipokuwa anaelezea ukweli kuhusu Wanafalsafa.
Lengo la kunukuu maneno haya ni kuangalia ukweli na uzito wa maneno haya kisha tuwajadili Wanafalsafa hawa na athari zao katika jamii zetu.
Anasema Imamu Ghazali :
"Siku hizi tunawaona watu wanaojidai kuwa ni bora kiakili kuliko wengine. Watu hawa wanayaangalia kwa dharau matendo ya kidini kwa kuwa wao wamejifunza majina yanayo ogopesha ya baadhi ya wanafalsafa wa kigiriki kama vile Aristotle,Socrates na Plato. Wamejifunza kutoka katika maandiko ya majisifu ya wafuasi wao kuwa wanachuo wa kigiriki wa zamani walifanya uvumbuzi wa kina katika nyanja za Hisabati,Mantiki,Fizikia na Elimu ya asili ya vitu,na na kuwa watafiti hawakuwa na kifani cha sifa za moyo,lakini wameikataa imani na mafundisho yake. Wakubwa wa kigiriki waliiagalia dini kama imani yenye kulazimishwa kwa wanaadamu bila kuwepo usaili wala uhakika. Sasa huku wakifuata hatua za viongozi wao,watu hawa wamekataa hata Dini ili wafuasi wao wawaone wao kama wenye akili huru na makini. Ili wajisingizie kuwa wao ni wataalamu na wasomi,watu hawa huikana Dini na ndiyo maana nikaona ipo haja ya kuyatambulisha makosa yanayofanywa na wanafalsafa wa kigiriki,katika maandiko yao kuhusu Elimu ya asili ya vitu. Pia nilikusudia kuonyesha wazi wazi jinsi jengo na kanuni,fikra na mtizamo wa wanafalsafa hawa zaidi ya mchezo wa kitoto,au kwa kweli,ni kichekesho"— Rejea kitabu (Incoherent of the Philosophers/Tahafut al-Falasifah/Kutokueleweka kwa Wanafalsafa
Wajuzi wa Wanafalsafa na mitazamo yao mnahitajika kulijadili au kuwajadili watu hawa.