Ili Tanzania ipone, ni Lazima CCM ife

Ili Tanzania ipone, ni Lazima CCM ife

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
19,488
Reaction score
26,109
Hii kazi inayo endelea ya kuikomboa Tanzania kutoka katika mikono ya waovu; Samia na Genge lake ni muhimu; lakini haitatosha kuleta mabadiliko chanya endapo CCM kama chama itaendelea kuwepo.

Kutokana na muundo wake na mfumo wa uendeshaji wa shughuli zake CCM daima itaendelea kuwa ni adui mkubwa wa nchi.

Nitaeleza maana yangu kwa mifano miwili:
Uongozi wa John Magufuli ulipoingia kuongoza nchi chini ya kiongozi huyo; chama kiligeuka kuwa kama ni mali yake na kukiendesha kama alivyopenda mwenyewe. Alitumia muundo wa chama hicho kupitisha yote aliyotaka yeye yafanyike.

Alipochukua hatamu Samia Suluhu Hassan, na yeye kachukua mtindo huo huo wa Magufuli kukitumia chama alivyo penda mwenyewe. Tofauti kidogo ikawa ni kuwaingiza Genge kushika hatamu za chama. Kwa hiyo chama sasa kinatumika kutimiza matakwa ya Samia na Genge lake.

Sasa je, tunaweza kubahatisha akatokea kiongozi mwenye nguvu ndani ya chama hicho na kukirudisha kwa wanachama wake na waTanzania kwa jumla?

Kiongozi wa namna hiyo katika hao wote waliomo ndani ya chama hicho sasa hivi simwoni; na pengine atakakuwa bado hajazaliwa! Kwani ukitazama hata hao UVCCM waliopo sasa wote wanapigana vibega tu kusaka maslahi binafsi.

Kesho Oktoba 29, twende tukatimize wajibu wetu wa mwanzo katika juhudi za kukipumzisha hiki chama ili Tanzania IPUMUE.
 
Unfortunately haifi sasa.
 
Juzi nchini Ireland alipatikana raisi ambae ni mgombea binafsi aitwae Catherine Connolly kwa asilimia 64.

Ni hadi hapo itakapopatikana nafasi ya kubadilishwa katiba na moja ya maingizo ni wagombea binafsi ambao wana sifa lakini si lazima watokee katika chama tawala.

Mgombea binafsi ambae atakuwa ni wa watanzania wote wataomkubali atafaa sana kuongoza nchi kama yetu yenye mgawanyiko ulotokana na tamaa na roho mbaya.
 
Mzee kalamu kwa umri wako ni bora utulie nyumbani unywe vidonge vyako vya presha kwa amani, machafuko unayotamani yakitokea hutatoboa hata nusu saa
 
Weye wafahamu vipi kama Kalamu atumia vidonge vya Pressure?

Au wamtania tu?
 
Mie hapa nina furaha kubwa sana, kuiona Tanzania isiyo na wahuni wenye nguvu na maamuzi tena, imefika.. CCM yenyewe yaenda paranganyika mazima
 
Unfortunately haifi sasa.
Hilo neno "unfortunately", halina uzito wowote wa kuzuia CCM kufa..
Mnaoitegemea CCM maishani mwenu inabidi mjiandae tu na shughuli nyingine za kuendesha maisha yenu.
 
Mzee kalamu kwa umri wako ni bora utulie nyumbani unywe vidonge vyako vya presha kwa amani, machafuko unayotamani yakitokea hutatoboa hata nusu saa
Wewe unadhani kwa umri wako huo unastahili kuwa "kafala" kwa mtu mwingine yeyote?
Kwa umri wako wewe na yeye siyo ajabu kutumia vidonge vya presha
Huna lolote ujualo kuhusu "ugonjwa wa presha", lakini kwa vile wewe ni nguruwe mfugwaji tu, huoni shida yoyote kuzungumzia usichokijuwa! Kama unavyozungumzia umri wangu kama wewe ndiye umenizaa!
 
