Ikulu yamkana aliyemtesa ulimboka

Mzushi ni atakaye jaribu kufunika na kuzuia tume huru!! ama sivyo aliyetajwa na ULI ndiye!!
Tume huru iwe na watu gani? SLAA, GENERALI ULIMMWENGU, KUBENEA, HELLEN KIJO BISIMBA, ANANILEYA NKYA? mbona hivi sasa wamenyamaza vurugu za PONDA na wenzake au wako busy na suala la ULIMBOKA? kazi kweli kweli.
 
WAKATI sakata la kutekwa, kuteswa na kisha kutupwa katika msitu wa Mwabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar ss Salaam kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk Steven Ulimboka, likiwa limefikia miezi mitatu, Ikulu imeibuka na kumkana mtumishi wake Ramadhan Ighondu anayetajwa kuhusika katika unyama huo.

Mwanzoni mwa wiki Dk. Ulimboka alitoa tamko akisema kwamba Ighondu ndiye aliyehusika na sakata la kumteka na kumtesa vibaya katika jaribio la kutaka kumuua.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumamosi, Ikulu jana, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, alisema kuwa hamfahamu mtumishi huyo aliyetajwa na Ulimboka. Alisisitiza kuwa Ikulu haipo kwa ajili ya kuteka na kutesa watu, hivyo wale wanaodai kuwa mtumishi wa ofisi hiyo anahusika na tukio hilo wanaongea tu.

“Wala simfahamu…Ikulu haipo kwa ajili ya kutesa watu na hao wanaomtaja mtumishi huyo kuwa yupo Ikulu hao wanazungumza tu,” alisema.

Wakati Balozi Sefue akitoa kauli hiyo, juzi Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, alisisitiza kuwa Ikulu haihusiki na
kwamba Rais Jakaya Kikwete alishalijibu suala hilo.

Katika tamko lake la kiapo lililotolewa kwa waandishi wa habari, Dk. Ulimboka, kupitia kwa wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Kicheere, alisema anamfahamu mtesaji wake, na kwamba hata akikamatwa leo hii, atakwenda kufanya utambuzi.

Alisema anashangaa kwamba polisi wameshindwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, licha ya kwamba alishatajwa na gazeti la MwanaHALISI na katika mtandao wa YouTube.

Alisema: “Nathibitisha kwamba Ramadhan Ighondu alitambulishwa kwetu kwa jina la Abeid. Binafsi ninamfahamu sana bwana huyu kwa sababu alikuwa akitumwa mara kwa mara kuja kukutana na mimi na tumekutana mara kadhaa kabla ya tukio lile.

“Nathibitisha kwamba mfanyakazi huyu wa Ikulu, ndiye aliyenipigia simu na kuniita kwenye kikao ambacho muda mfupi baadaye nilitekwa. Katika mawasiliano hayo, Abeid alikuwa anatumia simu namba 0713 760473.”

Dk. Ulimboka aliongeza kuwa, anakumbuka kuwa Abeid alitambulishwa kwake na kigogo mmoja, akiwa na wawakilishi wengine wa madaktari, kuwa ndiye angehusika katika kuchukua madai na hoja za madaktari katika mgogoro kati yao na serikali.

Kauli ya jana ya Balozi Sefue ni ya tatu kutolewa na Ikulu kuhusu Dk. Ulimboka. Mara ya kwanza, ilitolewa na Rais Jakaya Kikwete
alipokutana na baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ambapo alisema, “Dk. Ulimboka ana nini mpaka Ikulu imteke? Tumteke ili iweje?”

Kikwete alikwenda mbali zaidi na kusema hata Dk. Ulimboka mwenyewe alipokwenda Ikulu akiwa na viongozi wenzake, alinyamaza kimya tu na kwamba waliokuwa wakizungumza ni wengine.

Hata hivyo, kwa kuwa Ikulu imesema haihusiki, na Dk. Ulimboka mwenyewe ametamka kwamba anamjua aliyemtesa, na kwamba anafanya kazi Ikulu, ni juu ya umma kuamua nani anasema ukweli.

Juni 26, mwaka huu, Dk. Ulimboka alitekwa, akapigwa, akang’olewa kucha kabla ya kuokotwa msitu wa Mabwepande na kupelekwa katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) kwa matibabu. Hata hivyo, baadaye alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi na alirejea nchini Agosti 12, mwaka huu.

