Kama nitakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

VMWare-Oracle

JF-Expert Member
Dec 19, 2021
663
910
Habari zenu wana JF. Moja kwa moja kwenye mada;

Kulingana na maono yangu kuhusiana na suala la maendeleo katika jamii ya watu wa Tanzania, naona asilimia kubwa ya watu wamesahau kitu ambacho waasisi wetu wa taifa walikua wamekiacha kama kifaa cha kuleta maendeleo. Mnamo mwaka 1967 kulikuwa na azimio la Arusha kuhusiana na siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Siasa ya ujamaa na kujitegemea ililenga serikali kutumikia wananchi wake na watu katika jamii kusaidiana.Kila mtu kuweza kubuni fursa zitakazo tatua changamoto za kijamii.

Ni dhahiri kwamba waasisi wa taifa walikua na maono mazuri lakini walishindwa kubuni njia sahihi na nzuri za kuleta maendeleo. Hata sasa tunajua ya kuwa Mtanzania anaweza akatoa wazo zuri kwelikweli ambalo litatatua changamoto za kijamii, lakini hawawezeshwi kufikia ndoto zao.

Swali la msingi Watanzania wenzangu: Katika miaka 60 ya uhuru je Tanzania inafanya siasa ya ujamaa na kujitegemea au imebadilisha mlengo na kuingia katika siasa ya ubepari pasipo kuwa na azimio lolote lile?

Kama nitakua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania;

Nitakuwa moja ya viongozi wanaopinga siasa ya vyama vingi. Siasa ya vyama vingi ni siasa ya kibepari. Ili Tanzania iweze kuendelea ni lazima wote tuwe na malengo sawa na sawia.Nitavunja vyama vyote vya siasa(kuanzia kile nitakachokitumikia mpaka vile vya upinzani). Chama kipya cha taifa kitaundwa ambacho kitachukua viongozi na sio watawala. Yoyote yule aliye Mtanzania na mzalendo atajiunga pasipo kuangalia chama chake alichokitumikia hapo kabla. Nia ya kufanya hivyo ni kuwa na malengo sawa ya kimaendeleo hivyo kuhamasisha shauri na sio kupakaziana mabaya.

Mnamo mwaka 1944, Bretton Woods Institutions:IMF,WB ziliundwa nchini Marekani kwa lengo la kusaidia nchi za Ulaya kujijenga kiuchumi baada ya vita vya pili vya dunia. Lakini mnamo mwaka 1980 mlengo ulibadilika na kuhamia Afrika kwa kile walichokiita mpango wa kuondoa umasikini bara la Afrika.Ukoloni mambo-leo ukazaliwa na kuota mizizi katika ardhi ya bara la Afrika.

Zile SAP's ndizo chanzo kikuu cha ukoloni mambo-leo.Natumaini mnazijua SAP's pamoja na kanuni(principles) zake.

Leo hii watu wanaiita Marekani, mama wa demokrasia ilhali hiyo demokrasi yao imeleta mashoga(kwa misingi ya mtu kufanya chochote anachokitaka*Sisi Watanzania hatuna tamaduni hii na hatuwezi ikubali), imeshindwa kufuta ubaguzi wa rangi, maandamano ambayo jeshi la polisi limetumia nguvu ilhali watu wanasema ukweli, watu kuvamia bunge, masikini kukosa malazi(homeless) n.k.

Ukweli ni huu:wakati utafika Tanzania kuwa na demokrasia yake ambayo itaendana na mahitaji ya watu wake.Je panaweza kuwa na demokrasia ilhali chama cha siasa ni kimoja?Jibu langu ni ndiyo.Hili taifa kwa sasa halina enzi kuu(sovereignty) kwa sababu kuna viongozi ambao ni vibaraka wa nchi za kibepari na hutumia siasa ya vyama vingi kama chaka la kuficha maovu yao.

