Ikulu sio usukani wa kurudishia visasi

Ikulu sio usukani wa kurudishia visasi

Mbeke

Member
Joined
Aug 5, 2012
Posts
30
Reaction score
3
HIVI NDIVYO LOWASSA ALISHIRIKI RICHMOND
***********************************
26th October 2009​
*Nyaraka zaonyesha kila hatua aliweka mikono yake.
*Uthibitisho wa kuibeba Richmond watolewa peupe.
*Kumbe ndiye aliipora Tanesco kazi ya kusaka mzabuni.
*Wizara ya Nishari na Madini ilisubiri maamuzi yake.

Kilio cha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, bungeni kwamba alidhalilishwa sana kwa kuhusishwa na mkataba tata wa kampuni ya Richmond, si lolote wala chochote baada ya uchunguzi wa kina wa nyaraka uliofanywa na gazeti hili kubaini kwamba alihusika vilivyo katika mchakato mzima wa
zabuni hiyo.

Nyaraka kadhaa ambazo Nipashe imeziona, zimethibitisha si tu ushiriki wa Lowassa katika mchakato huo, bali alikuwa anatoa maelekezo ya nini kifanyike kwa kila hatua.

Nyaraka hizo zinaonyesha kwamba Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, Dk. Ibrahim Msabaha, alibakia kuwa kama karani tu wa kutekeleza maagizo ya Lowassa, kila hatua alikuwa anaamua Lowassa na kuifanya Wizara ya Nishati na Madini kutekeleza kile alichotaka
kiongozi huyo aliyejiuzulu Februari mwaka jana huku akilalamika kwamba ameonewa kwa kuzushiwa mambo kuhusu kashfa ya Richmond.

Akitii maagizo kutoka kwa Waziri Mkuu Lowassa, Dk. Msabaha, naye alimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Athur
Mwakapugi, Juni 21, 2006 akimwagiza atekeleze maagizo wa Waziri Mkuu ya kusaini mkataba na Richmond.

Kwa kifupi barua hiyo inasomeka hivi…"Iagize Tanesco iingie mkataba na kampuni ya Richmond
kwa ajili ya umeme wa kukodisha haraka iwezekanavyo. Nakuletea nakala ya kibali kilichotolewa kutoka ofisi ya Mhe. Waziri Mkuu kwa kumbukumbu za Wizara."

Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, Katibu Mkuu huyo, wakati huo, Arthur Mwakapugi, baada ya kupata maelekezo toka kwa waziri wake, naye alitoa maagizo siku hiyo hiyo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Balozi Fulgence Kazaura,
akimwagiza kuhakikisha shirika hilo linaingia mkataba na Richmond.

Maelezo hayo ambayo aliyaandika kwa mkono yalisomeka kwa kifupi... "Andaa barua kwa Mwenyekiti wa Tanesco kumuagiza waingie mkataba na Richmond."

Taarifa zinaonyesha kuwa baada kampuni ya Richmond Development Company LLC kuingia mkataba na Tanesco Juni 23, 2006 na baada ya
siku kusonga mbele bila kuwepo kwa dalili yoyote ya kupatikana kwa umeme wake katika kipindi cha siku 60 kama walivyosema wenyewe, maneno yalianza kuzagaa miongoni mwa wananchi, vyombo vya habari na hata baadhi ya wabunge, hivyo Lowassa akahisi kuwa kazi aliyokuwa ameisimamia kwa nguvu zote amechemsha na hivyo kutoa maelekezo mapya.

Katika maelekezo hayo, Lowassa kwa barua yake kwenda kwa Waziri Msahaba alisema: "Kama unavyofahamu yapo maneno mengi sana yanasemwa kuhusu uwezo wa kampuni tajwa (yaani Richmond) kuagiza Gas Turbines kama alivyopewa mkataba na Tanesco baada ya kushinda zabuni Yameandikiwa pia kwenye Gazeti la Thisday la jana (20.09.06).

"Inawezekana hivi vikawa ni vita vya kibiashara. Lakini kwa sababu ya meneno hayo yanasemwa na watu wengi na tofauti ni vizuri UKAJIRIDHISHA kwamba kampuni hii itaweza kutekeleza kazi hiyo. Kama utaona shaka lolote ni vizuri
kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu mapema ili tuweze kuchukua hatua zinazopasa mara moja."

Aidha, Lowassa akijua kwamba kuna jambo linazidi kuumuka juu ya Richmond, katika barua hiyo ya Septemba 21, 2006 alijipa moyo akisema: "Kwa upande mwingine kwa kuwa malipo yake ni kwa L/C hawezi kupata nafasi ya ‘kuturusha'. Ila unachoweza kufanya ni kuweka utaratibu wa
kumfuatilia kwa karibu ili kuhakikisha kwamba analeta ‘turbines' hizo zenye kiwango na kwa wakati. Napenda kupata taarifa za ufuatiliaji wa suala hili kila siku; bila kukosa."

