Ikulu yamtetea Prosper Mbena

Ikulu yamtetea Prosper Mbena

VYOMBO vya habari nchini vimeaswa kuripoti matukio yaliyofanyiwa uchunguzi wa kina na yenye kufuata maadili na taaluma ya habari, badala ya kufanya kazi kwa kuongozwa na ushabiki vinapotekeleza majukumu yake.

Hayo yameelezwa katika taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari ikikanusha kuhusika kwa Katibu wa Rais Jakaya Kikwete, Prosper Mbena katika kumpa mwongozo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu ili auruhusu uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyopo katika BoT.

Taarifa hiyo inasema baadhi ya vyombo vya habari (siyo HabariLeo) vimemhusisha Mbena kuingilia mchakato wa uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 306 katika akaunti hiyo iliyoibua hoja nzito nchini, kiasi cha Bunge kuingilia kati na kutaka baadhi ya mawaziri na watendaji serikalini wawajibike kwa kile kinachodaiwa kuchota fedha za umma, jambo ambalo bado halijathibitishwa rasmi. “Huu ni uongo na uzushi.

Ni jaribio jingine la kutia chumvi katika jambo ambalo limetawaliwa kwa kiasi kikubwa na mihemko ya aina yake.

Gavana Ndulu mwenyewe anathibitisha kuwa hajawahi kupokea barua yoyote kutoka kwa Katibu wa Rais kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow.

Akaunti ya Escrow ilifunguliwa baada ya kutokea kwa mgogoro wa kimaslahi baina ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL na Tanesco.


Chanzo:Habarileo

Kwanza hiyo source yenyewe tu eti "habari leo",si karatasi ya kufungia vitumbua hiyo na mihogo huku uswahilini kwetu.
 
...ikulu iliyokaliwa na wezi lazima wateteane....ndio maana hatua mpaka sasa hatua hazijachukuliwa kwa wezi....watanzania wanaona na wanasubiri....

kuwa na adabu, inaonekana hukufunzwa tabia njema na wazazi wako
 
kuwa na adabu, inaonekana hukufunzwa tabia njema na wazazi wako

..we juha mi wazazi wangu hawakunifundisha kuwaheshimu wezi...Inaelekea hamtaki kukubaliana na ukweli wa wezi kupanga ikulu yetu...lakini watanzania wanajua hivyo sasa...waambieni hivyo nyoka mnaowatetea hum jf.....
 
Kipande cha ripoti ya CAG kinasomeka kama ifuatavyo:


7.0. Ushauri wakuujulisha uongozi wa Nchi
Mnamo tarehe 24Oktoba, 2013, BoT ilimuandikia PST, ikimuomba kuchukua hatua kadhaa kuhusianana malipo ya IPTL. Miongoni mwa mambo yaliyoshauriwa na BoT yalikuwa ni:

  1. Kwamba ufungaji wa Escrow Account uzingatie kwamba mamlakaya kufanya hivyo yako kwa Paymaster General;
  2. Kwamba, kwa kuzingatia unyeti wa suala hili naukubwa wa malipo husika, Waziri wa Fedha apate fursa ya kuwajulisha MheshimiwaRais na Mheshimiwa Waziri Mkuu ili waeleze kama anaridhia au la; na
  3. Kwamba GoT iombe kutolewa kwa kingaitakayoikinga GoT dhidi ya madai yanayoweza kujitokeza baada ya malipo hayo kufanyika.

8.0. Kinga dhidiya Madai na Mashtaka
Baada ya kupokeamaombi hayo, BoT ilisisitiza kwamba ingependa kupata hakikisho kwamba baada yamalipo hayo, hakutakuwa na madai au mashtaka yoyote dhidi yake au GoT. Kutokanana msisitizo huo, tarehe 27 Oktoba, 2013, IPTL ilitoa hati ya Kinga (Indemnity) ambayo iliikinga BoT pamoja na GoT dhidi ya madai yote, ya sasa na ya baadae,mashauri ya kisheria, pamoja na kuahidi kuzifidia BoT na GoT gharama na tozo zozote ambazo zitawagharimu au zitakazotokana na uamuzi wao wa kuruhusu kuchukuliwa kwa fedha za Escrow au sehemu ya fedha hizo, kwa mujibu wa Makubaliano ya Kutoa Fedha.

