KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 30,290
- 69,596
Habari wakuu..
Sote twafahamu kwamba "umoja ni nguvu utengano ni udhaifu", ni jambo zuri nchi za Afrika kujiunga na kuwa kama nchi moja lakini jambo hili litawezekana kama tukiuondoa ukoloni mamboleo!
Bila kufanya hivi mataifa yenye nguvu yanayoshikilia ukoloni mambo leo yatatuletea shida na kuhakikisha jambo hili halifanikiwi hata kidogo, lazima watatia doa ilimradi kutia chungu na huenda wakaleta utenganifu maradufu ya uliopo.
Ili kuhakikisha umoja wa afrika unakuwa imara lazima kila nchi ya Afrika ihakiki haina chembe ya ukoloni mamboleo, udini,ukabila n.k
Jambo hili la kuondoa ukoloni mamboleo litatusaidia kujisimamia kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Kazi haipo kwenye kuungana, kazi ipo kwenye kuondoa dubwasha hili lililokubuhu(ukoloni mamboleo)
Huenda itatugharimu kutoa kizingiti hiki, lakini itatubidi kupambana maana linatufedhehesha na kutudumaza.
Inaniuma kila siku afrika ndo inabeba umaskini,magonjwa,ujinga,utumwa,vita n.k
Mimi yangu ni hayo tu.
sijui wadau wenzangu mnalizungumziaje hili swala..?