Ushiriki wa Lowassa haukuishia kwenye barua hiyo aliyoandika na kuisaini mwenyewe Septemba
21, 2006 tu; bali ushiriki wake mwingine unaonekana katika waraka wa Waziri Msabaha,
aliyegeuzwa karani katika mchakato mzima huo,
kwenda kwa Mwenyekiti wa bodi ya Tanesco, Balozi Flugence Kazaura.

Dk. Msabaha anamtaarifu Balozi Kazaura kuwa suala la kushughulikia mashine za umeme wa kukodi limekwisha kushughulikiwa na Waziri Mkuu Lowassa.

Katika barua hiyo ambayo pia Nipashe ilifanikiwa kuiona ya Aprili 12, 2006 inasema ifuatavyo:

"Nadhani hatukuelewana vizuri. Suala la kushughulikia gas turbines za kukodisha lilishashughulikiwa na Mhe. Waziri Mkuu, ambaye aliunda Kamati ya wataalam watatu – KM-
Hazina, KM Nishati na AG. Nia ni kuliondoa suala zima kwenye mikono ya Menejimenti ya Tanesco
ambayo imeshindwa kulishughulikia kwa ufanisi."

Kwa barua hiyo, si tu kwamba Dk. Msahaba aliweka wazi msimamo wa Lowassa katika suala zima la ukodishaji wa mitambo hiyo, bali pia alionyesha jinsi ilikuwa imekubalika kuwaweka pembeni Tanesco ambao walikuwa ni wataalam wa mitambo hiyo kuliko mtu mwingine yeyote kwenye masuala ya uzalishaji umeme.

"Waache Kamati iliyoteuliwa kufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na BODI yako na wataalam wa Tanesco kwa kadri watakavyoona inafaa. Pasiwe tena na picha kama vile Menejimenti ya Tanesco imerejeshewa kazi hiyo, maana huko kutakuwa ni kukiuka maagizo ya Mhe. Waziri Mkuu," kwa kauli hiyo ni dhahiri Lowassa alikuwa ndiye anayejua mwelekeo wa kile alichokuwa anakitaka.

Mikono ya Lowassa katika sakata la Richmond haipo tu kwenye kumwagiza Dk. Msabaha na Kamati ya Makatibu pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini pia inaonekana jinsi alivyobariki mapendekezo ya Timu ya Majadilino ya Serikali (GNT) iliyojadiliana na Richmond.

Kwa mujibu wa barua nyingine ya Waziri Msabaha ambayo pia Nipashe imefanikiwa kuiona ya Juni 17, 2006 siku sita tu kabla ya mkataba wa Richmond kusainiwa inaonyesha alivyoelezwa hatua kwa hatua za majadiliano baina ya GNT na Richamond na jinsi utekelezaji wa mkataba utakavyokuwa.

Katika barua hiyo, Lowassa alielezwa gharama za kuleta mitambo hiyo na mpangilio mzima wa kuileta kwa awamu tatu, kwa kuonyesha alivyokuwa amelipa suala hilo kipaumbele, Juni 21, 2006 Lowassa kupitia kwa Katibu wake,
aliyetambulika kama B. Olekuyan, alimtaarifu Katibu wa Waziri wa Nishati na Madini majibu ya bosi wake.

Majibu yalisema ifuatavyo:
"Mheshimwa Waziri Mkuu amekubali mapandekezo na ushauri wa Mheshimiwa Waziri. Tafadhali mjulishe."

Kwa kasi ya ajabu, siku hiyo hiyo, Dk. Msabaha akiwa anafanyia kazi majibu ya Lowassa, alimwagiza Katibu Mkuu wake, Arthur Mwakapugi, hatua za kuchukua juu mkataba wa Richmond.

"Serikali imekubali mapandekezo ya Wizara kuwa Tanesco iagizwe kuingia mkataba wa kuleta Gas
Turbines za kukodisha za jumla ya MW 105.6 na kampuni ya Richmond kwa mtiririko uliopendekezwa katika makubaliano kati ya Kampuni ya Richmond ya Marekani na GNT,"
ilisema barua hiyo na kuongeza kuwa:

"Iagize Tanesco iingie mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya umeme wa kukodisha haraka iwezekanavyo. Nakuletea kibali kilichotolewa kutoka kwa Ofisi ya Mhe. Waziri Mkuu kwa kumbukumbu za Wizara."

Mwakapugi naye kwa kasi kama ya Waziri Msabaha, siku hiyo hiyo, aliagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco aagize Tanesco waingie
mkataba na Richmond. Mkataba ambao kwa mujibu wa kumbukumbu za Kamati Teule ya
Bunge iliyochunguza mchakato wa mkataba wa Richmond, ulisainiwa usiku kwa haraka hizo hizo siku mbili baadaye.

Mikono ya Lowassa pia ilionekana kwenye mkataba wa Richmond kama waraka wa ndani wa Waziri Msabaha kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara akieleza kuwa Waziri Mkuu ameamrisha Richmond wapewe dili nyingine ya kuzalisha
megawati 40 za umeme.

