Ikulu yamkana aliyemtesa ulimboka

Si unajua hawa staff wa TISS wanapokuwa uraiani hujitambulisha kama wafanyakazi wa ofisi ya rais na ukienda wilayani hujitambulisha kama afisa tawala na ndio maana Dr. nadhani akajichanganya na kusema mfanyakazi wa Ikulu

Iwe anafanya wapi, Jina tayari limewekwa hadharani. Lazima IKULU ilikuwa inajua litakalotendeka. Mr LIWALO na LIWE alijua na lazima alim-"brief" Bosi wake Dhaifu kama "TOP SECRET"
 
WAKATI sakata la kutekwa, kuteswa na kisha kutupwa katika msitu wa Mwabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar ss Salaam kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk Steven Ulimboka, likiwa limefikia miezi mitatu, Ikulu imeibuka na kumkana mtumishi wake Ramadhan Ighondu anayetajwa kuhusika katika unyama huo.

Mwanzoni mwa wiki Dk. Ulimboka alitoa tamko akisema kwamba Ighondu ndiye aliyehusika na sakata la kumteka na kumtesa vibaya katika jaribio la kutaka kumuua.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumamosi, Ikulu jana, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, alisema kuwa hamfahamu mtumishi huyo aliyetajwa na Ulimboka. Alisisitiza kuwa Ikulu haipo kwa ajili ya kuteka na kutesa watu, hivyo wale wanaodai kuwa mtumishi wa ofisi hiyo anahusika na tukio hilo wanaongea tu.

“Wala simfahamu…Ikulu haipo kwa ajili ya kutesa watu na hao wanaomtaja mtumishi huyo kuwa yupo Ikulu hao wanazungumza tu,” alisema.

Wakati Balozi Sefue akitoa kauli hiyo, juzi Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, alisisitiza kuwa Ikulu haihusiki na
kwamba Rais Jakaya Kikwete alishalijibu suala hilo.

Katika tamko lake la kiapo lililotolewa kwa waandishi wa habari, Dk. Ulimboka, kupitia kwa wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Kicheere, alisema anamfahamu mtesaji wake, na kwamba hata akikamatwa leo hii, atakwenda kufanya utambuzi.

Alisema anashangaa kwamba polisi wameshindwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, licha ya kwamba alishatajwa na gazeti la MwanaHALISI na katika mtandao wa YouTube.

Alisema: “Nathibitisha kwamba Ramadhan Ighondu alitambulishwa kwetu kwa jina la Abeid. Binafsi ninamfahamu sana bwana huyu kwa sababu alikuwa akitumwa mara kwa mara kuja kukutana na mimi na tumekutana mara kadhaa kabla ya tukio lile.

“Nathibitisha kwamba mfanyakazi huyu wa Ikulu, ndiye aliyenipigia simu na kuniita kwenye kikao ambacho muda mfupi baadaye nilitekwa. Katika mawasiliano hayo, Abeid alikuwa anatumia simu namba 0713 760473.”

Dk. Ulimboka aliongeza kuwa, anakumbuka kuwa Abeid alitambulishwa kwake na kigogo mmoja, akiwa na wawakilishi wengine wa madaktari, kuwa ndiye angehusika katika kuchukua madai na hoja za madaktari katika mgogoro kati yao na serikali.

Kauli ya jana ya Balozi Sefue ni ya tatu kutolewa na Ikulu kuhusu Dk. Ulimboka. Mara ya kwanza, ilitolewa na Rais Jakaya Kikwete
alipokutana na baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ambapo alisema, “Dk. Ulimboka ana nini mpaka Ikulu imteke? Tumteke ili iweje?”

Kikwete alikwenda mbali zaidi na kusema hata Dk. Ulimboka mwenyewe alipokwenda Ikulu akiwa na viongozi wenzake, alinyamaza kimya tu na kwamba waliokuwa wakizungumza ni wengine.