Siasa ya ujamaa na kujitegemea ndiyo siasa pekee itakayoleta elimu bure,matibabu bure,uwajibikaji,uzalendo,ubunifu,uwezeshaji,umoja,upendo,amani,maisha yenye kipato kizuri kwa kila Mtanzania.Ila kama tutaendelea kwa njia hii ya kutegemea uwekezaji kutoka nje(ubepari) mafarakano kati ya mkulima na mwekezaji,mfugaji na mwekezaji,mchimba madini na mwekezaji hajataisha na nchi haitokuja kuendelea.

Kwa nini nchi haitokuja kuendelea?Jibu:kwa sababu wawekezaji wa nje ni lazima wachukue asilimia kubwa katika magawio ilo kupata faida.Sasa kumbuka wakati wao wanachukua faida kujenga nchi zao vilevile sisi tunapata faida lakini yenye hasara,kwa nini?Jibu:Kwa sababu sisi hatuna wawekezaji wakubwa katika nchi za kigeni hususani Ulaya na Marekani hivyo hatuchukui faida kutoka kwao.Wakati sisi tunapiga hatua moja wale wanapiga hatua mia moja.Sasa tutawafikia lini?Au kwenye ndoto?Hii nchi inavyoendeshwa kuelekea maendeleo ni kana kwamba nchi nyingine zimelala!!

Kama nitakua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.....
 
Mawazo ya kizamani kabisa haya! Ujamaa ulishindwa dunia na mbinguni! Leo hii bado tu unatamani kuwa Rais chini ya mfumo mfu wa Ujamaa!

Ujamaa ni mfumo wa kinafiki wa kuwanufaisha viongozi wachache, huku wananchi walio wengi wakiishi maisha ya kutaabika.

Ningekuunga mkono kama ungeifuta ccm baada ya kuwa Rais! na hivyo kuruhusu uwanja sawa wa watu kufanya demokrasia. Maana matatizo yote ndani ya nchi hii; kuanzia ya kijamii, kiuchumi na pia kisiasa! Chanzo ni ccm na sera zake mbovu.
 
Siasa ya ujamaaa ndio iliyotufikisha hapa tulipo mkuu. La sivyo labda tungekuwa tumepiga hatua zaidi.
Ngoja nianze na wewe.Siasa ya ujamaa ilikufa pale Mh.Hussein Ali Mwinyi aliposhika nchi na kuanzisha mfumo wa kila kitu 'ruksa'.

Mkuu mikopo ilinza kwa Mwinyi na kaa ukijua mfumo wa kuchukua mikopo ni wa kibepari chini ya Bretton Woods Institutions. Moja ya sababu Mwl.J.K.Nyerere kung'atuka(kujiuzulu/kuachia ngazi) ni shinikizo la mikopo baada ya kushindwa kutafuta mbinu sahihi za kijamii.

Hapa tulipo ni kwa sababu ya ubepari tangu enzi za mwinyi mnasingizia ujamaa kwa sababu hapakua na azimio lolote lile la ubepari lakini jinsi mfumo wa nchi inavyoendeshwa ni wakibepari. Ndio maana nikatanguliza kama mnajua SAP's
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mawazo ya kizamani kabisa haya! Ujamaa ulishindwa dunia na mbinguni! Leo hii bado tu unatamani kuwa Rais chini ya mfumo mfu wa Ujamaa!
Ujamaa ni mfumo wa kinafiki wa kuwanufaisha viongozi wachache, huku wananchi walio wengi wakiishi maisha ya kutaabika.

Ningekuunga mkono kama ungeifuta ccm baada ya kuwa Rais! na hivyo kuruhusu uwanja sawa wa watu kufanya demokrasia. Maana matatizo yote ndani ya nchi hii; kuanzia ya kijamii, kiuchumi na pia kisiasa! Chanzo ni ccm na sera zake mbovu.
Ujamaa ulishindwa duniani? Hivyo Urusi na China zipo ulimwengu upi?
Sema waasisi wa ujamaa walishindwa na sio ujamaa ulishindwa.

Ndugu kaa ukijua unafiki, umasikini na uwepo wa matabaka ni kwa sababu ya ubepari na nishasema nchi hii ilishaanza ongozwa kibepari tangu enzi za Mwinyi tatizo nikwamba hapakukua na azimio hivyo watu wanadhani tunaongozwa chini ya ujamaa.

