figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,895
Binafsi sitaki kumzungumzia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu kwai alivyopatikana kila mtu anajua.
Kuna watu ndani ya Nchi yetu ambao wakipewa nafasi kila mtu atapiga Saluti. Tanzania inahitaji watu waliokomaa kisiasa na wanaojua wajibu wao na miiko ya kiuongozi. Nikiangalia katika jeshi la Polisi, Mtu ambaye anaweza kuvaa hivi viatu vya IGP na akakubalika kwa kila mtu ni Kamanda Simon Siro.
Huyu mtu bwana muone hivi hivi. Ana Misimamo na hapelekeshwi bali huzingatia sheria. NI mtu anayejua kazi yake. Mimi nmeanza kumfahamu utendaji wake katika Operation Kimbunga.
Kwanza yupo karibu na watu, hadharau mkubwa wala mdogo, anamjua Mungu na anajua miiko ya kiuongozi. Ni mtu ambaye hana Kashifa ya Ufisadi na anauchukia Ufisadi.
Kamishna Simon Sirro amesema kitendo cha askari kunyang’anywa silaha na majambazi ni aibu na fedheha kwao na Jeshi la Polisi, akisema madhara yake yanaweza kuwa makubwa kwa jamii.
Ni mtu ambaye hapendi watu waonewe na ana huruma kwa Wananchi. Ni mtu anayeamin katika utii wa sheria bila shuruti na ndo Kauri mbiu yake.
Kwa wasio mjua Kamanda Siro, huyu ni Afande asiye na Tabaka na anayependa Miziki ya Bongo Freva. Huyu Kamishna Simon Sirro bwana, mimi nampenda sababu ana ushirikiano na Waandishi wa Habari Simon Siro, Huyu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, haogopi mtu. yeye malengo yake alitaka kuwa Padre sema ndo hivo maisha na Mlima kupanda na kushuka
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro Wakati anahojiwa na wandishi wa habari alisema ndoto yake ilikuwa kuwa Padri wa Kanisa Katoliki kabla ya kukatishwa na wazazi wake na kuamua kujiunga na jeshi hilo nchini.
Sirro ni kamanda wa 14 wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, aliteuliwa na Rais John Magufuli Februari 15, kushika wadhifa huo baada ya aliyekuwa kamanda wa kanda hiyo kuanzia mwaka 2008, Suleiman Kova kustaafu
“Unajua kama Mungu ameniweka hai na kunipa kazi sina cha kujutia. Wakati nikiwa kijana nilikulia katika maadili mazuri na kusoma seminari na sikuwa na mambo mengi sana labda najutia kutokuwa padri maana nilikuwa nimefikia hatua ya mbali sana.”
Kamanda Sirro ambaye ana sifa ya kuhamishiwa katika mikoa yenye matukio makubwa ya uhalifu na ujambazi, alipoulizwa sababu za kuacha upadri na kujiunga na Jeshi la Polisi alisema : “Ilikuja tu nikajikuta nimebadilisha mawazo, lakini kikubwa ilikuwa wazazi. Unajua wazazi kule kwetu Musoma ilikuwa hawakuelewi usipooa.”
Kamanda Sirro ambaye amewahi kuwa Kamanda wa polisi katika mikoa ya Tanga, Shinyanga na Mwanza alieleza jinsi alivyoweza kubadilika kutoka katika mtizamo na maadili ya kujiandaa kuwa padri hadi kuingia polisi.
“Fikiria zile amri kuu za Mungu. Kama unakuwa padri si ndiyo unasimamia hizo. Unaniuliza niliwezaje kubadilika sasa kama ukiwa padri mtu akivunja amri hizo unamfanyaje?” alihoji Sirro ambaye alieleza kuwa anapenda zaidi kusikiliza nyimbo za kanisa hilo.
“Lazima mtu uendane na wakati na mazingira yaliyopo. Ningekuwa padri mngekuja kunitembelea na kukuta chumba changu kina misalaba na pengine mngeshindwa hata kunihoji.”
Si jambo zuri kumpongeza mtu kwa mauaji, lakini kwa mauaji ya wahalifu, tena ambao walitoa roho za watu wasio na hatia mimi nadhani hili halina mjadala. Kamanda Siro naweza kusema kwa kasi yake, naanza kuamini kwanini watu wengi pamoja nami tunakuita Kamanda.
Naamini sasa umewaeleza askari unataka watu waishi kwa amani na wanaofanya biashara wafanye biashara pasipo hofu, na palipo na mianya ya uhalifu, unaishugulikia kwa kutokomeza kabisa magenge hayo.
Miaka fulani hapo nyuma tulikuwa tukisikia kuwa majambazi wameiba na kutokomea kusikojulikana wakiwa na pikipiki, lakini hivi sasa askari wale wale ambao walikuwa nao wakifanya kazi ya doria kwa kutumia pikipiki na magari, ndio hao hao sasa hivi wanakula sahani moja na majambazi na kufanikiwa ama kuwakamata hai au wafu.
Si tu kuwakamata majambazi, lakini pia tunashuhudia upatikanaji wa silaha ambazo majambazi hawa walikuwa wakizitumia. Vyema sasa makamanda wa mikoa mingine, nao wakaiga kazi hii inayofanywa na Afande Siro.
Kwani watu wachache wanamuangusha sababu ya vyeo vyao. Tumpe nafasi Kamanda Siro aongoze jeshi letu, Ni mtu mwenye plan ya Kazi zake na kafanyi kazi ili asifiwe.
Ni wakati wa Kanda Sirro. Twende na Wakati