Ilhamu ya Riwaya

Njopino

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2014
Posts
3,468
Reaction score
5,072
ILHAM

Maisha ni tufe lililosheheni mduara wa muendelezo wenye visa na matukio yenye mipaka ya wakati. Imani hujenga mwanzo na mwisho. Uhalisia huzingatia kuwepo kwa mwanadamu na kuaga kwake. Visa na mikasa hujenga madhira yanayofinyangwa kwenye mazingira. Moyo mpevu uilopevuka hasa huyaelewa haya na kuyahimili kwa kuyaendeleza na kuendeleza wakati. Moyo mpevu usiopevuka hugeuka madhira na majanga unaoshindwa kuyahimili na kuacha wengine waendeleze. Kila mwanzo ni kimbunga, kila mwanzo ni muendelezo. Changusina ni binadamu anayetamani kuanza upya lakini anaishia kuendeleza. Sikujua, huyu hakujua kweli anaanzia wapi kwa upofu huu anaishia kuendlezana kuachawengine waendeleze, waendelee na madhira yao. Mwaija na Msomali nao hivyo hivyo wanatamani kuanza wanaishia kuendeleza na kuacha wengine waendeleze.

Looo….! Moyo Mpevu, uliojaa masumbuko, yanayopelekea binadamu kushindwa kuhimili mikikimikiki ya ulimwengu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…