Ili CCM ishinde 2015 ifanye hivi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ili CCM ishinde 2015 ifanye hivi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Mar 7, 2011.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mafanikio ya CCM kwenye uchaguzi wa 2015 na hakika miaka ya mbeleni baada ya hapo ita tegemea sana na safu ya wagombea itakayo wakilisha kwa wananchi hapo 2015. Kwa vile JK kikatiba hata ruhusiwa kugombea 2015 hakuna sababu ya CCM kusumbuliwa na utaratibu wao wa kumpitisha raisi anaye toka chama chao kugombea muhula wa pili bila kupingwa.

  Nikisema safu ya wagombea namaanisha wote wabunge pamoja na mgombea uraisi. Nitajaribu kuelezea jinsi wagombea ubunge na uraisi watakavyo kiua au kukifufua CCM.

  1. Wagombea ubunge:
  Kwanza hapa wanabidi wafuate demokrasi na kuhakikisha alieshinda kura za maoni ndiyo mgombea. Lazima mgombea ubunge aonekane kuwa chaguo la watu laa sivyo wapiga kura wataona walio pitishwa ni wagombea wenye kutetea maslahi ya wachache ndani ya chama na si wananchi.

  Wahakikisha wana pata wagombea ubunge wenye mvuto kwa jamii na rekodi nzuri katika utumishi. Hii ita saidia kukipa mvuto tena chama na kurudisha imani ya wananchi kwake. Kuna wanaCCM wengi tu wanaopendwa na kuheshimiwa na jamii pamoja ya kwamba CCM kiujumla wake si maarufu kwa sasa.

  Wahamasishe vijana wengi zaidi wagombee ubunge kupitia chama chao. Na hapa namaanisha vijana ambao hawaji na mzigo wowote i.e. not the Laus and the like. Kwa kawaida vijana wana clean record na jamii ipo tayari zaidi kuwapa nafasi. Lakini muhimu zaidi itaonyesha kwamba chama kipo tayari kuanza upya na kufungua ukurasa mpya.

  2. Mgombea urais:
  Sihitaji kusisitiza umuhimu wa mgombea raisi kwa chama chochote. Mgombea uraisi ndiyo kama "kapteni" wa safu ya wagombea ofisi za umma wa chama chochote. Mgombea uraisi kwa mvuto wake ana weza hata kusaidia wagombea wa nafasi mbali mbali toka chama chake washinde. Mgombea uraisi ndiye sura wa chama katika chaguzi na ndiyo kiashiria ya nini tutegemee kutoka kwa chama hicho.

  Hapa CCM isilambe matapishi yake. Hapa namaanisha kuto kung'an'gania kumuweka mtu ambae alisha poteza mvuto kwa jamii. Nadhani hapa wote mnajua namaanisha nini. Mgombea uraisi siyo lazima atoke kwenye kundi la wale "usual suspects". Washtueni wananchi kwa kumuweka hata mtu ambae hawaja fikiria kabisa ange gombea kama ilivyo kuwa kwa Chadema na Dr. Slaa.

  Wakati wa kuchagua mgombea msiangalie tu CCM mnamtaka nani bali angalieni wananchi wanamtaka nani. Kwani mgombea uraisi ni wa chama ila akisha kuwa raisi ana kuwa raisi wa wananchi wote. Kwa hiyo msiangalie tu maslahi ya chama.

  Hakika msi chague mtu yoyote ambae ana connections na failures za awamu itakayo kuwa ina maaliza muda wake. Hii itaonekana kama muendelezo wa yale yale kama vile John McCain wa Marekani alivyo onekana angekua muendelezo wa yale yale ya George Bush. Kuweni makini sana. Kwa safari hii nawa shauri mvunje utamaduni na kuto kumchagua mtu yoyote aliye kuwa waziri katika awamu hii ya nne.

  Chagueni mtu ambae hana madeni makubwa ya fadhila! Hii itampunguzia uwezo wa kuchagua watu kwenye nafasi za uteuzi kwa kuzingatia merit za hao watu. Kila mwanasiasa ana madeni kwa vile hamna anaeingia ofisini bila kuwa na nguvu za watu nyuma yake ila wekeni mtu mwenye deni dogo iwezekanavyo.

  Mwisho:
  Haya ni maoni yangu tu. Hakika maamuzi ya mwisho ni ya CCM yenyewe na hatma ya chama ipo katika uongozi wa sasa. Sitegemei kwamba nita sikilizwa mwananchi wa kawaida kama mimi. Ila mwishoni hakika hamtaweza kusema hamkuambiwa.
   
 2. M

  Mwera JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli tupu nakupa thanx.
   
