Ila wanawake kwanini mnapenda Udaku na Upatu

Ila wanawake kwanini mnapenda Udaku na Upatu

Machuchu

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2017
Posts
1,260
Reaction score
969
Za leo wakuu.
Pitapita zangu leo nimeingia ofisi moja pale Mzumbe University ya Upanga, uyu mwanamama anafundisha pale ila mezani kwake ana magazeti ma2 ya udaku na 1 kalishikilia anasoma. Niijiuliza sana na kusema mule anafuata habari gani za maana.??

Pia wanawake wengi wanapenda Upatu (mchezo wa kupeana ela) huu mchezo ni maarufu sana uswahilini na mala nyingi huwa wanazulumiana na ugomvi juu na ukiwauliza kwa nini usihifadhi mwenyewe anajibu kua kuweka Tsh. 2000/= kila siku hawezi, ila wapo wanaocheza Tsh.20,000/= kila wiki anatoka mtu Tsh.100,000/= kwa mwezi, cha kushangaza ukienda kushtaki polisi huwa hawatambui huu mchezo kisheria.
 
Kwamba tunakosea??? Embu tuacheni wanawake tupate raha
 
Kama nyie mnavyopenda mpira si tunapenda udaku, ndio tunakopunguzia stress mnazotupa huko majumbani.
 
Kila watu na starehe zao...
Wanaume wanapenda mpira, kukaa bar na vijiweni, kubet
 
Huo upatu ndio noma kabisa unashangaa umekaa unaangalia tv yako watu wanaingia wanabeba ukiuliza ni mambo ya upatu
 
Back
Top Bottom