Ili kuendelea kitaifa, Kuna umuhimu wa masikilizano baina ya Serikali na Wananchi wake

Dec 26, 2021
33
23
Kwa sababu tumeshindwa kusikilizana ndio maana hatuendelei.

Kwa muda mrefu, tumekuwa tukishindwa kutatua mizizi ya matatizo yetu. Tumeshindwa kutatua vyanzo vya matatizo yetu.
Taifa kiujumla na serikali zetu kwa awamu mbali mbali, kwa ujumla tumeshindwa tafuta suluhu ya matatizo yetu ya siku zote ujinga, umaskini na maradhi. Matatizo haya sio kuwa yanashindikana kutatuliwa, bali tumeshindwa kutafuta suluhu sahihi ya matatizo yetu.

Matatizo yetu ya siku zote ujinga, umaskini na maradhi, yameanza kuzungumziwa toka serikali awamu ya kwanza, lakini mpaka sasa serikali awamu ya sita bado tumeshindwa kuyatatua yakakoma.
Kinachopelekea tukose suluhu ya matatizo yetu ni kwa sababu tu hatutaki kusikilizana ndani ya nchi, Chama tawala na vyama pinzani haviwezi kukaa pamoja na kujadili namna ya kupata suluhu ya matatizo yetu.

Ndani ya serikali zote za nyuma na sasa, chama tawala ndio kimekuwa madarakani muda wote. Lakini bado hakijafanikiwa kutatua matatizo haya, na sio kwamba hata chama pinzani kikipewa madaraka kitaweza kuyamaliza matatizo haya.
Kama tunadhania kuwa matatizo haya yatamalizwa na kikundi cha watu wa aina moja au chama kimoja au chama fulani, basi tunasafari ndefu sana.

Matatizo haya hayatotatulika na mtu mmoja au CHADEMA au CCM pekee, matatizo haya tunaweza kuyatatua kwa kukubali kusikilizana. Tukikubali kusikilizana, tutaweza kushikamana, kuungana na kushirikianana ndipo utakuwa mwanzo wa kutatua matatizo haya.

Kwa aina ya siasa, iliyopo nchini na ndio watoto wetu na wajukuu wetu watarithi ni ngumu sana, kutatua matatizo yetu kama taifa. Matatizo haya ili tuweze kuyamaliza kwanza inabidi tuwe na self esteem na discipline kama taifa, na sio kwa mtanzania mmoja mmoja. Kama vyama vyote vya siasa nchini, vinasema vipo tayari kuona matatizo haya yakitatuliwa, basi inabidi vikubali kusikilizanza kwa heshima, adabu, misingi na taratibu zilizowekwa nchini.

Pahala popote pasipo kuwepo kusikilizana, huzaa ushindani na hatimae migogoro, ndio kinachotokea nchini kwetu. Serikali ya hayati Magufuli imefanya mazuri na mengi ndani ya muda mfupi, kuna kiongozi wa vyama pinzani aliyetoka hadharani na kumpongeza? Jibu ni hamna, lakini huenda tusingekuwa tunafanya aina hii ya siasa, angetoka hata mmoja na angewasihi wamu-unge mkono na kumtia moyo.

Bungeni, mbunge wa chama pinzani anaweza pendekeza hoja na yenye tija kwenye maslahi mapana ya taifa lakini asikilizwe kutokana tu anatokea chama pinzani. Tunatanguliza toafuti zetu kuliko maslahi ya taifa letu na wananchi wake.

Aina yetu ya siasa tunaoifanya ndio hupelekea tushindwe kusikilizana. Ifikie pahala tu, tubadili nyenendo zetu kama taifa. Tubadili aina siasa, tufanye siasa zenye tija kwa tiafa na wananchi wake kiujumla.

Ningependa kuona siku Mh: Freeman Mbowe, anateuliwa kwenye wizara itayoendana na taaluma yake na apate kuonyesha weledi wake na utendaji kazi wake. Wengi watasema kwa sasa haiwezekani? Sasa na mimi nitawauliza lini sasa?

Maana kinachotokea nchini, wakina Warioba walikuwa serikalini na kwenye kuanda katiba ya sasa walikuwepo. Wamezeeka na hawapo kwenye nyadhifa za maamuzi leo wanapendekeza katiba mpya. Au ndio mtanzania akizeeka ana-anza kujitambua?
 
Wanasiasa bana.

Wataongea were, watapiga keleeee lakini mwwisho wa siku wanataka MADARAKANI au Waitwe mezani watumbue Kodi za Mlalahoi.

Nchi in makundi mengi, lakini kundi la Wanasiasa usipolipa linachotaka unaweza kudhani ARDHI YA NCHI IMEGEUKA CHINI JUU🤣
 
Kwa sababu tumeshindwa kusikilizana ndio maana hatuendelei.

Kwa muda mrefu, tumekuwa tukishindwa kutatua mizizi ya matatizo yetu. Tumeshindwa kutatua vyanzo vya matatizo yetu.
Taifa kiujumla na serikali zetu kwa awamu mbali mbali, kwa ujumla tumeshindwa tafuta suluhu ya matatizo yetu ya siku zote ujinga, umaskini na maradhi.
Matatizo haya sio kuwa yanashindikana kutatuliwa, bali tumeshindwa kutafuta suluhu sahihi ya matatizo yetu.

Matatizo yetu ya siku zote ujinga, umaskini na maradhi, yameanza kuzungumziwa toka serikali awamu ya kwanza, lakini mpaka sasa serikali awamu ya sita bado tumeshindwa kuyatatua yakakoma.
Kinachopelekea tukose suluhu ya matatizo yetu ni kwa sababu tu hatutaki kusikilizana ndani ya nchi, Chama tawala na vyama pinzani haviwezi kukaa pamoja na kujadili namna ya kupata suluhu ya matatizo yetu.

Ndani ya serikali zote za nyuma na sasa, chama tawala ndio kimekuwa madarakani muda wote. Lakini bado hakijafanikiwa kutatua matatizo haya, na sio kwamba hata chama pinzani kikipewa madaraka kitaweza kuyamaliza matatizo haya.
Kama tunadhania kuwa matatizo haya yatamalizwa na kikundi cha watu wa aina moja au chama kimoja au chama fulani, basi tunasafari ndefu sana.

Matatizo haya hayatotatulika na mtu mmoja au CHADEMA au CCM pekee, matatizo haya tunaweza kuyatatua kwa kukubali kusikilizana. Tukikubali kusikilizana, tutaweza kushikamana, kuungana na kushirikianana ndipo utakuwa mwanzo wa kutatua matatizo haya.

Kwa aina ya siasa, iliyopo nchini na ndio watoto wetu na wajukuu wetu watarithi ni ngumu sana, kutatua matatizo yetu kama taifa. Matatizo haya ili tuweze kuyamaliza kwanza inabidi tuwe na self esteem na discipline kama taifa, na sio kwa mtanzania mmoja mmoja. Kama vyama vyote vya siasa nchini, vinasema vipo tayari kuona matatizo haya yakitatuliwa, basi inabidi vikubali kusikilizanza kwa heshima, adabu, misingi na taratibu zilizowekwa nchini.

Pahala popote pasipo kuwepo kusikilizana, huzaa ushindani na hatimae migogoro, ndio kinachotokea nchini kwetu. Serikali ya hayati Magufuli imefanya mazuri na mengi ndani ya muda mfupi, kuna kiongozi wa vyama pinzani aliyetoka hadharani na kumpongeza? Jibu ni hamna, lakini huenda tusingekuwa tunafanya aina hii ya siasa, angetoka hata mmoja na angewasihi wamu-unge mkono na kumtia moyo.

Bungeni, mbunge wa chama pinzani anaweza pendekeza hoja na yenye tija kwenye maslahi mapana ya taifa lakini asikilizwe kutokana tu anatokea chama pinzani. Tunatanguliza toafuti zetu kuliko maslahi ya taifa letu na wananchi wake.

Aina yetu ya siasa tunaoifanya ndio hupelekea tushindwe kusikilizana. Ifikie pahala tu, tubadili nyenendo zetu kama taifa. Tubadili aina siasa, tufanye siasa zenye tija kwa tiafa na wananchi wake kiujumla.

Ningependa kuona siku Mh: Freeman Mbowe, anateuliwa kwenye wizara itayoendana na taaluma yake na apate kuonyesha weledi wake na utendaji kazi wake. Wengi watasema kwa sasa haiwezekani? Sasa na mimi nitawauliza lini sasa?

Maana kinachotokea nchini, wakina Warioba walikuwa serikalini na kwenye kuanda katiba ya sasa walikuwepo. Wamezeeka na hawapo kwenye nyadhifa za maamuzi leo wanapendekeza katiba mpya. Au ndio mtanzania akizeeka ana-anza kujitambua?
Kusikilizana maana yake nini?
 
Lugha yetu ni changa.

Listening na hearing ni tofauti Sana fuatilia.

Nchi yetu tumeshindwa kusikilizana Yani listening to each other.
Mimi na wewe tunashindwa kusikilizana?

Nakuuliza kusikilizana maana yake nini, unanijibu nchi yetu tumeshindwa kusikilizana.

Hata anayesema tumeshindwa kusikilizana kashindwa kusikilizana?

Hujajibu swali.

Kusikilizana ni nini?
 
Kusikiliza ni uwezo wa kupokea na kutafsiri kwa usahihi na umakini ujumbe katika mchakato wa mawasiliano.
 
Back
Top Bottom