Source: Tanzania Daima

kwa mawasiliano na ulimboka,email

ulimboka@yahoo.com
 
Tume huru iwe na watu gani? SLAA, GENERALI ULIMMWENGU, KUBENEA, HELLEN KIJO BISIMBA, ANANILEYA NKYA? mbona hivi sasa wamenyamaza vurugu za PONDA na wenzake au wako busy na suala la ULIMBOKA? kazi kweli kweli.
Wewe kumbe una mengine yanayokusumbua pole sana!!
 
ikulu sasa hivi wapo chini ya uamsho.Ndio maana maana wamepewa siku kadhaa wakamrudisha kiongozi wao.hawajui impact ya wanayofanya.Next move ya uamsho ndio watawajua vyema baada ya hili promo la serikali.

Ikulu haiotosihia hapo kutoa majibu ya kuchekesha.
 
Kwamba ni mfanyakazi wa TISS Dr. Ulimboka asengejua. Umeambiwa alitambulishwa kwake na kigogo mmoja na walikuwa wakikutana naye kusuluhisha mgomo wa madaktari. Hapo ina maana alitambulishwa kama mfanya kazi wa ikulu na mpaka waende ikulu waliohusika kupanga vikao hivyo ni Ighondu huko ikulu. Kuwa ni mfanya kazi wa TISS inawezekana kwa kiasi kikubwa lakini inawezekana ikulu ilianza kumtumia kwa kazi hiyo huko huko ikulu. Kinachodhihiri ni kuwa ikulu inamfahamu Ramadhan Ighondu lakini alipelekwa ikulu kwa kazi maalum kama si mfanyakazi wa ikulu au ni mfanyakazi wa ikulu ila hawawezi kusema.

N i sawa kabisa unachosema, nilichofanya mimi ni kujaribu kuiweka wazi kona wanayojifichia Ikulu, ila ukweli unabaki vile vile kuwa mtesaji wa Dr. Uli ni serikali dhalimu na dhaifu ya CCM.
 
ulimbokatwisteditorial.jpg


HAYA RAHA TUPI IKULU; URAIS SIO MCHEZO wa BAO
 
Dr Ulimboka uliumizwa sana Tukamuomba Mungu Umepona Nakushauri hizi Habari uachane nazo hazina Tija Achana nazo fanya kazi kama ulishawastaki Subiri sheria ifanye kazi Sifurahishwi na hayo majibizano na White House
 
Ikulu wasikanushe tu kwenye media, kama kweli hawakuhusika kwa nini wasiunde tume huru? What's the point? Hapa ni tume huru tu itamaliza ubishi!
 
MUHIMU ni kuwa mhalifu anajulikana! hao serikali wanangoja nini kumtia nguvuni jambazi Rama Ighondu? Huyu ni wa TISS na huwa wanajitambulisha kuwa wanafanya IKULU!! SEFUE usitukoroge aisee!

vyovyote vile itakavyokuwa,hakuna mwenye akili timamu aliyedhani serikali inaweza kuibuka hadharani na kukiri waziwazi kuhusika na tukio hilo la kinyama,wanachofanya sasa hivi ni kujitetea tetea tu huku wakiwa na imani kwamba they will get away of the saga by the passage of time.kama sio wao waliouhusika na tukio hilo basi ni nani?wangapi wameshatiwa mbaroni kuhusiana na tukio hilo?upelelezi wake umefikia wapi?
 
Tu-asume Ikulu haihusiki ila Ramadhani Ighondu anahusika, sioni kwa nini serikali inachelea kumkamata huyu Ighondu au kakimbia nchi?
 
Dr Ulimboka uliumizwa sana Tukamuomba Mungu Umepona Nakushauri hizi Habari uachane nazo hazina Tija Achana nazo fanya kazi kama ulishawastaki Subiri sheria ifanye kazi Sifurahishwi na hayo majibizano na White House

dr. ulimboka is a real fighter na haogopi consequence yeyote. Kama walitaka kumuua wamuue basi cause he is not coward! DETERMINATION IS OUR MOTTO!! - mzumbe high school.
 
Back
Top Bottom