Ilikuwaje bbc waudanganye ulimwengu juu ya mauaji ya arusha??

DON KILLUMINATI

Senior Member
Jan 2, 2011
193
83
HESHIMA KWENU WANA JAMVI.

TUMESHUHUDIA NA YALIYOJIRI ARUSHA NA KUSABABISHA KUPOTEZA ROHO ZA MASHUJAA WETU KUTOKANA NA UBABE WA SERIKALI YA CCM.

KITU KIKUBWA NINACHOJIULIZA NI KWAMBA, SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA UINGEREZA - BBC, NI SHIRIKA LINALOHESHIMIKA DUNIANI KWA KUTOA HABARI ZA UHAKIKA.

MARA BAADA YA TUKIO LA ARUSHA, SHIRIKA HILO LILIRIPOTI KUPITIA MTANDAO WAKE WA BBC Swahili - Mwanzo KWAMBA ZAIDI YA WATU 10 WAMEUAWA KATIKA VURUGU HIZO.

LAKINI HABARI HIYO ILIKUJA KUWA TOFAUTI NA TAARIFA YA POLISI KWAMBA WAMEKUFA WATU 2 TU, LAKINI HAPO HAPO MGANGA MKUU WA HOSPITALI YA MT. MERU, NAYE ALITHIBITISHA KWAMBA NI WATU 3.

SWALI NI KWAMBA, INAKUWAJE SHIRIKA KUBWA KAMA HILI KUANDIKA HABARI ZA UPOTOSHAJI? NA JE NI HATUA GANI ALIZOCHUKULIWA MWANDISHI WA HABARI ILE?

UKIFUATA LINK YA ILE HABARI UTAONA YA KWAMBA WAMEBADILISHA NA KUWEKA KWAMBA WATU WAWILI NDIO WALIOUAWA KATIKA MAANDAMANO YALE.
 
UKIFUATA LINK YA ILE HABARI UTAONA YA KWAMBA WAMEBADILISHA NA KUWEKA KWAMBA WATU WAWILI NDIO WALIOUAWA KATIKA MAANDAMANO YALE.

mkuu... utoaji wa habari unaenda na mtiririko wa upatikanaji wa habari.... kuna instant kutoka kwenye scene (habari za awali) na mwisho kuna confirmed reports.... wapo sahihi .., wasingesahihisha ndio pangekua na upotoshaji
 
Pamoja na swali hilo, ongezea lifuatalo:

Ilikuwaje M/Kiti wa cdm taifa adanganye kuwa waliuawa watu sita Arusha na kwamba maiti nne zilikuwa KCMC na zingine Mawenzi?

Jibu ni moja tu:
Wote ni watu wa kukurupuka.
Wanatoa kauli za kuzusha zisizofanyiwa utafiti.
 
Waliokufa ni zaidi ya 1O,hilo halina ubishi,kitengo cha intelijensia cha cdm kiliweza kutambua idadi hiyo,pia wengine wakiwa na risasi motuary ya kcmc na mawenzi,kuna habari kuwa polisi kwa kushirikiana na halmashauri walizika miili miwili usiku huo huo,,,,ni siku ya ukombozi
 
Kwani hii itakuwa mara za kwanza CHADEMA kutoa habari zisizo sahihi?

BBC nao wamejifunza kitu, kuanzia sakata la uchaguzi hadi kwenye issue hii.
 
Waliokufa ni zaidi ya 1O,hilo halina ubishi,kitengo cha intelijensia cha cdm kiliweza kutambua idadi hiyo,pia wengine wakiwa na risasi motuary ya kcmc na mawenzi,kuna habari kuwa polisi kwa kushirikiana na halmashauri walizika miili miwili usiku huo huo,,,,ni siku ya ukombozi

Waliozikwa hawana ndugu wa kuja kulalamika huko cdm ili miili hiyo ifukuliwe na kuzikwa kwa heshma?

Acha kuweka upuuzi hapa. Kama huna la kuchangia si lazima uweke pumba humu.
 