9.0. Maombi yaTRA kuhusu VAT
Kwa barua iliyoelekezwa kwa PST na nakala kwa Gavana wa BoT,Mamlaka ya Mapato (TRA) iliomba msaada wa PST katika kukata kiasi cha Shilingi 26.9 bilioni, kama Kodiya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa malipo ambayo yaliwekwa kwenye Escrow Account. Kiasi hicho kilikokotolewa kutoka katika kiasi cha Shilingi 176,649,195,314.00 ambacho kilikadiriwa kuwepo katika Escrow Account.

Hata hivyo,katika ushauri ambao ulitolewa na AG tarehe 18 Novemba, 2013, ilielezwa kwamba malipo ya Capacity Charge hakikuhusishaVAT na kwamba kiasi chote kilichokuwamo katika Escrow Account kilikuwa ni malipo yaIPTL pasipo na VAT. Ushauri wa AG ulitokana na barua ya BoT na ile ya PSTambazo ziliomba ufafanuzi kuhusu suala hilo kabla ya uhamishaji wa fedha kwenda IPTL.

10.0. Kibali chakuhamisha fedha kwenda IPTL
Mnamo tarehe 14Novemba, 2013, PST aliwasilisha kwa utekelezaji, maagizo ya Mheshimiwa Raisambaye aliagiza kwamba “Maamuzi ya Mahakama Kuu yatekelezwe kama alivyoshauri AG”. Maagizo ya Mheshimiwa Rais yaliwasilishwa kwa PST kwa barua ya tarehe 13 Novemba, 2013, na ilisainiwa na Katibu wa Rais, Bwana Prosper Mbena.

Baada ya kupatamaelekezo hayo, BoT ilimwandikia PST, ikiomba muongozo kuhusiana na suala la madai ya TRA kuhusiana na VAT. Barua hii iliandikwa tarehe 15 Novemba, 2013, na nakala yake kupelekwa kwa AG, na ilizingatia ukweli kwamba madai ya kodi za Serikali yanachukuliwa kama madai yenye umuhimu wa juu (first charge) katika malipo yoyote.

Ni barua hii ndiyo iliyoleta ufafanuzi wa AG - kwa barua yake ya tarehe 18 Novemba, 2013- ambao ulisisitiza kwamba malipo ya capacitycharge hayakuwa na VAT na kwamba fedha zihamishwe kwenda IPTL bila kukata fedha za VAT.
 
..we juha mi wazazi wangu hawakunifundisha kuwaheshimu wezi...Inaelekea hamtaki kukubaliana na ukweli wa wezi kupanga ikulu yetu...lakini watanzania wanajua hivyo sasa...waambieni hivyo nyoka mnaowatetea hum jf.....

wape vidonge vyao.
Hatakama wameiba na ela wanazo lkn 2015 ndi mwisho Wao.

Et maisha bora. Sera yenye ni wizi tu.
 
Wezi utawajua tu kwa sarakasi zao.
Mahangaiko yao wataishia kuumbuka mwaka huu.
 
hata Membe alikanusha kuhusu meno ya Tembo na msafara Xi Jinping
 
kuwa na adabu, inaonekana hukufunzwa tabia njema na wazazi wako

Unahemuka kitu gani kama huna KIRUSI cha wizi kwenye damu yako au ni beneficiary wa wizi!! uliona wapi mwizi akakiri kuwa ni mwizi?! Usitufundishe woga, mwizi lazima aitwe mwizi, na muongo aitwe muongo,period., kwa neema za Mungu tunao tumbili wa kuwakamata wezi, bravo Kafulila, long live UKAWA
 
wabunge wengi huwa wanazungumza kwa sifa tu lakini ukiwaambia walete viambatisho au uthibitisho usikuwa na shaka mavi debe wanajivunia ile kinga ya bunge kuongea hata ujinga usiokuwa na maana.
Kwani mkuu ulikuwa unategemea jibu gani toka serikalini? Sisi wengine hilo ndilo jibu tulilolitegemea.

Sent from my SM-G800H using Tapatalk
 
Kawashtaki kama wametengeneza vya kughushi

Umemjibu vyema.Na ndiyo maana Singasinga anaipigisha kwata serikali sababu wamekul wote.Hivi utawezeje kama muwekezaji kumwambia kiongozi wa taasisi ambaye ni mteuliwa wa Rais awekwe jela sababu tu anatimiza majukumu yake.

Maskini Tanzania yangu.Hivi kwanini kama aliona hana uwezo wa kuongoza aliogombea? Kweli kabisa mpaka Sasa Tanzania hatuna rais bali tuna mtalii ambaye kwa sasa amelala eti ana ED.
 
Well said kurugenz ya mawasiliano.tunashukuru kwa kutoa taarifa na wameisikia
 
Back
Top Bottom