Ikitokea CCM ikaondolewa madarakani kwa njia yoyote ile, itamsumbua sana atakayekuwa anatawala kwa kutumia watu na mifumo iliyokuwa imejiwekea na iliyoifaidisha kwa muda mrefu.

Siku hiyo ikija, kiongozi mpya atalazimika kubomoa na kujenga upya kila mfumo uliopo kuanzia wa kipolisi, mahakama, elimu, mifumo ya kisiasa kama Tume ya Uchaguzi na Msajili wa Vyama, vyama na timu za michezo, vyama vya wafanyakazi, nk. Kazi itakuwa kubwa sana.

Bila kufanya hivyo watamuendesha na kumtikisa hadi aombe poo.

Mimi nalilia ukosefu wa dhamira ya kweli ya kukubali mfumo wa kidemokrasia wa vyama vingi. Bila CCM kukubali mfumo huu kwa moyo mmoja, yote ni kazi bure na Tanzania itaendelea kupata tabu sana.
 
Hii kazi inayo endelea ya kuikomboa Tanzania kutoka katika mikono ya waovu; Samia na Genge lake ni muhimu; lakini haitatosha kuleta mabadiliko chanya endapo CCM kama chama itaendelea kuwepo.

Kutokana na muundo wake na mfumo wa uendeshaji wa shughuli zake CCM daima itaendelea kuwa ni adui mkubwa wa nchi.

Nitaeleza maana yangu kwa mifano miwili:
Uongozi wa John Magufuli ulipoingia kuongoza nchi chini ya kiongozi huyo; chama kiligeuka kuwa kama ni mali yake na kukiendesha kama alivyopenda mwenyewe. Alitumia muundo wa chama hicho kupitisha yote aliyotaka yeye yafanyike.

Alipochukua hatamu Samia Suluhu Hassan, na yeye kachukua mtindo huo huo wa Magufuli kukitumia chama alivyo penda mwenyewe. Tofauti kidogo ikawa ni kuwaingiza Genge kushika hatamu za chama. Kwa hiyo chama sasa kinatumika kutimiza matakwa ya Samia na Genge lake.

Sasa je, tunaweza kubahatisha akatokea kiongozi mwenye nguvu ndani ya chama hicho na kukirudisha kwa wanachama wake na waTanzania kwa jumla?

Kiongozi wa namna hiyo katika hao wote waliomo ndani ya chama hicho sasa hivi simwoni; na pengine atakakuwa bado hajazaliwa! Kwani ukitazama hata hao UVCCM waliopo sasa wote wanapigana vibega tu kusaka maslahi binafsi.

Kesho Oktoba 29, twende tukatimize wajibu wetu wa mwanzo katika juhudi za kukipumzisha hiki chama ili Tanzania IPUMUE.
Dini ni adui ya Africa. Dini za kuzungu ni ukoloni na ubeberu
 
Ni rahisi kuzilaumu dini; lakini sijawahi kusikia dini inayomcha Mungu ambaye anawabagua binaadam kwa misingi ya utofauti wao katika maswala mbalimbali.

Haya ya mitafaruku yanaibuka tu kwenye hizo dini kwa kuchochewa na makundi yenye misimamo hasi dhidi ya binaadam wengine.

Na haya sasa yanakolezwa sana huku kwetu Afika
 
Hawa watu wamekiri kwa vinywa vyao kwenye majukwaa ya kampeni, kuwa wanao uhalali kutoka kwa Mungu wa kutawala Tanzania.. there is no political solution to what Tanzania is facing
 
Mzee kalamu kwa umri wako ni bora utulie nyumbani unywe vidonge vyako vya presha kwa amani, machafuko unayotamani yakitokea hutatoboa hata nusu saa
machafuko yapi tena ameyasema , ebu tuambie vzr mkuu
 
Back
Top Bottom