Ile timu tuliyoaminishwa kuwa ni bendi kwakuwa imekusanya wakongo wengi hatimae imetinga fainali ya CAFCC

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Ile timu tuliyoaminishwa kuwa ni bendi kwakuwa imekusanya wakongo wengi hatimae imetinga fainali ya CAFCC duuh, na ndo hao hapo wanakata mayenu baada ya kumaliza kazi ya msingi iliyowaleta Tanzania, wametujibu kwa vitendo nje na ndani ya uwanja, wametufunga midomo tuliowabeza, kumbe walikuwa wanaona na kusikia.

Yule Mzee wa "Mikimbio" jana ametujibu pia, hili jina alibatizwa na wachambuzi, haikuwa kwa heri hata kidogo ila ilikuwa ni njia ya kubeza usajili wake na kutaka kuaminisha umma kuwa Wananchi wamepigwa kwenye usajili ule..ni sisi hao wabongo na bongo zetu, huwa tunataka mchezaji akisajiliwa lazima afunge goli/magoli kwenye mechi ya kwanza tu...sasa jamaa jana kadhihirisha yeye na mikimbio ni dam dam na laiti kama Mudathir angekuwa makini jana mikimbio yake ingezaa assist 3 na goli 1..Muda ni hakimu mzuri sana, kwani hamuoni aibu huko.

Ukitaka kuweka kufuli kuimarisha ulinzi wa Boma lako panda bus za Abood mpaka Morogoro nauli haizidi shilingi 8000/= tu, na pesa kidogo ya daladala kamchukue JOB muweke kulia, mwambie KIBWANA akae kushoto kisha wape majukumu ya kuzurura kwenye kona za nyumba wasivuke geti kwenda kwa jirani maana vibaka ni wengi huo mtaa kisha waulize kama wamekuelewa.. mpigie simu Bacca, mwambie anapotoka kwao unguja ashukie bandari ya Tanga, atamkuta Mwamnyeto anamsubiri pale, tiketi zao za kuja Dar zimeshalipiwa wanasubiriwa wao wakabidhiwe funguo za Boma wanatakiwa kubeba wao.. ni muhimu sana wasisitize kuwahi Lindo maana jua ndo hilo linazama na usiku unaingia.

Kwakuwa kuna nyakati hekaheka zinatakiwa nyingi kwenye himaya ya mpinzani..DJ Nabi walete stejini Djuma Shaban na Joyce Lomalisa maana kwa jirani kunapigwa bonge moja la singeli wanenguaji wamevaa kanga moko..wananchi hawahitaji maji kwenye vidumu aisee, kwanini kujibanabana ? Ng'oa koki zote za kulia na kushoto aya mwaga maji.Wananchi wana raha buanaaa. Nje NTITI ndani NTITI

Hawavuki hawa, wamevuka.hawashindi pale, wameshinda...sasa mapambio yamebadilika mara ooh wamekutana na vibonde..Oyaa wananchi waambieni hizo siyo shida zenu. Kutoka kuambiwa wanatengeneza bendi mpaka kuambiwa hamchukui kombe.MAUMIVU HAYA..congrats @yangasc
Follow Instagram @kipatamaestro

FB_IMG_1684483916997.jpg
 
Back
Top Bottom