Hata hivyo, kwa kuwa Ikulu imesema haihusiki, na Dk. Ulimboka mwenyewe ametamka kwamba anamjua aliyemtesa, na kwamba anafanya kazi Ikulu, ni juu ya umma kuamua nani anasema ukweli.

Juni 26, mwaka huu, Dk. Ulimboka alitekwa, akapigwa, akang’olewa kucha kabla ya kuokotwa msitu wa Mabwepande na kupelekwa katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) kwa matibabu. Hata hivyo, baadaye alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi na alirejea nchini Agosti 12, mwaka huu.

Source: Tanzania Daima

Umma unaamua kivipi yani, haya maneno ya uchochezi ndiyo hayatakiwi.
 
Iwe anafanya wapi, Jina tayari limewekwa hadharani. Lazima IKULU ilikuwa inajua litakalotendeka. Mr LIWALO na LIWE alijua na lazima alim-"brief" Bosi wake Dhaifu kama "TOP SECRET"

Hijo ni hisia tu.
 
Dr. Ulimboka amejichanganya katika hayo maelezo yake, Rama ni mfanyakazi wa TISS, na siyo Ikulu, ila haijaondoa ukweli kuwa Serikali dhalimu ya CCM ndiyo iliyopanga kumuua Dr. Ulimboka baada ya kushindwa kujibu hoja zake.

Huyu ulimboka alikuwa akikutana na Rama mara kwa mara wapi? Mbona hatujawahi kusikia mahusiano haya aidha akielezea hatua iliyofikiwa kutokana na mazungumzo hayo hadi kuteswa kwake?
 
Dr. Ulimboka amejichanganya katika hayo maelezo yake, Rama ni mfanyakazi wa TISS, na siyo Ikulu, ila haijaondoa ukweli kuwa Serikali dhalimu ya CCM ndiyo iliyopanga kumuua Dr. Ulimboka baada ya kushindwa kujibu hoja zake.
Kwamba ni mfanyakazi wa TISS Dr. Ulimboka asengejua. Umeambiwa alitambulishwa kwake na kigogo mmoja na walikuwa wakikutana naye kusuluhisha mgomo wa madaktari. Hapo ina maana alitambulishwa kama mfanya kazi wa ikulu na mpaka waende ikulu waliohusika kupanga vikao hivyo ni Ighondu huko ikulu. Kuwa ni mfanya kazi wa TISS inawezekana kwa kiasi kikubwa lakini inawezekana ikulu ilianza kumtumia kwa kazi hiyo huko huko ikulu. Kinachodhihiri ni kuwa ikulu inamfahamu Ramadhan Ighondu lakini alipelekwa ikulu kwa kazi maalum kama si mfanyakazi wa ikulu au ni mfanyakazi wa ikulu ila hawawezi kusema.
 
Wameshasahau, ndiye guyu huyu aliyeonekana katika msafara wa Rais pale jangwani alipokuwa akikagua mradi wa mabasi yaendayo kwa kas??Na picha watu wanazo akiwa karibu kabisa na JK?!!
 
Naungana na dr ulimboka kuitaka serikali iunde tume huru ili kuubaini ukweli!
 
Awe mfanyakazi wa ikulu ,au wa TISS hiyo itajulikana mbele kwa mbele. Kukanusha kwenye vyombo vya habari hiyo nayo siyo jambo kubwa au sheria.
Cha maana huyo Ighondu ameshatambuliwa ndiyo mtu wa kati aliyehusika kuchukua order kutoka anakokujua na kumuingiza kingi Uli kwa makuwadi wa kutoa roho za watu AKAMATWE NA AFIKISHWE MAHAKAMANI TU akajitete huko na kutaja washirika wake na siyo ikulu kukana tu wakati mtu yupo au labda wameshamuua naye kupoteza ushahidi.
 
Ramadhan Ighondu ni daktari kwa kong'oa meno na kucha bila Ganzi!

