Ilianza balozi kutoa ONYO, likaja baraza la Congress, sasa Ikulu ya Marekani ila Kiburi, majivuno yatazaa Vikwazo vya kiuchumi kujiona sisi matajiri

Naomba tukumbushane hapa,

Balozi wa Marekani alishatoa maonyo mengi juu ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwemo hali ya demokrasia nchini, uhuru wa habari (Kabendela), mahakama kuingiliwa na kutotoa haki ikiwemo kubambikiziana kesi kwa vinogozi wa vyama pinzani, watu kupotea na kutekana, haki za watoto hasa wanaopata mimba mashuleni nk.

Ikaja baraza la Congress kumwandikia rais Magufuli mwezi Dec 2019 lakini sio Ikulu, wala wizara ya mambo ya nje iliyojibu kwa press kama walivyofanya hao wanaoitwa Mabeberu.

Jana Ikulu ya Marekani imeanza process ya kuwekea vikwazo watanzania na baadhi ya viongozi kuingia marekani ikiwa ni mwanzo wa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.

Huku kujimwambafy kunatuumiza hasa sie raia kwa viongozi wazembe ambao wanakula na kulala kwa kodi zetu.

Ifike kipindi tuwaambie zile ngojera za kiwa mabeberu wanatuonea wivu ni wivu gani wakati kila kitu kinatoka kwao kuanzia teknolojia hadi wafanyakazi wa hiyo miradi tunayojidai nayo?
Maskini jeuri huishia kula maneno yake mwenyewe. Sheria na kanuni zake tumezitunga sisi wenyewe, maazimio ya kimataifa tumeyaridhia sisi wenyewe, viapo vya kuitunza, kuiheshimu na kuitii katiba ya nchi yetu tulitoa nadhiri sisi wenyewe tena kwa kupitia imani zetu kwa kushika misahafu yetu kwa mikono yetu tukimalizia kwa kusema "Ee Mwenyezi Mungu na unisaidie"

Sasa hao mabeberu wanawasaidia viongozi wetu kukumbuka mambo hayo muhimu, kwa kuwa ni dhahiri inaonyesha ya kuwa wamekengeuka. Tuache kulalamika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni ubeberu tuu, wazalendo hatutakubali tutasimama na rais wetu Magufuli.



P

Wewe huoni haki za binadamu zinavyokandamizwa
Au umeamua tu uongee ujinga hapa
Nashangaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni ubeberu tuu, wazalendo hatutakubali tutasimama na rais wetu Magufuli.



P
Mkuu Pascal heshima yako.

Naomba nikuulize swali lakitoto (hope umenikubalia)

Una amini TANZANIA Inaweza kushindana na USA?

Distributed Denial-of-Service
 
Jana Ikulu ya Marekani imeanza process ya kuwekea vikwazo watanzania na baadhi ya viongozi kuingia marekani ikiwa ni mwanzo wa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.
Hatuwezi kufika huko! lile katazo ni kwa ajili ya hatua za kiusalama tu na bado linaweza kuondolewa muda wowote wakiona hamna tishio la ugaidi au uhalifu.
 
Huu ni ubeberu tuu, wazalendo hatutakubali tutasimama na rais wetu Magufuli.



P
Subiri yule profesa wa jalalani apigwe vikwazo sijui mtatoa wapi mtu mwingine wa kwenda kuongea kiingereza huko kwa mabeberu
 
Akili zako zinakutosha mwenyewe nyinyi muda ubavu gani wa kumdindia Marekani hivyo mnavyoikali ZANZIBAR kijeshi kwajiona tayari mshaitawala Dunia PAMBAFFF

Sent using Jamii Forums mobile app
Nmemshangaa sana huyu jamaa

Utafikiri haoni waandishi wenzake wanavyokandamizwa

Na sasa nmeamini

Labda ni spy wa TISS who knows

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona majina hujaweka mleta mada?

Halafu hivi unaweza muwekea vikwazo vya mtu kutoingia nchini kwako mtu asiyesafiri na asiye na mpango wa kuja nchini kwako?
Hili swali huwa najiuliza sana.
Baadae nikajipa majibu kuwa inawezekena wale wanaowekewa vikwazo niwale walioficha pesa huko

God save us
 
Endeleeni kuota, juzi tu umoja wa Ulaya na Us,Uk wametoa bil 230+ kusaidia mambo ya elimu.
(Reuters) - The Trump administration is planning to add seven countries - Belarus, Eritrea, Kyrgyzstan, Myanmar, Nigeria, Sudan and Tanzania - to its travel ban list, U.S. media reports said on Tuesday.
 
Huu ni ubeberu tuu, wazalendo hatutakubali tutasimama na rais wetu Magufuli.



P
Kumtetea mtoto wetu mpendwa Zimbabwe afunguliwe imekuwa ukosefu wa adabu. Haya bana ni bora tuitikie nyimbo za China na Mrusi. Hakuna namna
 
Huu ni ubeberu tuu, wazalendo hatutakubali tutasimama na rais wetu Magufuli.



P
alafu kiukweli sijaiona sababu ya msingi zaidi ya Uonevu na Ubabe tu, kana kwamba mfanye watakavyo wao
 
Vikwazo rasmi vitawekwa baada ya Jiwe kulazimisha ushindi wa asilimia 99.99%

Kabudi anapita huku na huko akiomba Zimbabwe iondolewe vikwazo kana kwamba yeye ni foreign minister wa Zimbabwe sasa atapata kazi rasmi ya kuiombea Tanzania iondolewe vikwazo
 
WASHINGTON—The Trump administration plans to add seven countries to a group of nations subject to travel restrictions, including Nigeria, Africa’s most populous country, along with others in Africa and Asia, according to administration officials who have seen the list.

The new restrictions would apply to travelers and immigrants from Belarus, Eritrea, Kyrgyzstan, Myanmar, Nigeria, Sudan *and Tanzania.* The countries wouldn’t necessarily face blanket bans on travel to the U.S., but could have restrictions placed on specific types of visas, such as business or visitor visas, administration officials said.

Some countries could be banned from participating in the diversity visa lottery program, which awards green cards to people in countries with low levels of immigration to the U.S. President Trump has called for an end to that program, saying it lets undesirable people into the U.S., and he has proposed reorienting the existing visa system toward skilled workers instead.

The officials said the list isn’t final, and on Tuesday the White House was still debating whether to include one or two of the countries.

The Department of Homeland Security didn’t respond to request for comment. The State Department declined to comment.


Read more Trump Administration Plans to Expand Travel Restrictions to Seven Countries

Sent using Jamii Forums mobile app
Good news,
 
Huu ni ubeberu tuu, wazalendo hatutakubali tutasimama na rais wetu Magufuli.



P
Maneno mepesi sana hayo ukilinganisha na mazingira ya dunia inavyo kwenda sasa.

Aidha umejibutu bora liende na kunakitu unachofikiri ila unashindwa tu kukielezea kwa upanawake kwa sababu flani flani.



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom