Ili kubana matumizi, uchaguzi Zanzibar usifanyike Shein atangazwe mshindi.

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,819
49,016
Kwa vile CUF wamesusia uchaguzi na kwa vile hakutakuwa na chama kingine zaidi ya CCM kitakachoshinda uchaguzi wa marudio.....

Nashauri, kuliko kufanya uchaguzi Zanzibar, Jecha amtangaze tu Dr. Shein kuwa ni mshindi awe rais ili maisha yaendelee kama kawaida.

Lakini kwa vile wanataka kusindikizwa kuonyesha dunia kuwa Tanzania tuna demokrasia ya kweli wakati ni "plastic democracy", watalazimisha uchaguzi ufanyike, huku wakijua ni matumizi mabaya ya kodi ya mwananchi kwa sababu mshindi anajulikana.

Rais Magufuli, kama umeshindwa kuacha matakwa ya wananchi yaheshimiwe, amuru uchaguzi usifanyike na Shein atangazwe ameshinda uchaguzi wa marudio.
 
It is true, hakuna haja ya kufanya uchaguzi wa marejeo unaoitwa uchaguzi wa vyama vingi wakati infact utakuwa ni uchaguzi wa chama kimoja, Chama Cha Majipu.

Hizo bilioni 7 zilizotengwa kwa ajili ya uchaguzi ni bora hata zingejengea barabara au zingenunulia dawa hospitali.

Ni ujuha na wastage of public funds kutumia bilioni 7 kwa uchaguzi huo ambao watawala wamepanga hata kwa kutunia vyombo vya dola kuwa ni lazima Dr Shein aapishwe na kuendelea na Urais.

Kama Magufuli alifuta sherehe za uhuru na akaokoa bilioni 4 ambazo hivi sasa zinapanua barabara toka Mwenge hadi Moroko- Kinondoni.

Kwa hiyo ni vyema Dr Shein (Gbagbo) wa TZ naye akaufuta uchaguzi huo ili yeye aapishwe tu na pesa hizo zifanye shughuli za maendekeo.
 
Uchaguzi ambao hauna waangalizi wa ndani nje unakua hauna grade na huwa hauaminiki ni kufuja pesa za wananchi tu .yeye mwenyewe juzi dk shein kakiri kwamba yeye ni raisivwa katiba tu ila hakusema kama alishinda kwenye uchaguzi
 
Kwa vile CUF wamesusia uchaguzi na kwa vile hakutakuwa na chama kingine zaidi ya CCM kitakachoshinda uchaguzi wa marudio.....

Nashauri, kuliko kufanya uchaguzi Zanzibar, Jecha amtangaze tu Dr. Shein kuwa ni mshindi awe rais ili maisha yaendelee kama kawaida.

Lakini kwa vile wanataka kusindikizwa kuonyesha dunia kuwa Tanzania tuna demokrasia ya kweli wakati ni "plastic democracy", watalazimisha uchaguzi ufanyike, huku wakijua ni matumizi mabaya ya kodi ya mwananchi kwa sababu mshindi anajulikana.

Rais Magufuli, kama umeshindwa kuacha matakwa ya wananchi yaheshimiwe, amuru uchaguzi usifanyike na Shein atangazwe ameshinda uchaguzi wa marudio.
Dr. Shein ameshajitangaza kuwa yeye ni Rais halali kwa mujibu wa Katiba, mimi pia sioni sababu ya msingi kwa wanamapinduzi wa Zanzibar kutaka uchaguzi wa marudio.Kwa nini wanataka kuharibu fedha kwa kuchapisha vikaratasi? Fedha zitumike kuwasaidia wazee(vikongwe) waweze kupata mlo mmoja kwa siku.

Link Maneno yao hayanisumbui mimi Rais kwa mujibu wa Katiba. — President's Office State House and Good Governance

Link2. "Mimi ndiye Rais Halali wa Zanzibar na Nisiposema Mimi Nitawatuma Wasaidizi wangu Kuwaeleza" - Dk Shein | MPEKUZI

Back
Top Bottom