Kwa lugha rahisi rejea katika kamusi ya kiswahili maneno haya:ujamaa, ubepari.Hapa utaelewa kua uozo huu wote ni kwa sababu nchi inaongozwa kibepari chini ya mwavuli wa ujamaa.
 
Ujamaa ulishindwa duniani?Hivyo Urusi na China zipo ulimwengu upi?

Ujamaa wa China ulikufa mwanzoni mwa miaka ya 1970's baada ya vifo vya waasisi wa huo ujamaa, akina Mao Ze Dong na wenzake.

Na ujamaa wa USSR ( na hiyo Urusi ikiwa ndani) ulijisifia mwanzoni mwa miaka ya 1990's baada ya kuanguka kwa hilo Shirikisho la Kisoviet. Kinachotokea China na Urusi kwa sasa siyo ujamaa unao ufahamu wewe! Ule ubepari ulio jificha kwenye huo ujamaa wa uongo.
 
Habari zenu wana JF. Moja kwa moja kwenye mada;

Kulingana na maono yangu kuhusiana na suala la maendeleo katika jamii ya watu wa Tanzania, naona asilimia kubwa ya watu wamesahau kitu ambacho waasisi wetu wa taifa walikua wamekiacha kama kifaa cha kuleta maendeleo. Mnamo mwaka 1967 kulikuwa na azimio la Arusha kuhusiana na siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Siasa ya ujamaa na kujitegemea ililenga serikali kutumikia wananchi wake na watu katika jamii kusaidiana.Kila mtu kuweza kubuni fursa zitakazo tatua changamoto za kijamii.

Ni dhahiri kwamba waasisi wa taifa walikua na maono mazuri lakini walishindwa kubuni njia sahihi na nzuri za kuleta maendeleo.Hata sasa tunajua ya kuwa Mtanzania anaweza akatoa wazo zuri kwelikweli ambalo litatatua changamoto za kijamii, lakini hawawezeshwi kufikia ndoto zao.

Swali la msingi Watanzania wenzangu:Katika miaka 60 ya uhuru je Tanzania inafanya siasa ya ujamaa na kujitegemea au imebadilisha mlengo na kuingia katika siasa ya ubepari pasipo kuwa na azimio lolote lile?

Kama nitakua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania;

Nitakuwa moja ya viongozi wanaopinga siasa ya vyama vingi. Siasa ya vyama vingi ni siasa ya kibepari. Ili Tanzania iweze kuendelea ni lazima wote tuwe na malengo sawa na sawia.Nitavunja vyama vyote vya siasa(kuanzia kile nitakachokitumikia mpaka vile vya upinzani).Chama kipya cha taifa kitaundwa ambacho kitachukua viongozi na sio watawala.Yoyote yule aliye Mtanzania na mzalendo atajiunga pasipo kuangalia chama chake alichokitumikia hapo kabla.Nia ya kufanya hivyo ni kuwa na malengo sawa ya kimaendeleo hivyo kuhamasisha shauri na sio kupakaziana mabaya.

Mnamo mwaka 1944, Bretton Woods Institutions:IMF,WB ziliundwa nchini Marekani kwa lengo la kusaidia nchi za Ulaya kujijenga kiuchumi baada ya vita vya pili vya dunia.Lakini mnamo mwaka 1980 mlengo ulibadilika na kuhamia Afrika kwa kile walichokiita mpango wa kuondoa umasikini bara la Afrika.Ukoloni mambo-leo ukazaliwa na kuota mizizi katika ardhi ya bara la Afrika.

Zile SAP's ndizo chanzo kikuu cha ukoloni mambo-leo.Natumaini mnazijua SAP's pamoja na kanuni(principles) zake.

