Ikulu yabadili anuani ya Tovuti yake

Ikulu yabadili anuani ya Tovuti yake

Naomba abadili na jina la huu mtaa ilipo ikulu,maana naona aibu kuwa ikulu yetu ipo mtaa wa Barack Obama.
 
Hivi ni kwa nini barabara ya ikulu inaitwa BARACK OBAMA? Huu ni ujinga!
Kuna kina Mkwawa, Mirambo, Kinjeketile, etc!
Rais wa marekani ndo barabara ya ikulu inapewa jina lake?

Mkuu hata mimi inanikasirisha sana. Ni usanii wa Kikwete huo. Bora wangeacha jina la zamani!
 
Kweli nchi inaundwa upya sasa, hii ni saluti kwa rais wetu.
 
Kama inavyoonekana hapo chini tangu kuingia kwa Raisi Magufuli Ikulu yetu haitumii tena anwani ya .. gmail.com bali inatumia . Ikulu.co.tz !


1.jpg

Ingekuwa vema na hilo jina la "Barack Obama Road" likafutiliwa mbali.

Bado sijaona tatizo kwa nini Jina mtaa wa Luthuli liliondolewa.

Albert Luthuli kama history inavyoonyesha alikuwa ni Mwafrika wa kwanza Duniani kupata tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1960, ikiwa ni kuthamini mchango wake katika kupiga vita "apartheid".

Huyu Mmarekani wa juzi juzi ambaye anaishi, anawaza na kufikiri Kimarekani ndio aje kutubadilishia masuala yetu hapa!
 
Last edited by a moderator:
Nina muomba na kumsihi Mh Magufuli afutiliye mbali mwenge kama si kuuweka jumba la makumbusho, huu mwenge unatumia hela nyingi sana za taifa kuzunguka nchi nzima
 
Back
Top Bottom