Atakuwa ni mmoja wa Madaktari wenzake aliowasaliti, inawezekanje mtu asiye daktari akawa na utaalamu wa kung'oa watu meno na kucha? Halafu huyo Ulimboka bwana amekopi na ku paste yale aliyoyaandika SAID KUBENEA kwa nini? Hii ikulu imekuwa kama kariakoo, kila mmoja anaishambulia hata ambaye nini maana ya IKULU. Mimi ningekuwa Serikali ewote hao wanaoeneza chuki kwa Serikali wote ningesweka ndani maanake sasa si huru wa kuongea bali uhuru wa kutukana.
 
WAKATI sakata la kutekwa, kuteswa na kisha kutupwa katika msitu wa Mwabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar ss Salaam kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk Steven Ulimboka, likiwa limefikia miezi mitatu, Ikulu imeibuka na kumkana mtumishi wake Ramadhan Ighondu anayetajwa kuhusika katika unyama huo.

Mwanzoni mwa wiki Dk. Ulimboka alitoa tamko akisema kwamba Ighondu ndiye aliyehusika na sakata la kumteka na kumtesa vibaya katika jaribio la kutaka kumuua.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumamosi, Ikulu jana, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, alisema kuwa hamfahamu mtumishi huyo aliyetajwa na Ulimboka. Alisisitiza kuwa Ikulu haipo kwa ajili ya kuteka na kutesa watu, hivyo wale wanaodai kuwa mtumishi wa ofisi hiyo anahusika na tukio hilo wanaongea tu.

“Wala simfahamu…Ikulu haipo kwa ajili ya kutesa watu na hao wanaomtaja mtumishi huyo kuwa yupo Ikulu hao wanazungumza tu,” alisema.

Wakati Balozi Sefue akitoa kauli hiyo, juzi Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, alisisitiza kuwa Ikulu haihusiki na
kwamba Rais Jakaya Kikwete alishalijibu suala hilo.

Katika tamko lake la kiapo lililotolewa kwa waandishi wa habari, Dk. Ulimboka, kupitia kwa wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Kicheere, alisema anamfahamu mtesaji wake, na kwamba hata akikamatwa leo hii, atakwenda kufanya utambuzi.

Alisema anashangaa kwamba polisi wameshindwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, licha ya kwamba alishatajwa na gazeti la MwanaHALISI na katika mtandao wa YouTube.

Alisema: “Nathibitisha kwamba Ramadhan Ighondu alitambulishwa kwetu kwa jina la Abeid. Binafsi ninamfahamu sana bwana huyu kwa sababu alikuwa akitumwa mara kwa mara kuja kukutana na mimi na tumekutana mara kadhaa kabla ya tukio lile.

“Nathibitisha kwamba mfanyakazi huyu wa Ikulu, ndiye aliyenipigia simu na kuniita kwenye kikao ambacho muda mfupi baadaye nilitekwa. Katika mawasiliano hayo, Abeid alikuwa anatumia simu namba 0713 760473.”

Dk. Ulimboka aliongeza kuwa, anakumbuka kuwa Abeid alitambulishwa kwake na kigogo mmoja, akiwa na wawakilishi wengine wa madaktari, kuwa ndiye angehusika katika kuchukua madai na hoja za madaktari katika mgogoro kati yao na serikali.

Kauli ya jana ya Balozi Sefue ni ya tatu kutolewa na Ikulu kuhusu Dk. Ulimboka. Mara ya kwanza, ilitolewa na Rais Jakaya Kikwete
alipokutana na baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ambapo alisema, “Dk. Ulimboka ana nini mpaka Ikulu imteke? Tumteke ili iweje?”

Kikwete alikwenda mbali zaidi na kusema hata Dk. Ulimboka mwenyewe alipokwenda Ikulu akiwa na viongozi wenzake, alinyamaza kimya tu na kwamba waliokuwa wakizungumza ni wengine.

Hata hivyo, kwa kuwa Ikulu imesema haihusiki, na Dk. Ulimboka mwenyewe ametamka kwamba anamjua aliyemtesa, na kwamba anafanya kazi Ikulu, ni juu ya umma kuamua nani anasema ukweli.