Leo hii watu wanaiita Marekani,mama wa demokrasia ilhali hiyo demokrasi yao imeleta mashoga(kwa misingi ya mtu kufanya chochote anachokitaka*Sisi Watanzania hatuna tamaduni hii na hatuwezi ikubali),imeshindwa kufuta ubaguzi wa rangi,maandamano ambayo jeshi la polisi limetumia nguvu ilhali watu wanasema ukweli,watu kuvamia bunge,masikini kukosa malazi(homeless) n.k.

Ukweli ni huu:wakati utafika Tanzania kuwa na demokrasia yake ambayo itaendana na mahitaji ya watu wake.Je panaweza kuwa na demokrasia ilhali chama cha siasa ni kimoja?Jibu langu ni ndiyo.Hili taifa kwa sasa halina enzi kuu(sovereignty) kwa sababu kuna viongozi ambao ni vibaraka wa nchi za kibepari na hutumia siasa ya vyama vingi kama chaka la kuficha maovu yao.

Siasa ya ujamaa na kujitegemea ndiyo siasa pekee itakayoleta elimu bure,matibabu bure,uwajibikaji,uzalendo,ubunifu,uwezeshaji,umoja,upendo,amani,maisha yenye kipato kizuri kwa kila Mtanzania.Ila kama tutaendelea kwa njia hii ya kutegemea uwekezaji kutoka nje(ubepari) mafarakano kati ya mkulima na mwekezaji,mfugaji na mwekezaji,mchimba madini na mwekezaji hajataisha na nchi haitokuja kuendelea.

Kwa nini nchi haitokuja kuendelea?Jibu:kwa sababu wawekezaji wa nje ni lazima wachukue asilimia kubwa katika magawio ilo kupata faida.Sasa kumbuka wakati wao wanachukua faida kujenga nchi zao vilevile sisi tunapata faida lakini yenye hasara,kwa nini?Jibu:Kwa sababu sisi hatuna wawekezaji wakubwa katika nchi za kigeni hususani Ulaya na Marekani hivyo hatuchukui faida kutoka kwao.Wakati sisi tunapiga hatua moja wale wanapiga hatua mia moja.Sasa tutawafikia lini?Au kwenye ndoto?Hii nchi inavyoendeshwa kuelekea maendeleo ni kana kwamba nchi nyingine zimelala!!

Kama nitakua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.....
Mkuu, housegirl anaumwa, katoe vyombo mezani halafu ufagie uwanja
 
Ujamaa wa China ulikufa mwanzoni mwa miaka ya 1970's baada ya vifo vya waasisi wa huo ujamaa, akina Mao Ze Dong na wenzake.

Na ujamaa wa USSR ( na hiyo Urusi ikiwa ndani) ulijisifia mwanzoni mwa miaka ya 1990's baada ya kuanguka kwa hilo Shirikisho la Kisoviet. Kinachotokea China na Urusi kwa sasa siyo ujamaa unao ufahamu wewe! Ule ubepari ulio jificha kwenye huo ujamaa wa uongo.
Mkuu ushaidi wangu ni huu:China inatoa matibabu bure kwa wazee. Je Marekani inatoa?

Urusi imewajengea watu wasio na malazi(homeless), lockers za kuweka mizigo yao. Je homeless people wa Marekani hawalali juu ya mifuko ya rambo yenye mizigo yao?

Marekani usipokua na uwezo wa kifedha you are nothing ila China usipokua na uwezo wa kifedha utatafutiwa karama yoyote ile hata ya kujenga fly overs za Tanzania, kutengeneza saa za 1000/= na kuzitupia Afrika.

Mkuu toa ushaidi wako unaosadifu huo ubepari(nadhani unaelewa maana ya ubepari).
 
Kwanza huelewei demokrasia ni nini.
Demokrasia ni moja tu duniani kote na misingi na kanuni zake ni zile zile duniani kote.
Habari zenu wana JF. Moja kwa moja kwenye mada;

Kulingana na maono yangu kuhusiana na suala la maendeleo katika jamii ya watu wa Tanzania, naona asilimia kubwa ya watu wamesahau kitu ambacho waasisi wetu wa taifa walikua wamekiacha kama kifaa cha kuleta maendeleo. Mnamo mwaka 1967 kulikuwa na azimio la Arusha kuhusiana na siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Siasa ya ujamaa na kujitegemea ililenga serikali kutumikia wananchi wake na watu katika jamii kusaidiana.Kila mtu kuweza kubuni fursa zitakazo tatua changamoto za kijamii.