 3. M

  Mwera JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli tupu,ila ccm wanasema ina wenyewe.
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Una maanisha nini mkuu? Sija kuelewa vizuri.
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,878
  Likes Received: 2,343
  Trophy Points: 280
  wamfukuze Makamba ili kurudisha umoja wao na kuua makundi, Mwamuombe samahani Six na wengineo waliowanyonyoa bila kosa kwenye chaguzi zao. Wamshughulike RA.

  Kwa CCM hii ya leo hawataweza kuyafanya hayo yote aliyoyasema mwana falsafa, ndiyo maana tunasema CCM imeishiwa nguvu za Hoja na kuanza kukilaumu CHADEMA, baada ya kujibu hoja wao wanaomba msaada wa dola kama kawaida yao.

  Walizoea ku relax baada ya chaguzi za nyuma kwa sasa wameshikwa, viongozi wavivu wa kutafuta solution za matatizo ya wananchi ndiyo hao hao wanakurupuka na kusema CHADEMA Inafanya nchi isitawalike.

  Watanzania wa leo si wale wa miaka ya 80. CCM kwisha kazi.
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  FUSO nakubaliana na wewe kwamba Watanzania wa leo si wale wa kale. Tatizo CCM badala ya kushughulikia roots za matatizo yao (ambayo yana tokana na chama) wana tafuta wachawi nje. So far hiyo tactic haijafanya kazi. Ni lazima wajiangalie wao wenyewe na watambue kwamba yote yanayo semwa dhidi ya chama na serikali si ya uwongo wala ya kupuuzwa.
   
 7. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Ningekuwa Mwenyekiti wao kitaifa basi wanachama woooote walioviongozi wa CCM toka ngazi ya shina mpaka taifa hivi sasa wangekuwa safarini Loliondo wakanywe dawa inayotibu magonjwa yote labda ingesaidia kukomesha ufisadi uliojengeka ndani ya mioyo yao
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ha ha ha interesting statement mkuu. Ila tatizo mwili ukisha kuwa na magonjwa mengi sugu ni vigumu kujua uanze kutibu nini na utumie dawa gani. Mimi binafsi nadhani mtu kabla hajawa kiongozi wa chama fulani ni lazima apitie mafundisho kuhusu chama ikiwemo utumishi, falssafa na itikadi ya chama. Nadhani ndiyo dawa wanayo hitaji.
   
 9. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Kabla ya kuanza kufikiria ushindi wa 2015 kwanza tuwaombe hao CCM wayatekeleze haya,kama wakiyaweza tu haya basi ushindi hautakuwa na matatizo yeyote kabisa.

  CCM wanapaswa kuchukua hatua hizi haraka iwezekanavyo,lasivyo uchaguzi ujao itakuwa ni ndoto kabisa kwao.Hatua hizo ni:

  1.kupunguza mfumuko wa bidhaa,kwa kupunguza kodi ya bidhaa muhimu au kwa kuweka fedha maalumu katika sekata hizo( incentives) ili kupunguza mfumuko wa bei.

  2.kuongeza mishahara kama China wanavyofanya kwa sasa.Huwezi kunieleza mshahara ule ule utakidhi mahitaji wakati zamani nilinunua sukari 1600 leo 2200, petrol iko juu,nauli ziko juu ..je huyo mtu ataishije??

  4.Hapo ndipo serikali inapotakiwa ichukue hatua za haraka zaidi wala sio kuanza kulaumiana na CDM au watu wengine.Wenye matatizo ni wananchi wala sio CDM kama wananyotaka kusema.

  5.Kama watasema kuwa hawana pesa basi walifanye hili, kupunguza mishahara ya watu wakubwa wote kama wabunge,mawaziri etc Hawa wapunguziwe kabisa hiyo mishahara yao au wawekewe tax kubwa zaidi ili hizo pesa ziende moja kwa moja ku-subsidize wale wenye low income ,hili linafanywa na nchi za wenzetu na limeonekana kuwa linafaa sana.Mwaka juzi nimeshuhudi kipindi cha mtikisiko wa Uchumi Serikali ya Hong-Kong ilipitisha sheria ya kupunguzwa mishahara kwa wote wanakuwa over-paid ili ku-compensate na wale wasio kuwa na kipato kabisa.

  Cha kushangaza sisi katika serikali yetu pamoja na hali kuwa ngumu kwa uchumi bado wameendela kuwa na matumizi yale yale ya mwaka 1947 kitu ambacho hakiendani na uhalisia wa hali ya sasa.Tumeona USA katika bajeti yao wamepunguza na kutoa mambo mengi sana ambayo yanaonekana kuwa hayana kipaumbele na hao wenzetu wana pesa sembuse na sisi tulio ombaomba katika kila kitu?

