Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 362
- 906
IKULU YA KWANZA YA KONGO.
Na.Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Sunday-4/07/2021
Marangu, Kilimanjaro, Tanzania
Picha hizo zinaonesha ikulu ya kwanza ya Kongo DRC, ikulu hiyo inaitwa "Palais de la Stanley" (Palace of Stanley) japo kwa Sasa hufahamika kama "Palace of Téké" jina hili la pili iliitwa na Mobutu Seseseko Kuku Ngwendu Wazabanga mwaka 1971, ntalieleza hilo mbele kidogo.
Ikulu hii ya "Palais de la Stanley" au "Palais de la Téké" ipo kaskazini mashariki mwa jiji la Kinshasa, katika kitongoji cha Gombe, ndani ya viunga vya Ngaliema barabara iendayo jijini Matadi kilometa 60 kabla ya mpaka wa jimbo la Kongo Central (zamani Bakongo) na jimbo la Kinshasa.
Ikulu hii ipo kwenye eneo lenye muinuko wa mita 2017 kutoka usawa wa bahari, eneo lote la ikulu hiyo lipo kwenye mlima hufamikao kama mlima Ngaliema, ambao pia kipindi cha ukoloni wa Mberigiji mlima huo uliitwa Mlima Stanley.
Ujenzi wa Ikulu hii................
Ikulu hii ilianza kujengwa mwaka 1901 na kukamilika mwaka 1905, jengo lake lilibuniwa na muhandisi wa majengo wa Kiberigiji aliyeitwa Marcel Lambrichs, wakati wa ujenzi wake lilijengwa kwa ajili ya makazi ya gavana wa Uberigiji nchini Kongo, lakini baadae kabla ya kukamilika kwake likabadilishwa matumizi na kuwa makazi rasmi ya gavana wa mkoa wa Leopoldville (Kinshasa ya Sasa), kisha ujenzi wa makazi ya gavana yakajengwa eneo jingine linalofahamika kama "palace de la Prima" (ambapo kwasasa ni makazi rasmi ya Waziri mkuu wa Kongo).
Japo baadae mwaka 1925 serikali ya Uberigiji ilianza ujenzi wa makazi mapya ya General Governor wa Belgium Congo eneo jingine la viunga vya Gombe, ambapo makazi hayo hufahamika kama "Palais de la Nation" au "Palace of the Nation" japo jengo hili pia huitwa majina ya utani ya "independence Hall", "Palace of Lumumba" na "Grade de la Kinshasa", hili jengo la "Palais de la Nation" Ndio lilotumika wakati wa sherehe za Uhuru wa Kongo mwaka 1960 na Ndio Patrice Lumumba alipo toa ile hutuba yake maarufu ya "speech of the Nation".
Palais de la Nation ilitumika kama makazi rasimi ya General Governor wa Kongo na baada ya Uhuru mwaka 1960 ilitumika kama bunge la Kongo mpaka mwaka 2001 pale raisi Joseph Kabila alipo anza kulitumia kama Ikulu ya Raisi wa Kongo.
Sasa turejee kwenye Ikulu ya "Palais de la Stanley"............
Ikulu ya "Palais de la Stanley" ilitumika kama makazi ya Governor wa Kinshasa (leopaldville) mpaka tarehe Juni 30, 1960, baada ya sherehe za Uhuru ambapo majengo hayo yakawa makazi rasmi ya Ikulu ya Kongo, ambapo raisi wa kwanza kuishi Ikulu hiyo alikuwa ni raisi wa kwanza wa Kongo Joséph Kasavubu, Kasavubu aliitumia "Palais de la Stanley" kama eneo la makazi ya Raisi japo ofisi zake zilikuwa Palais de la Nation.
Hivyo Ikulu ya Palais de la Stanley ikaendelea kuwa makazi ya Rais wa Jamhuri, Ikulu hiyo inaukubwa wa km za mraba 17km², Ipo kwenye eneo la Mlima Stanley.
Eneo hilo pia kuna wanyama kadhaa ambao walihamishiwa humo mwaka 1969 na Mobutu, baada ya mapinduzi yaliyo fanywa na Mobutu mwaka 1964 aliifanya Ikulu hiyo ya Palais de la Stanley kuwa Ikulu rasmi ya Kongo, kusini mwa Ikulu hiyo Mobutu alijenga kambi ya makomando iliyopewa Jina la Ngaliema camp au Camp 8179.
Mwaka 1971 wakati Mobutu alipo anzisha operation utamaduni aliibadilisha Jina la Ikulu hiyo na kuita Palais de la Téké, Jina "Téké" ni jina la chifu wa eneo hilo la Ngaliema ambae ndio aliyesaini Maktaba na Stanley kipindi cha ujio wa kikoloni, ikumbukwe kuwa kipindi cha mwaka 1971 ndio Raisi Mobutu alitangaza utaratibu wa kutumika majina ya asili kwa nchi nzima.
Ikulu hiyo imetumika kama makazi ya Raisi toka mwaka 1960 mpaka mwaka 1998 pale Mobutu alipofurushwa na Mzee Laurent Dezile Kabila, Mzee Kabila hakuitumia sana Ikulu hiyo badala yake alitumia makazi ya "Palais de la Marbre", Ikulu ambayo huko nyuma ilikuwa hekalu la mfalme Baudoin kipindi cha ukoloni, hiyo Palais de la Marbre ilijengwa kama nyumba ya mfalme wa Uberigiji kufikia iwapo ataitembelea Kongo.
Mwaka 2001 Joseph Kabila alipoingia madarakani baada ya baba yake Mzee Kabila kuwawa alibadili makazi ya Raisi na kuhamia Palais de la Nation, jengo ambalo lilitumika kama bunge huko nyuma, ikumbukwe kuwa mwaka 1998 jengo la Palace of people la Kinshasa lilibadiliswa matumizi na kuwa bunge la nchi hiyo mpaka Sasa.
Wakati wa utawala wa Mzee Kabila na Joseph Kabila na raisi wa sasa Felix Thisekedi Ikulu ya Palais de la Téké imeendelea kuwa makazi ya Raisi wa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Mara kadhaa raisi Kabila alipenda kufanya mapumziko yake kwenye Ikulu ya Palais de la Téké na hata vikao vyake kadhaa vya mawaziri vilifanyika kwenye Ikulu ya Palais de la Téké, mwaka 2011 rais Kabila alijenga majengo mengine upande wa kaskazini mwa Ikulu hiyo ya Palais de la Téké ambayo huitwa Nord wing au JKK wing.
Kwa Sasa Palais de la Téké ni moja ya makazi ya Raisi wa Kongo japo makazi rasmi ya raisi na ofisi ya Raisi wa Kongo DRC yamebaki kuwa Palais de la Nation.
Palais de la Téké imekuwa eneo lilopendwa na rais Kabila na hata raisi wa sasa Felix Tshikedi, ambapo wote hao husema kuwa Ikulu ya Palais de la Téké ni eneo tulivu kwakuwa lipo nje ya mji kidogo na mazingira yake ni mazuri kutokana na ubaridi juu ya kilima cha Mlima Ngaliema.
Palais de la Téké ndio mama wa mji wa NGALIEMA, hapo ndipo ilipo historia ya miaka 34 ya utawala wa Mobutu Seseseko Kuku Ngwendu Wazabanga.
Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
Copyright 2021, All Rights Reserved.
Maktaba Kuu.

written by Comred Mbwana Allyamtu•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana AllyamtuKwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
Copyright 2021, All Rights Reserved.
Maktaba Kuu.