Ni dhahiri kwamba waasisi wa taifa walikua na maono mazuri lakini walishindwa kubuni njia sahihi na nzuri za kuleta maendeleo.Hata sasa tunajua ya kuwa Mtanzania anaweza akatoa wazo zuri kwelikweli ambalo litatatua changamoto za kijamii, lakini hawawezeshwi kufikia ndoto zao.

Swali la msingi Watanzania wenzangu:Katika miaka 60 ya uhuru je Tanzania inafanya siasa ya ujamaa na kujitegemea au imebadilisha mlengo na kuingia katika siasa ya ubepari pasipo kuwa na azimio lolote lile?

Kama nitakua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania;

Nitakuwa moja ya viongozi wanaopinga siasa ya vyama vingi. Siasa ya vyama vingi ni siasa ya kibepari. Ili Tanzania iweze kuendelea ni lazima wote tuwe na malengo sawa na sawia.Nitavunja vyama vyote vya siasa(kuanzia kile nitakachokitumikia mpaka vile vya upinzani).Chama kipya cha taifa kitaundwa ambacho kitachukua viongozi na sio watawala.Yoyote yule aliye Mtanzania na mzalendo atajiunga pasipo kuangalia chama chake alichokitumikia hapo kabla.Nia ya kufanya hivyo ni kuwa na malengo sawa ya kimaendeleo hivyo kuhamasisha shauri na sio kupakaziana mabaya.

Mnamo mwaka 1944, Bretton Woods Institutions:IMF,WB ziliundwa nchini Marekani kwa lengo la kusaidia nchi za Ulaya kujijenga kiuchumi baada ya vita vya pili vya dunia.Lakini mnamo mwaka 1980 mlengo ulibadilika na kuhamia Afrika kwa kile walichokiita mpango wa kuondoa umasikini bara la Afrika.Ukoloni mambo-leo ukazaliwa na kuota mizizi katika ardhi ya bara la Afrika.

Zile SAP's ndizo chanzo kikuu cha ukoloni mambo-leo.Natumaini mnazijua SAP's pamoja na kanuni(principles) zake.

Leo hii watu wanaiita Marekani,mama wa demokrasia ilhali hiyo demokrasi yao imeleta mashoga(kwa misingi ya mtu kufanya chochote anachokitaka*Sisi Watanzania hatuna tamaduni hii na hatuwezi ikubali),imeshindwa kufuta ubaguzi wa rangi,maandamano ambayo jeshi la polisi limetumia nguvu ilhali watu wanasema ukweli,watu kuvamia bunge,masikini kukosa malazi(homeless) n.k.

Ukweli ni huu:wakati utafika Tanzania kuwa na demokrasia yake ambayo itaendana na mahitaji ya watu wake.Je panaweza kuwa na demokrasia ilhali chama cha siasa ni kimoja?Jibu langu ni ndiyo.Hili taifa kwa sasa halina enzi kuu(sovereignty) kwa sababu kuna viongozi ambao ni vibaraka wa nchi za kibepari na hutumia siasa ya vyama vingi kama chaka la kuficha maovu yao.

Siasa ya ujamaa na kujitegemea ndiyo siasa pekee itakayoleta elimu bure,matibabu bure,uwajibikaji,uzalendo,ubunifu,uwezeshaji,umoja,upendo,amani,maisha yenye kipato kizuri kwa kila Mtanzania.Ila kama tutaendelea kwa njia hii ya kutegemea uwekezaji kutoka nje(ubepari) mafarakano kati ya mkulima na mwekezaji,mfugaji na mwekezaji,mchimba madini na mwekezaji hajataisha na nchi haitokuja kuendelea.

