Ili kubana matumizi, uchaguzi Zanzibar usifanyike Shein angazwe mshindi

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,816
49,000
Kwa vile CUF wamesusia uchaguzi na kwa vile hakutakuwa na chama kingine zaidi ya CCM kitakachoshinda uchaguzi wa marudio.....

Nashauri, kuliko kufanya uchaguzi Zanzibar, Jecha amtangaze tu Dr. Shein kuwa ni mshindi awe rais ili maisha yaendelee kama kawaida.

Lakini kwa vile wanataka kusindikizwa kuonyesha dunia kuwa Tanzania tuna demokrasia ya kweli wakati ni "plastic democracy", watalazimisha uchaguzi ufanyike, huku wakijua ni matumizi mabaya ya kodi ya mwananchi kwa sababu mshindi anajulikana.

Rais Magufuli, kama umeshindwa kuacha matakwa ya wananchi yaheshimiwe, amuru uchaguzi usifanyike na Shein atangazwe ameshinda uchaguzi wa marudio.
 
Kuna logic katika bandiko lako.

Maana kwa kuwa CUF hawaatashiriki huu uchaguzi ni dhahiri CCM itakuwa kinara.
 
CCM Hawato kubali kufanya hiki kitu,itaonekana kama walikuwa wanahofu na CUF!Lazima uchaguzi wa maigizo ufanyike
 
Unachokisema kipo poa sana,sema lazima wafanye hayo maigizo maana hatma ya ruzuku ya chama inatokana idadi ya kura kwa kila chama na ndio maana umeona wanafiki kama ADC wamekua wa kwanza kutangaza kua watashiriki wakidhani wanaweza pata kura nyingi zitakazo boost ruzuku ya chama chao
 
Naunga mkono hoja 100%.Hakuna mantiki ya kufanya huu uchaguzi wakati mshindi anajulikana.Hongera zao mahafidhina wa kijani na njano,waokote tu embe kwenye mpaipai.
 
Back
Top Bottom