Ili kuijenga upya nchi yetu tunahitaji vitu 4

Hebu tufafanulie mkuu.

Watu= Watu ndio rasilimali mama, na ili maendeleo ya kweli yapatikane lazima uwe na watu na hao watu lazima wawe na Elimu Bora, Chakula Bora, Mavazi Bora na Malazi Bora, Watu wanatakiwa wawezeshwe kumudu maisha yao, na kuwa huru kuabudu na kufanya chochote kisichovunja sheria, KWA TANZANIA WATU WAPO WENGI LAKINI KIUKWELI WAMEKOSA ELIMU BORA, UHAKIKA WA PAKULALA, CHAKULA BORA NK

Ardhi= Ardhi including maji na rasilimali zote zilizopo (Misitu, wanyama, madini ect) ndio nyenzo muhimu kwa maendeleo ya watu binafsi na maendeleo ya taifa kwa ujumla, uchumi wa nchi yoyote lazima utegemee pande la Ardhi wanalolimiliki, ndani ya Ardhi ndimo kunamopatikana chakula, na mengineyo mengi yanayohusiana na maendeleo, ARDHI BADO TUNAYO KUBWA ILA TUNASHINDWA KUITUMIA, RASILIMALI ZA NCHI TUNAZIGAWA BILA KUZINGATIA MISINGI IMARA YA KIUCHUMI, NI TATIZO KWA TZ

Siasa Safi= Kwa kweli siasa ya nchi ndio inayodetermine maendeleo ya wanacnhi wake na nchi kwa ujumla, hapa tunazungumzia siasa inayofata Demokrasia na utawala bora wa Sheria, KWA TANZANIA TUNASIASA BORA YA MFUMO WA VYAMA VINGI, TATIZO LIPO KWENYE UENDESHAJI WA HIYO SIASA, UENDESHAJI WA SIASA UNAIPELEKEA IONEKANE KAMA SIO BORA, (mSAJIRI, JESHI, POLICE, MWAKUU WA MIKOA NA WILAYA) WOTE WANAINGILIA SIASA NA KUIFANYA SIASA ISIWE SAFI TENA

Uongozi Bora= unaweza kuwa na siasa safi ya Kidemokrasia na inayofata sheria, lakini ukawa na uongozi usio bora kabisa, na mara nyingi Uongozi usio bora unapelekea Siasa Safi kuchafuka, KWA TANZANIA HATUNA UONGOZI BORA, BALI TUNA BORA UONGOZI, VIONGOZI NDIO VICHWA WA WANANCHI WOTE, LAKINI WAO (VIONGOZI), WANAPOJIINGIZA KWENYE MASWALA YA KIFISADI NA RUSHWA BASI NA NCHI NZIMA INAYUMBA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom