Ikulu Vs gazeti la Mwananchi!

kukurupuka kwa salva na wenzake kumbe hakujaisha
 
Bora wameacha kutumia ki email cha Yahoo. Lakini naona Kiswahili bado kinawapiga chenga.
 
Bora wameacha kutumia ki email cha Yahoo. Lakini naona Kiswahili bado kinawapiga chenga.

Hata hivyo bado mawasiliano ya ikulu ya TZ hayajawa encripted na hii sijui wanafanya makusudi au ni kutokujua. Email za ikulu, mambo ya ndani, ulinzi na jkt zinakuwa intercepted bila hata kutumia akili nyingi. Mfano kuna server mbili za mambo ya ndani ziko wazi hata kwa wapita njia wenye high-tech-wifi.
 
Hivyo, Ikulu inapenda kuwaambia wananchi kuwa kama ilivyokuwa kwenye habari ile ya Mei 21, habari ya jana ya gazeti hilo pia siyo ya kweli na ni ya kufitinisha watu na inastahili kudharauliwa na kupuuzwa.

Mmh, sasa wananchi watawezeje kudharau na kupuuza kitu ambacho Ikulu imeshindwa si tu kudharau bali hata kukipuuza na imebidi itumie rasilimali za taifa kupinga? Si vyema na wananchi wakapewa haki ya kupima na kuamua kwa hiyari yao kama habari ya Mwananchi ina ukweli au la, badala ya kuamuriwa kudharau na kupuuza? Maana lugha iliyotumika sio hata ya kushauri wananchi wadharau na kupuuzia, bali wananchi wanaambiwa na kurugenzi ya mawasiliano kuwa habari iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi siyo ya kweli na inastahili kudharauliwa na kupuuzwa!

Annina
 
Kama salva yupo hivyo
je aliyemteua yupoje?
 
Houseboy uliyemtoa bush ataanzaje kukuletea umwamba??
Afate unayotaka au apotee kwako...
 
Serikali ya JK imekuwa kama mtu aliyeshika chungu cha moto. Inatapapata kujaribu kuweka sawa mambo katika mazingira tata na ambayo haiingii akilini kwa wajuzi wa mambo.

Inajibu hoja kwa kwa kujichanganya. Kama Mwaziri hawatumwi na mtu yeyote huko mikoani, huu Waraka wa kuwazuia kusafiri nje ulitolewa kwa madhumuni gani??.


 

Napata tabu sana na uelewa wa huyu mtu anaeitwa Salva Rweyemamu hapa IKULU. Siku zote kazi yake imekuwa ni propaganda za kupotosha mambo na wamekuwa wakimpotosha hata JK katika mengi na ndio maana mpaka leo IKULU haina vyombo vya hakika vya mawasiliano ikiwemo tovuti na hata hizo tovuti zao za Serikali ni utumbo mtupu kutokana na huyu kilaza kuwa pale. Huu Waraka niliwahi kuupost hapa kuhusu safari za watumishi wa UMMA wakiwemo mawaziri ambazo zinahitaji vibali vya wakubwa wao. Sasa akisema Mawaziri hawatumwi na yeyote..haiingii akilini kabisa kama si kujikangaya na kutapatapa.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
​


Anwani ya Simu: "UTUMISHI", DSM. Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
Simu Nambari: 2118531-4 S.L.P. 2483,
Fax: 2131365 Dar es Salaam,
​


Barua Pepe: permsec@estabs.go.tz

TANZANIA.​


Unapojibu tafadhali taja:​


Kumb. Na: EA 45/257/01 Tarehe: 27 Agosti, 2004​





WARAKA WA UTUMISHI NA.7 WA MWAKA 2004​



KIKOMO CHA SIKU ZA KUWA NJE YA KITUO CHA KAZI​




KWA WATUMISHI WA UMMA​




1:0. UTANGULIZI:​


1:1. Wakati huu ambapo mchango wa Utumishi wa Umma unatambuliwa
kuwa muhimu katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo ya jamii, Serikali inaweka mikakati ya kuhakikisha watumishi wanafanya kazi katika vituo vyao vya kazi kwa sehemu kubwa ya muda wao wa kazi. Hapo hapo Serikali inatambua umuhimu wa watumishi wa umma kujiongezea ujuzi wa kazi kwa kushiriki katika kongamano za kitaaluma.​



1:2. Pia Serikali imeweka viwango vya posho za safari za nje ya vituo vya
kazi kwa siku vinavyokidhi gharama za kujikimu ambavyo ni vya kiwango cha juu na vinavyoongeza matumizi ya Serikali.​


1:3. Nyaraka za Rais Na.1 wa mwaka 1992 na Na.1 wa mwaka 1998 zimesisitiza kupunguza safari za watumishi ili kupunguza matumizi ya Serikali.​


2:0. MADHUMUNI YA WARAKA​


2:1. Ili kuhakikisha maelekezo haya yanatekelezwa ipasavyo sasa inaagizwa kwamba mtumishi hataruhusiwa kuwa nje ya kituo chake cha kazi kwa sababu za kikazi, mafunzo mafupi, kuhudhuria warsha, kongamano na mengineyo kwa zaidi ya siku za kazi sitini (60) kwa kila mwaka wa fedha.​



2:2. Pale inapobidi kuzidisha siku sitini itabidi yatolewe maelezo ya kina
yatakayomridhisha msimamizi wa kazi.​


2:3. Pamoja na Waraka huu tumeanzisha fomu maalum – (TFN 856 &
856A) za kujazwa na mtumishi na kuidhinishwa na msimamizi wake wa
kazi.
3:0. UTARATIBU UTAKAOTUMIKA KUANZIA TAREHE YA KUANZA
KUTUMIKA KWA WARAKA HUU​


Utaratibu ufuatao utatumika kwa watumishi wa umma wanaosafiri nje ya
kituo cha kazi.​


3:1. Kiwango cha juu cha muda wa kusafiri nje ya kituo cha kazi kitakuwa
siku SITINI (60) KWA MWAKA WA FEDHA.​


3:2. Kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma safari zote kwa madhumuni tajwa zitaidhinishwa kwa kuzingatia utaratibu ufuatao:-
3:2:1. Makatibu Wakuu na Wakuu wa Idara za Serikali Zinazojitegemea safari zitaidhinishwa na Katibu Mkuu Kiongozi baada ya kushauriana na Waziri wa Wizara/Idara inayohusika.
3:2:2. Makatibu Tawala wa Mikoa safari zitaidhinishwa na Wakuu wa
Mikoa.​


3:2:3. Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za
Serikali za Mitaa, safari hizo zitaidhinishwa na Wakuu wa Wilaya.​


3:3. Kwa Watumishi wengine wote, safari hizo zitaidhinishwa na Watendaji
Wakuu wa sehemu zao za kazi.​


3:4. Inashauriwa kuwa Mikutano, Semina, Jopo na Makongamano ipunguzwe sana na kubakia ile ya muhimu tu ambayo ina mwelekeo wa mafunzo muhimu kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi.​


3:5. Pia Watendaji Wakuu wasiende safari na Wasaidizi wao Wakuu kwa wakati mmoja na kuacha eneo lao la kazi bila kiongozi mwenye uwezo wa kutoa maamuzi au ufafanuzi wa mambo muhimu yanayoihusu Taasisi yao.​


3:6. Mtumishi yeyote aliyepata kibali cha kusafiri, akisharudi kutoka safari lazima athibitishe kwamba alikaa huko alikokwenda kwa muda wa siku​



alizoomba au alizoruhusiwa kwa kuandika ripoti ya kazi ya safari yake
na kumkabidhi kiongozi wake wa kazi.​


4. TAREHE YA KUANZA KUTUMIKA
Waraka huu unaanza kutumika tarehe 1 Septemba, 2004.​





Joseph A. M. Rugumyamheto​



KATIBU MKUU (UTUMISHI)​



 
Nilikuwa Sifahamu kumbe moja ya Job Description za Mawaziri ni Kufafanua Mafanikio ya Serikali kwa Wananchi.

Hii ni failuire ya ku-compose watu wanaofaa kuwa ikulu. Hao mawaziri wana umoja gani huo unaowafanya wote kwa pamoja waamuwe kwenda mikoani bila kutumwa? Au sasa ndo wanaonyesha kihelehele cha uongozi wao?

Hiyo kurugenzi lazima ikubali kwamba boss wao ni mzigo na kila wakati ni mihangaiko ya kumusafisha. Eti mazungumzo na TUCTA! Si mpangaji wetu alisema hahitaji kura za wafanyakazi?
 
Duuuu!!!!!!.Kwakweli Sijui jamii tunafundishwa nini katika hili? Mungu ibariki Tanzania.Tusioweza kuwa Vubaraka Tuna wakati Mgumu sana,Na mambo haya hayapo Serikalini tu,hata katika mashirika Binafsi,Usipokuwa kibaraka hupati haki zako za msingi.Wajameni?????Kweli kazi ipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…