Kwa nini nchi haitokuja kuendelea?Jibu:kwa sababu wawekezaji wa nje ni lazima wachukue asilimia kubwa katika magawio ilo kupata faida.Sasa kumbuka wakati wao wanachukua faida kujenga nchi zao vilevile sisi tunapata faida lakini yenye hasara,kwa nini?Jibu:Kwa sababu sisi hatuna wawekezaji wakubwa katika nchi za kigeni hususani Ulaya na Marekani hivyo hatuchukui faida kutoka kwao.Wakati sisi tunapiga hatua moja wale wanapiga hatua mia moja.Sasa tutawafikia lini?Au kwenye ndoto?Hii nchi inavyoendeshwa kuelekea maendeleo ni kana kwamba nchi nyingine zimelala!!

Kama nitakua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.....
 
Ujamaa ulishindwa duniani?Hivyo Urusi na China zipo ulimwengu upi?
Sema waasisi wa ujamaa walishindwa na sio ujamaa ulishindwa.
Ndugu kaa ukijua unafiki, umasikini na uwepo wa matabaka ni kwa sababu ya ubepari na nishasema nchi hii ilishaanza ongozwa kibepari tangu enzi za Mwinyi tatizo nikwamba hapakukua na azimio hivyo watu wanadhani tunaongozwa chini ya ujamaa.

Kwa lugha rahisi rejea katika kamusi ya kiswahili maneno haya:ujamaa, ubepari.Hapa utaelewa kua uozo huu wote ni kwa sababu nchi inaongozwa kibepari chini ya mwavuli wa ujamaa.
Taja nchi tatu tu za kijamaa leo hii.
 
Kwanza huelewei demokrasia ni nini.
Demokrasia ni moja tu duniani kote na misingi na kanuni zake ni zile zile duniani kote.
Kwanza mkuu unamuaibisha the great thinker, Albert Einstein.

Wasema demokrasia ni moja?Hivi nikuulize kwanza demokrasia ilianzia wapi?
 
Urusi,China,Korea kaskazini na washirika wao wengine wa eastern block.
Urusi na China sio nchi za kijamaa, Korea Kaskazini ni nchi ya ujamaa uchwara ambayo Kiduku na kikundi chake kidogo wanatumia mkono wa chuma kunyonya jasho la raia watawaliwa waliobaki mafukara na skelton tupu.
 
Naomba ushaidi? Kuna Uzi pia hapa JF una haya maudhui. Sijawahi elewa kwa nini masikio yenu yapo sensitive kumsikiliza Mmarekani. Kwanza naomba ushaidi alafu niambie China inaongozwa na chama gani, je kuna vyama vingapi, na sera zao ni zipi? Sasa tuone hizo sera ni za kijamaa au kibepari. Vilevile toa ushaidi kwamba sera za urusi ni za kibepari.

Vilevile nitajie rank ya North Korea kiuchumi duniani? Nanitolee ushaidi wa picha unaoonyesha umasikini wa nchi hiyo.Kama umetanguliza sikio kabla ya jicho basi hakuna unachojua maana utaishia kusema: mara kuna mtu alitoroka akahojiwa UN...., mara wanawake wananyanyaswa, maneno kibao pasipo ushaidi wa picha ni ubatili
 
Naomba ushaidi?Kuna Uzi pia hapa JF una haya maudhui.Sijawahi elewa kwa nini masikio yenu yapo sensitive kumsikiliza Mmarekani.Kwanza naomba ushaidi alafu niambie China inaongozwa na chama gani,je kuna vyama vingapi,na sera zao ni zipi?Sasa tuone hizo sera ni za kijamaa au kibepari.Vilevile toa ushaidi kwamba sera za urusi ni za kibepari.

Vilevile nitajie rank ya North Korea kiuchumi duniani?Nanitolee ushaidi wa picha unaoonyesha umasikini wa nchi hiyo.Kama umetanguliza sikio kabla ya jicho basi hakuna unachojua maana utaishia kusema:mara kuna mtu alitoroka akahojiwa UN....,mara wanawake wananyanyaswa,maneno kibao pasipo ushaidi wa picha ni ubatili
 
Back
Top Bottom