Ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kupunguza tatizo la ajira nchini ni vyema pasiwepo na teuzi, nafasi zote za kazi zipite Utumishi wa Umma

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,045
10,476
Uwendawazimu ni kufanya kitu kilekile huku ukitegemea matokeo tofauti.

Tukiwa tunaendelea kupendekeza Rais wetu mpendwa aongeze kipindi cha uongozi ili kutufikisha kuwa nchi iliyoendelea(developed country) itakuwa si vibaya tukiangalia vitu vingine ambayo vinahitaji mapendekezo kubadilishwa ili kuendana na hali ilivyo sasa na kwa vile ilishatamkwa kuwa katiba sio msaafu inaweza kubadilika pale itapoonekana inahitaji mabadiliko.

Natumia haki yangu kama Mtanzania kutoa maoni ambayo kwa upande wangu nimeona yanaleta tija kwa taifa ili siku Tanzania ikiwa nchi iliyoendelea nijisikie fahari kuwa sehemu ya mafanikio.

Mapendekezo yangu ni kuwa nafasi za mawaziri, wakuu wa mikoa/wilaya, Idara na Taasisi za kiserikali zipite katika mfumo wa Ajira(AjiraPortal) pawepo na sifa maalumu kama ilivyo kwenye Taaluma nyingine kwa mfano mkuu wa wilaya awe angalau ana Bachelor degree inayohusiana na uongozi inapotokea panahitajika mkuu wa wilaya Tangazo libandikwe Watanzania wenye sifa watume barua za maombi watakaokuwa na vigezo waitwe kwenye usaili na mwisho apatikane mmoja aliyecompetent apewe nafasi kupitia huu mfumo tutapunguza yafuatayo.

1. Kutokomeza Upendeleo wa aina yoyote kama vile upendeleo wa kichama, kabila, undugu na kirafike ifahamike hata Mimi nikipewa mamlaka watu wa kwanza kuwakumbuka ni watu wangu wa karibu sitojali uwezo wao wa utendaji.

2. Kutengeneza ajira nyingi kwa kuwa Mbunge ataendelea kuwa mwakilishi wa wananchi wake huku nafasi za Uwaziri zikichukuliwa na watu wengine hapa ndipo linakuja swala la Division of labour ili kuongeza ufanisi yawezekana hata mawaziri walioshindwa kumudu wizara zao hawakuwa wabovu Bali walikuwa na majukumu mengi ya kuwakilisha wananchi yaliyopelekea kusahau majukumu yao ya uwaziri ni vizuri mbunge akabaki kuwa mbunge tu huku nafasi za mawaziri zishikwe na Watanzania wengine nchi hii ni yetu sote.

3. Kuepuka mtu kuwajibishwa kutokana na chuki, wivu au maamuzi ya mtu mmoja kwa kuwa waziri atakuwa mwaajiriwa atakapoenda kinyume na maadili ya kazi kamati ya nidhamu itakaa kumjadili na pengine atapewa fursa ya kusikilizwa na kamati itatoa hukumu yenye haki na pia stahiki.

Mwisho nipende kushukuru hii ni Freedom of expression yawezekana maoni yangu yamemkwaza mtu ili tuweke pembeni maslahi binafsi tujali maslahi mapana kwa ajili ya Watanzania wote kiujumla.
 
Tatizo la ajira litaendelea kuwepo tu mpaka tubadili mfumo wetu wa elimu na tuwe na sera madhubuti za kukuza sekta binafsi (kikiwemo kilimo) kwa sababu huyo ndiye mwajiri mkuu. Tunafyatua wasomi maelfu kila mwaka wakati mwajiri mkuu ni serikali. Hiyo serikali itaajiri wangapi?

Hata teuzi zikiondolewa system ni ile ile na watakaoendelea kufaidika ni wale wale waliomo kwenye system. Usifikiri eti ajira zote zikipita utumishi ndiyo siku moja from nowhere mtoto wa mkulima ataukwaa ukuu wa mkoa au wilaya bila kuwa kwenye system. Nevaaaa !!!
Kupitia mazoea tayari ushatengeneza fikra kuwa kuna vitu haviwezi kutokea huko ni kukariri na nipende kukumbusha kuwa kuna baadhi ya viongozi ni watoto wa wakulima tena wa hali ya chini kuabisa jitahidi kuwa unafutilia profile za viongozi na walipotokea utathibitisha hilo.

Kuhusu kilimo kutoa ajira nyingi ni kweli lakini kutegemea kilimo pekee kumaliza tatizo la ajira ni kukionea kilimo inabidi pawepo na chain kubwa itakayosababisha mazao kuwa na soko kama uwepo wa viwanda, miundombinu mizuri ya usafirishaji, import na export kwa hiyo lazima pawepo na wasimamizi wengine ambao wanatoka serikalini.
 
Haujakwaza mtu, suala lako linaingia kwenye 'katiba mpya', suala tsyari liliwekwa vizuri na Hon.Warioba, lakini likawekewa zengwe kihuni huni tu.
 
Rais atawale si zaidi ya miaka kumi, ili kuleta ufanisi na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana. Akiondoka mapema, Vijana watakuwa na nafasi ya kupata hiyo nafasi aliyoiacha.
 
Uhuru wa kutoa maoni.

Mfano nafasi ya CDF au IGP nayo tutume maombi ajira portal?

I wish i could be IGP.
 
Back
Top Bottom