Wana jf, salaam. Waziri wa maliasili na utalii, lazaro nyalandu ameshinda vita. Kwa ghiliba na ushawishi wenye nguvu zisizo kifani, amefanikiwa kuwabadili mawazo wakuu wa ikulu akiwamo katibu mkuu kiongozi. Kwa nguvu hizo, profesa songorwa na profesa kidegesho sasa wanahamishwa wizarani na kupelekwa katika taasisi mbalimbali. Juzi, katibu mkuu kiongozi alimuita nyalandu na wakakamilisha mpango huo. Nyakandu amewaandaa watu wake ili bajeti yake ikwamishwe ktk bunge. Wanaotajwa kusimamia mpango huo ni wabunge wanne. Lengo lao ni kuhoji kwanini maazimio ya bunge yamepuuzwa kwa maprofesa kurejeshwa wizarani. Wanaotajwa ni lugora, lembeli, shelukindo (keshajilipua), sendeka na ndugai. Nchi hii imekufa! Wanaodai uraia wa nchi mbili wameona mbali. Nguvu za pesa zimeshinda.
Kamati ya Bunge ya maliasili na mazingira imekuwa na double standards. Katika sakata hilo Nyalandu naye alikuwepo wizarani. Inabidi haya mambo yachunguzwe. Isije ikawa kama Mfutakamba alivyotaka kutumia kamati ya Sserukamba kumshughulikia Nundu wakati naye alikuwa na yake.