Ili kurudisha Uzalendo, Media zote nchini ziwe zinaungana na TBC katika kupata Habari. Iwe ni LAZIMA kufuatilia

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,685
11,988
Hiki kizazi kilichozaliwa TANU haipo, wameikuta CCM tu wengi hawana uzalendo
Namaanisha waliozaliwa kuanzia 1977 kuja juu wengi hawana Elimu ya uzalendo

Ili kuepusha kizazi kisichokuwa na maadili muhimu kuwe na vipindi vya t.v. na redio angalau saa moja kwa siku ili vijana wafundishwe uzalendo
Iwe ni lazima kusikiliza au kuangalia,Hii itafanya Vijana wengi wawe na sprit ya uzalendo km enzi za Baba wa Taifa mwalimu Nyerere

Unawaona wachina,wakorea,wajapan walivyo na utii na heshima kwa Nchi yao ni Kwasababu ya vipindi mbali mbali vinavyorushwa kuwajenga kimaadili vijana na ni lazima kufuatilia toka wakiwa watoto hadi wanakuwa

Ndio maana sio rahisi kusikia mjapan au mkorea anaitukana na kuidhihaki Nchi yake

Wizara ya michezo na utamaduni ipeleke mswaada bungeni ili kutengeneza Vijana wenye maadili tofauti na hawa wa sasa waliokosa nidhamu na heshima
 
Viongozi wenyewe hawana uzalendo alafu hizo nchi unazozizungumzia wanamisingi imara sana ya kiuzalendo, Tz bado hatuna elimu ya vyama vingi na uzalendo pia.
 
Ni muda sana sijasikiliza media za Tanzania.

Nyingi zina shabaha ya kutu brainwash.Nyingi ni za kusifu juhudi za awamu ya tano.Zingine zilizobaki ni za kilokole.

MEDIA za tanzania haziruhusu midaholo ya watu wenye mawazo tofauti.

Binafsi napenda kusikiliza VOA , BBC na DW ingawa najua ata hizi zitakuja kupigwa marufuku siku za usoni.
 
Hiki kizazi kilichozaliwa TANU haipo, wameikuta Ccm tu wengi hawana uzalendo
Namaanisha waliozaliwa kuanzia 1977 kuja juu wengi hawana Elimu ya uzalendo

Ili kuepusha kizazi kisichokuwa na maadili muhimu kuwe na vipindi vya t.v. na redio angalau saa moja kwa siku ili vijana wafundishwe uzalendo
Iwe ni lazima kusikiliza au kuangalia,Hii itafanya Vijana wengi wawe na sprit ya uzalendo km enzi za Baba wa Taifa mwalimu Nyerere

Unawaona wachina,wakorea,wajapan walivyo na utii na heshima kwa Nchi yao ni Kwasababu ya vipindi mbali mbali vinavyorushwa kuwajenga kimaadili vijana na ni lazima kufuatilia toka wakiwa watoto hadi wanakuwa

Ndio maana sio rahisi kusikia mjapan au mkorea anaitukana na kuidhihaki Nchi yake

Wizara ya michezo na utamaduni ipeleke mswaada bungeni ili kutengeneza Vijana wenye maadili tofauti na hawa wa sasa waliokosa nidhamu na heshima
Tuliozaliwa kabla ya 1977 tulikuwa tunaangalia tv wapi hata tukawa na heshima na uzalendo kwa taifa?

Tulikuwa na viongozi ambao mwenyewe utapenda umsikilize hata ktk redio kwa balozi kwasababu hawakuwa na tabia ya kujimwambafai kama hawa tulio nao zama hizi.

Kwangu nilishapiga marufuku kuangalia tbc kwa upuuzi wao. Nani ataangalia channel iliyoungana na tbc? Atapona? Sipendi ujinga nyumbani kwangu.
 
Hiki kizazi kilichozaliwa TANU haipo, wameikuta Ccm tu wengi hawana uzalendo
Namaanisha waliozaliwa kuanzia 1977 kuja juu wengi hawana Elimu ya uzalendo

Ili kuepusha kizazi kisichokuwa na maadili muhimu kuwe na vipindi vya t.v. na redio angalau saa moja kwa siku ili vijana wafundishwe uzalendo
Iwe ni lazima kusikiliza au kuangalia,Hii itafanya Vijana wengi wawe na sprit ya uzalendo km enzi za Baba wa Taifa mwalimu Nyerere

Unawaona wachina,wakorea,wajapan walivyo na utii na heshima kwa Nchi yao ni Kwasababu ya vipindi mbali mbali vinavyorushwa kuwajenga kimaadili vijana na ni lazima kufuatilia toka wakiwa watoto hadi wanakuwa

Ndio maana sio rahisi kusikia mjapan au mkorea anaitukana na kuidhihaki Nchi yake

Wizara ya michezo na utamaduni ipeleke mswaada bungeni ili kutengeneza Vijana wenye maadili tofauti na hawa wa sasa waliokosa nidhamu na heshima
Una akili ya kijinga sana
 
Iwe ni lazima kusikiliza au kuangalia,Hii itafanya Vijana wengi wawe na sprit ya uzalendo km enzi za Baba wa Taifa mwalimu Nyerere
Niseme tu unamkosea adabu Mwalimu Nyerere kutumia hiyo picha yake. Kuna picha chungu nzima ambazo zingekufaa sana zikiendana na mawazo yako haya.
Nakusikitikia sana kama wewe umezaliwa na kukulia kwenye enzi za Mwalimu Nyerere.

Lakini upande mmoja ngoja niiunge mkono hoja yako kuhusu
Ili kuepusha kizazi kisichokuwa na maadili muhimu kuwe na vipindi vya t.v. na redio angalau saa moja kwa siku ili vijana wafundishwe uzalendo
Iwe ni lazima kusikiliza au kuangalia...
hotuba za kiongozi wetu aliyepo madarakani.
 
Kuna nini cha kuonyesha kitakacholeta hiyo nidhamu na heshima?

Kitu pekee kinaweza kuwavutia ni Hotuba za Mwalimu Nyerere tu, Zikiisha wanaenda kuangalia mpira.

Sisi "Hawa wa sasa waliokosa nidhamu na heshima" Unatupeleka wapi?

Mara mtuambie tufanye kazi, sasa mnatulazimisha kuangalia na TV, mbona mnatuchanganya?

Na hizo TV mtatugawia bure? na umeme mtatulipia, make sisis tunaangalia TV huko Bar tunako angalia mipira.
 
Tatizo sio uzalendo,,,
Wananchi wengi hususan Vijana wanakosa uzalendo kutokana na kuminywa kwa uhuru wa habari hapa nchini kwetu
 
Inatakiwa pia kila wafanyakazi wakifika kazini washukulu juhudi za awamu ya tano kwakuwalinda usiku kucha na hii itasaidia sana nidham na uzarendo alisikia ndondocho fulan ivi kutoka mitaa ya lumumba
 
Back
Top Bottom