Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,811
- 218,468
Wilaya ya Ileje ni miongoni mwa Wilaya zilizounda Mkoa wa Mbeya (naambiwa sasa imehamishiwa Mkoa wa Songwe ) ni miongoni mwa wilaya zinazounda Mkoa huo, historia inaonyesha kwamba kabla ya kuwa Wilaya. Ileje ilikuwa sehemu ya Wilaya ya Rungwe.
Mpaka sasa imetimia miaka 48 tangu Ileje iliporasimishwa na kuwa Wilaya. Bali umasikini unaoiandama Wilaya hii unatisha. Kibaya zaidi Hali ya Umasikini wa kutupwa wa Ileje inafichwa na viongozi wa serikali na ccm ili kuepusha Aibu, shule ni duni, huduma za afya ni duni, huduma za kijamii ni duni, hali ya uchumi wa mtu mmoja mmoja inasikitisha, kwa ufupi ni kwamba Ileje inanuka umasikini wa kutia aibu.
Lakini cha kushangaza ni kwamba , Wilaya, Halmashauri na Jimbo hilo vimeongozwa na ccm kuanzia enzi za Uhuru hadi leo, ukiacha madiwani wawili watatu kutoka NCCR, TLP na CHADEMA.
Iko haja sasa ya wananchi kushikamana kwa pamoja kuikomboa Ileje kwa Udi na Uvumba ili kunusuru maisha ya Watu .