Ikulu yamtetea Prosper Mbena

Ikulu yamtetea Prosper Mbena

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,162
Reaction score
162,594
VYOMBO vya habari nchini vimeaswa kuripoti matukio yaliyofanyiwa uchunguzi wa kina na yenye kufuata maadili na taaluma ya habari, badala ya kufanya kazi kwa kuongozwa na ushabiki vinapotekeleza majukumu yake.

Hayo yameelezwa katika taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari ikikanusha kuhusika kwa Katibu wa Rais Jakaya Kikwete, Prosper Mbena katika kumpa mwongozo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu ili auruhusu uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyopo katika BoT.

Taarifa hiyo inasema baadhi ya vyombo vya habari (siyo HabariLeo) vimemhusisha Mbena kuingilia mchakato wa uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 306 katika akaunti hiyo iliyoibua hoja nzito nchini, kiasi cha Bunge kuingilia kati na kutaka baadhi ya mawaziri na watendaji serikalini wawajibike kwa kile kinachodaiwa kuchota fedha za umma, jambo ambalo bado halijathibitishwa rasmi. "Huu ni uongo na uzushi.

Ni jaribio jingine la kutia chumvi katika jambo ambalo limetawaliwa kwa kiasi kikubwa na mihemko ya aina yake.

Gavana Ndulu mwenyewe anathibitisha kuwa hajawahi kupokea barua yoyote kutoka kwa Katibu wa Rais kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow.

Akaunti ya Escrow ilifunguliwa baada ya kutokea kwa mgogoro wa kimaslahi baina ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL na Tanesco.

Chanzo:Habarileo
 
Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imetoa taarifa kwa vyombo vya habari ikikanusha kuhusika kwa katibu wa raisi Jakaya Kikwete,Prosper Mbena kumpa Mwongozo Gavana wa benk kuu,bwana Benno Ndulu ili aruhusu uchotwaji wa fedha kutoka kwenye akunti ya Tegete Escrow.

Pia,imeripotiwa kuwa Gavana nae amekanusha kupokea barua yoyote kutoka kwa katibu wa raisi kuhusu akaunti hiyo ya Escrow.

CHANZO:Habarileo

UKAWA kwa kutunga uwongo na kutengeneza barua za kughushi hawajambo.
Wakiongea wanavyotoa macho bungeni unaweza dhani wanaongea ukweli kumbe ni kamba tu kuanzia maneno yao hadi viambatanisho vyao vya barua na viambatanisho vingine.

Iko haja ya mbunge anayetoa barua au viambatanisho vya kughushi bungeni aondolewe kinga na awe anaburuzwa mahakamani.Vinginevyo bunge litageuka kuwa kijiwe cha uongo na uzalishaji nyaraka feki.
 
Wanasiasa wanajaribu kutumia kila mbinu kuichafua IKULU , sijui ni kwa maslahi ya nani na kwa nini hayo hayakusemwa Bungeni hata kama CAG aliogopa kuandika kwa sababu wabunge wana kila aina ya Kinga na ndiyo maana hata LISSU alidiriki kumtukana Jk bila ya hatua zozote kuchukuliwa.
 
UKAWA kwa kutunga uwongo na kutengeneza barua za kughushi hawajambo.
Wakiongea wanavyotoa macho bungeni unaweza dhani wanaongea ukweli kumbe ni kamba tu kuanzia maneno yao hadi viambatanisho vyao vya barua na viambatanisho vingine.

Iko haja ya mbunge anayetoa barua au viambatanisho vya kughushi bungeni aondolewe kinga na awe anaburuzwa mahakamani.Vinginevyo bunge litageuka kuwa kijiwe cha uongo na uzalishaji nyaraka feki.

wanafikiri hiyo ndiyo gear ya ushindi serikali za mitaa, kweli wameishiwa.
 
UKAWA kwa kutunga uwongo na kutengeneza barua za kughushi hawajambo.
Wakiongea wanavyotoa macho bungeni unaweza dhani wanaongea ukweli kumbe ni kamba tu kuanzia maneno yao hadi viambatanisho vyao vya barua na viambatanisho vingine.

Iko haja ya mbunge anayetoa barua au viambatanisho vya kughushi bungeni aondolewe kinga na awe anaburuzwa mahakamani.Vinginevyo bunge litageuka kuwa kijiwe cha uongo na uzalishaji nyaraka feki.
Ni mbunge gani wa CCM aliethubutu kuomba muongoza kuhusu hilo na kuhoji uhalali wa document za wapinzani?

Acha ujuha!
 
UKAWA kwa kutunga uwongo na kutengeneza barua za kughushi hawajambo.
Wakiongea wanavyotoa macho bungeni unaweza dhani wanaongea ukweli kumbe ni kamba tu kuanzia maneno yao hadi viambatanisho vyao vya barua na viambatanisho vingine.

Iko haja ya mbunge anayetoa barua au viambatanisho vya kughushi bungeni aondolewe kinga na awe anaburuzwa mahakamani.Vinginevyo bunge litageuka kuwa kijiwe cha uongo na uzalishaji nyaraka feki.

Hili jambo limetamkwa siku nyingi Bungeni mbona halikukanuswa kipindi hicho. Mambo kama haya kucherewa kunanusha ndiyo yanaondoa imani kwa jibu hili.
 
Ujinga upuuzi wote ule ulioongelewa Bungeni kama kweli IKULU ilihusika wasingesita kuropoka, humu sasa tunapika majungu tu.

Mkuu hata kama una mahaba sio ki hivyo......Hivi kweli nafsi yako inakuambia ukweli kabisa kuwa Ikulu inaweza kusema Ni kweli huyo bwana amefanya hayo aliyofanya........ Uwe Mkweli tu wa nafsi
 
UKAWA kwa kutunga uwongo na kutengeneza barua za kughushi hawajambo.
Wakiongea wanavyotoa macho bungeni unaweza dhani wanaongea ukweli kumbe ni kamba tu kuanzia maneno yao hadi viambatanisho vyao vya barua na viambatanisho vingine.

Iko haja ya mbunge anayetoa barua au viambatanisho vya kughushi bungeni aondolewe kinga na awe anaburuzwa mahakamani.Vinginevyo bunge litageuka kuwa kijiwe cha uongo na uzalishaji nyaraka feki.

Nakumbuka ulivyoweweseka hadi ukaanzisha uzi ukimuita Suleiman Nchambi, Mbunge wa Kishapu (CCM) kuwa ni mwanasheria wa UKAWA. Pole sana mkubwa kwa upotoshaji ule uliopelekea uzi wako kufungwa na MODS faster!
 
wapo wanahabari ambao wanafaa kuandika habari za watoto wa shule za msingi tu mfano mwandishi kama wa tanzania daima unategemea ataandika kitu cha maana wao huandika anachosema mbowe basi kwahiyo wao kuchafua watu ni kawiada sana.
 
1. Sijui kwa nini kuna watu wanadhani chenge na wenzie wanaweza kuiba mabilioni wazi wazi kupitia mkombozi bank, wakati chenge huyo huyo ni bingwa wa kuficha fedha nje? kwa kupewa fedha kupitia benki ya nchini maana yake hakuwa na wasiwasi juu ya uhalali wa fedha zile. Vinginevyo kina chenge si wajinga kiasi hicho.
2. kuna watu wanadhani ikulu inaweza kuhusika kwenye wizi halafu ikaacha paper-trail?
 
watajibu watakavyo lakini ukweli tulishaujua na ukweli utasimama mapema sana subirini mtaona tu

kwani umejua ukweli gani ambao wewe unaona ni ukweli usio na shaka.
 
Back
Top Bottom