Ili uishi kwa amani ni vyema uwasaidie watu kulingana na kipato chako. Kukopesha fedha tuwaachie bank na microfinance

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,746
36,268
Mtu amepewa kadi za hharusi na send-off 5, na zote inabidi achangie kulipa fadhila.
VICOBA vitatu vyote anadaiwa, upatu unamtesa, tv ya mkopo, mpaka nguo za mkopo.
Akipata pesa anapunguza huku, anakopa kule anakula anaanza tena kukopa.
Utasikia nikopeshe laki tarehe 10 nakulipa unamwambia subiri mambo si mazuri. Inafika tarehe 11 anaomba tena umkopeshe. Unajiuliza si alisema tarehe 10 atakuwa na pesa , ina maana ningemkopesha siku ile tarehe aliyoniahidi ilikuwa ni tarehe hewa,.
Usipozingatia kwenye suala la misaada, michango na kukopesha utaishia kuwa maskini
 
Kuna watu wanakopa huku wakijua kabisa hawana mpango wa kulipa deni au watalipa baada ya kukuzungusha sana. Tarehe wanayotoa ya kurudisha mkopo huwa ni "hewa".
 
kuna mmoja nilimkopesha kajikausha kabisa, sasa kila akija kukopa tena namkumbushia deni langu anaondoka bila kuaga.
 
Back
Top Bottom