Kwani waliozikwa leo ni wangapi? Na hao ni pamoja na Mkenya?
 
kwani waliozikwa leo ni wangapi? Na hao ni pamoja na mkenya?

kwenye taarifa ya habari wametangaza wawili, mmoja kasafirishwa kwenda rombo, na mwingine kazikwa usa river, suala la mkenya sijalisikia kabisa. Labda mdau mwenye taarifa zaidi atujuze.
 
Kwani hii itakuwa mara za kwanza CHADEMA kutoa habari zisizo sahihi?

BBC nao wamejifunza kitu, kuanzia sakata la uchaguzi hadi kwenye issue hii.

kimenuka! Naona mambo ya u-simba na u-yanga yameshaingia na hoja nzima imetupwa kule.
 
Vyombo vya habari vya kimagharibi vina agenda moja tu, kuhakikisha vina halalisha unyonyaji kwa nchi za Afrika kupitia migogoro inayotokea! sasa hivi utawasikia wazungu wanatikisa kiberiti kuhusu misaada. Nakumbuka waliumbuka sana kule zanz. baada ya Seif kukubali matokeo kirahisi, waandishi wa habari wa wazungu wasikika wakisema kuwa 'hakuna habari tena huku ! maana Seif keshakubali tena du! mi nakuja bara bwana' ni propaganda juu ya propaganda WANApenda kukuza jambo lionekane linahitaji msaada wa kimataifa wapenyeze hoja zao za AFCOM. na KUFILISI BARA HILI KWA KUBEBA RASILIMALI ZOTE
 
Neno la ukombozi kwao wanaopotea ni upuuzi,,huu ndio ukweli,nilikuwepo kwenye tukio na kcmc nimeziona,cdm hatutafuti public smpath,na kwa information kuna majeruhi wenye hali mbaya sana,,,,,
 
Waliozikwa hawana ndugu wa kuja kulalamika huko cdm ili miili hiyo ifukuliwe na kuzikwa kwa heshma?

Acha kuweka upuuzi hapa. Kama huna la kuchangia si lazima uweke pumba humu.


Kishongo wewe ndiyo MPUUZI.

Ni kweli kuwa watu waliokufa ni more than 10! Mpaka sasa maiti ambazo ziko rasmi katika vyombo vya habari na Jeshi la Polisi ni 2 plus ile ya 3 ya MKENYA.

Kuna watu kama omba omba waliouwa kwa kupigwa RISASI na hawana ndugu zao Arusha. Hao utasemaje??? Kumbuka hawa Polisi walikuwa wana-shoot blindly kwa kuwazia kuwa BAADA YA WATU KUFA LAWAMA ZITAENDA CHADEMA.

Think about yule Mkenya wa watu,kulikuwa na sababu gani ya kum-shoot? A kenyan citizen ni lini alikuwa mwana-CHADEMA? Haya yalikuwa ni mauaji ya makusudi tu almradi ionekane kuwa CDM wamesababisha mauaji?? Hii inathibitisha kuwa JESHI LOTE LA POLISI KUANZIA IGP MWEMA mpaka corporal wa VV ni vihiyo watupu. Wote ni ma-failures wa Darasa la 7,Form 4 na Form 6!!

Polisi wote wana IQ za kuku. Wakishapewa amri ni kutekeleza tu hakuna ku-reason!!! Hiyo ndo Polisi yako. Kwa hiyo usijaribu kutetea upuuzi. Polisi ni kweli wamezika maiti zisizokuwa na ndugu zao hasa za ombaomba. Hii watu wamelithibitisha. Kwa hiyo acha kabisa ushabiki wa kipuuzi. Usitake kuchochea hasira za watu, bado tuna uchungu. Pambaf!
 
Yaliyotangazwa na bbc kwa mara ya kwanza ndio yenye ukweli. Lakini baadae taarifa ilipindishwa ikaonekana ni watu wawili, yu wapi mkenya aliyeuawa???
 
Back
Top Bottom