Juni 26, mwaka huu, Dk. Ulimboka alitekwa, akapigwa, akang’olewa kucha kabla ya kuokotwa msitu wa Mabwepande na kupelekwa katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) kwa matibabu. Hata hivyo, baadaye alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi na alirejea nchini Agosti 12, mwaka huu.

Source: Tanzania Daima
MUHIMU ni kuwa mhalifu anajulikana! hao serikali wanangoja nini kumtia nguvuni jambazi Rama Ighondu? Huyu ni wa TISS na huwa wanajitambulisha kuwa wanafanya IKULU!! SEFUE usitukoroge aisee!
 
Naungana na dr ulimboka kuitaka serikali iunde tume huru ili kuubaini ukweli!

Ulimboka anatapatapa tu, yaani kila anayekufa iundwe tume. Ajilaumu yeye mwenyewe Ulimboka, kitendo cha kuwa na maongezi faragha na watu asiyowajua ndicho kilichomponza, hivi huyu rama hawezi kuwa alitumwa na madakari wenzake baada ya kuona anawasaliti? Mimi binafsi ningeishauri serikali imbane vizuri Ulimboka pamoja na rafiki yake DEO wanajua walikuwa wanafanya maongezi ya faragha na nani? jana nimemsikiliza vizuri Daktari DEO akisema mara ya mwisho walikuwa lidaz Club na madaktari wengine muda mfupi kabla Ulimboka hajatekwa, ni akina nani hao madaktari mbona hawataji?
 
bado kila jambo lina mwanzo na mwisho!

vifo vya eagonjwa mbona amvitaji,mnamzungumzia ulimboka tu,kwani awo waliokufa au kupoteza maisha kwa sbb,ya mgomo ulioratibiwa na ulimboka awana samani??au mwenye samani ni ulimboka??upuuzi tu ulimboka kwani ni nani si ni mpuuzi mmoja tu awo waliomdunda awakumdunda vizuri,akutakiea kupona hata kidogo pambaafu kapisa.
 
Jama mwenye picha ya IGHONDU pls iwekeni hapa!!
810847697.jpg

othman_304.jpg
 
Awe mfanyakazi wa ikulu ,au wa TISS hiyo itajulikana mbele kwa mbele. Kukanusha kwenye vyombo vya habari hiyo nayo siyo jambo kubwa au sheria.
Cha maana huyo Ighondu ameshatambuliwa ndiyo mtu wa kati aliyehusika kuchukua order kutoka anakokujua na kumuingiza kingi Uli kwa makuwadi wa kutoa roho za watu AKAMATWE NA AFIKISHWE MAHAKAMANI TU akajitete huko na kutaja washirika wake na siyo ikulu kukana tu wakati mtu yupo au labda wameshamuua naye kupoteza ushahidi.

Yaani mfanyakazi wa IKULU alafu wamuue? tatizo la kufanyakazi kwa hisia ndo kama hivi, kila mtu atakuja na lake.
 
Hivi Ikulu mbona wanajiaibisha?kwa nini wanajitahidi kujitetea?Anayetakiwa kujibu hoja ya Dr ULIMBOKA ni ikulu au mhusika mwenyewe Ramadhani,kama ikulu haihusiki kwa nini wanakubali wachafuliwe kwa suala hili?hata kama hawamjui Ramadhani,lakini huyo kijana ni mtu ambaye yupo na anaishi nchi hii,kwa nini ikulu wasimtafute wamlete mbele ya waandishi wa habari yeye binafsi athibitishe kuwa hana mahusiano na ikulu na amehusika kumtesa ULIMBOKA au la na kama ndiyo alitumwa na nani,pia kwa nini polisi wasitumike kuisafisha ikulu kwa kuamriwa kumkamata Ramadhani na kumhoji au kumfungulia mashitaka na umma ujulishwe kilichotokea.Hapa kuna maigizo yanaendelea,atuhumiwe Ramadhani,Rywemamu ndo ajibu tuhuma,tutaelewa vip kuwa ikulu haihusiki kwa namna wanavyotapatapa
 
Back
Top Bottom