  Pamoja na miradi mingi kuwa inachangiwa na nchi za wahisani serikali yetu matumizi yake ni mengi sana na mzigo mkubwa kwa walipa kodi.Hili ni lazima libadirike,lasivyo siku zijavyo sitashangaa kusikia kuwa miradi yote iko juu ya mawe,sababu serikali inachangia kiasi kidogo sana katika miradi ya maendeleo wakati pesa nyingi zikitumika katika uendeshaji wa serikali ,na nchi wahisani pia wako katika hali ngumu sana kiuchumi hivyo itafika wakati nao watasema hatuwezi kuendelea kusaidia ninyi wakati wananchi wetu nao wanahitaji msaada.

  6.Ukweli ni kwamba kuna income gap kubwa kati ya rich and the poor na hapo social instability haiepukiki lasivyo wawasaidie hao walio na kipato cha chini.Kuna watu wanaoishi maisha ya kifalume na wakati wengine hata ule mlo mmoja kwa siku ni anasa.

  This can be done without even affecting other social development projects.
   
 10. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Duh mbona umewapa masharti magumu hivyo, watayaweza kweli?? mbona naona ni kama hakuna hata moja linaloweza kutekelezwa?
   
 11. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu uogozi uliopo sasa umeshindwa kudeliver na sidhani kama wata kuja kudeliver. Ndiyo maana mimibinafsi naona bora waji pange tu umpya.
   
 12. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ili waanze safari ya Tija wafuatao wafukuzwe chama
  RA
  EL
  MK
  AK
  EC

  Kwa kuanzia tu, halafu vikao vitafanyika.:hand:
   
 13. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Fred nadhani orodha yako itakaa vizuri iwapo tukimwongeza aliyeasisi makundi na matusi ndani ya chama. Sioni unafuu kumwondoa RA au EL ukamwacha JK.
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kuna baadhi ya watu wana hitaji kuondoka ila hawawezi kuondoka kwa hiari. Lazima watu wawachallenge katika nafasi zao. Kwa vile hawa watu wana nguvu ya pesa ndani ya chama challengers wao inabidi wawe na charisma kubwa sana. Otherwise itakua ni swala la kusubiri wazeeke na kuji chokea zao.
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Mar 7, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,136
  Trophy Points: 280
  Mwanafalsafa1,

  ..CCM imeoza kila mahali.

  ..labda kwa kuanza Kamati Kuu, Halmashauri kuu, viongozi wote wa mikoa na wilaya wajiuzulu.

  ..baada ya hapo Chama kiundwe upya kiuongozi na kiitikadi.

  ..cosmetic changes za kuvutia vijana na kupachika mgombea Uraisi asiyefahamika[read asiye na rekodi] hazitasaidia chochote.
   
 16. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu Jokakuu that means basi CCM kwa kizazi hichi cha viongozi wame kwisha. Labda wasubiria vijana watakao warithi...right?
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Mar 7, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Politicians are the same all over. They promise to build a bridge even where there is no river.
   
 18. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #18
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  "Ushauri wako in kunyume kabisa na mila,desturi, imani na matarajio ya CCM,
  Ushauri gani huu ambao una lengo la kupandikiza chuki, dharau, uhasama na ugomvi ndani ya chama chetu!
  Ushauri wako una lengo la kuuwa moyo wa ushirikiano, udugu na mshikamano ndani ya chama chetu"


  Hayo ndo yatakuwa maoni yao kuhusu ushauri wako
  HAWASHAURIKI

  Waacheni jama chama hicho kife na kizikwe

  Itakuwa ni faida kwa wanaCCM, wananchi wengine na nchi kwa ujumla!
  Tunapaswa kuvuta hewa mpya jamani!
  Mnataka Chama hicho kiwepo mpaka lini?
  Hamuoni kuwa hiyo itakuwa ni kama laana kwa Watanzania?
   
 19. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #19
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu ni kweli kwamba mwili wa kufa hausikii dawa. Ni juu yao kujitibu kabla ugonjwa hauja wamaliza.
   
 20. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  La kwanza na muhimu kabisa kuanza kutekelezwa ni Tendwa kukifuta na kukiondoa kwenye ramani ya vyama vya siasa duniani. Kisha wenye moyo safi wa wakulima na wafanyakazi waanzishe chama kipya cha kisiasa, na watumikia tumbo waachwe solemba. Hili Tendwa anatakiwa kulitekeleza mara moja ili kuepusha anguka la hicho chama ifikapo 2015, hasira ya watu kabla haijakiondoa madaraka.
  Hili dodoki limezoa uchafu kiasi ambacho haieleweki tena shobo ya huyo uchafu ulomeza bado nalo linatakiwa kuvuka 2015. Aaaaah HAPANA ama kwa kuazima maneno - hii ni BIG NO
   
Loading...