Waraka huo wa Julai 13, 2006 baada ya kusainiwa kwa mkataba wa Richmond na Tanesco, unasema:

"Nimezungumza tena na Mheshimiwa Waziri Mkuu leo juu ya bei ya mitambo ya Aggreko. Msimamo ni uleule niliokueleza awali na ameagiza tuulize Richmond kama anaweza kutoa 40 MW kwa bei isiyozidi ile ile ya 4.99 cents per kwh na kama tunaweza kuipata basi achukuliwe Richmond."

Kwa maelekezo ya Lowassa, Msabaha katika barua hiyo kwa Katibu Mkuu alisema: "Nimempigia simu Mohamed Gire wa kampuni ya
Richmond juu ya upatikanaji wa hizo MW 40. Gire amekubali kuwa anaweza kutoa MW 40 za ziada ifikapo Septemba na kwa bei hiyo ya USD cents 4.99 @ kwh. Amesema hatahitaji majadiliano
mapya. Inatosha kama ataandikiwa barua tu ya nyongeza MW 40."

Kwa mtiririko mzima wa kusakwa kwa Richmond, hakuna hata hatua moja ambayo Lowassa anaweza kudai hakuhusika katika mchakato
mzima, na kama vile Dk. Msabaha alikuwa anajua kitakachotokea wakati wote alionyesha kwamba
alikuwa akifanyia kazi maelekezo ya bosi wake, yaani Lowassa.

Kuna habari kwamba wakati Serikali itakapowasilisha ripoti ya utekelezaji wa maazimo ya Bunge juu ya Richmond, hoja ya kutaka
kusafishwa kwa Lowassa itaibuka ikilenga kuionyesha kwamba alionewa na Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza mchakato wa mkataba wa Richmond na Tanesco.

SOURCE: NIPASHE
 
Hatudanganyiki kwa maneno ya maccm kama EL alihusika richmond kwa nn miaka yote saba hajapelekwa mahakamani? je mbona suala la EPA watu mpaka mida hii wameishahukumiwa na ESCROW wameitwa kwenye kamati ya maadili vp kuhusu RICHMOND? Jibu ni jepesi tu kuwa RICHMOND mwizi aliyehusika ana kinga ya kisheria bali kina EL walijitoa kafara!
 
HIVI NDIVYO LOWASSA ALISHIRIKI RICHMOND
***********************************

*Nyaraka zaonyesha kila hatua aliweka mikono yake.
*Uthibitisho wa kuibeba Richmond watolewa peupe.
*Kumbe ndiye aliipora Tanesco kazi ya kusaka mzabuni.
*Wizara ya Nishari na Madini ilisubiri maamuzi yake.

Kilio cha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, bungeni kwamba alidhalilishwa sana kwa kuhusishwa na mkataba tata wa kampuni ya Richmond, si lolote wala chochote baada ya uchunguzi wa kina wa nyaraka uliofanywa na gazeti hili kubaini kwamba alihusika vilivyo katika mchakato mzima wa
zabuni hiyo.

Nyaraka kadhaa ambazo Nipashe imeziona, zimethibitisha si tu ushiriki wa Lowassa katika mchakato huo, bali alikuwa anatoa maelekezo ya nini kifanyike kwa kila hatua.

Nyaraka hizo zinaonyesha kwamba Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, Dk. Ibrahim Msabaha, alibakia kuwa kama karani tu wa kutekeleza maagizo ya Lowassa, kila hatua alikuwa anaamua Lowassa na kuifanya Wizara ya Nishati na Madini kutekeleza kile alichotaka
kiongozi huyo aliyejiuzulu Februari mwaka jana huku akilalamika kwamba ameonewa kwa kuzushiwa mambo kuhusu kashfa ya Richmond.

Akitii maagizo kutoka kwa Waziri Mkuu Lowassa, Dk. Msabaha, naye alimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Athur
Mwakapugi, Juni 21, 2006 akimwagiza atekeleze maagizo wa Waziri Mkuu ya kusaini mkataba na Richmond.

Kwa kifupi barua hiyo inasomeka hivi…“Iagize Tanesco iingie mkataba na kampuni ya Richmond
kwa ajili ya umeme wa kukodisha haraka iwezekanavyo. Nakuletea nakala ya kibali kilichotolewa kutoka ofisi ya Mhe. Waziri Mkuu kwa kumbukumbu za Wizara.”

Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, Katibu Mkuu huyo, wakati huo, Arthur Mwakapugi, baada ya kupata maelekezo toka kwa waziri wake, naye alitoa maagizo siku hiyo hiyo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Balozi Fulgence Kazaura,
akimwagiza kuhakikisha shirika hilo linaingia mkataba na Richmond.

Maelezo hayo ambayo aliyaandika kwa mkono yalisomeka kwa kifupi... “Andaa barua kwa Mwenyekiti wa Tanesco kumuagiza waingie mkataba na Richmond.”

Taarifa zinaonyesha kuwa baada kampuni ya Richmond Development Company LLC kuingia mkataba na Tanesco Juni 23, 2006 na baada ya
siku kusonga mbele bila kuwepo kwa dalili yoyote ya kupatikana kwa umeme wake katika kipindi cha siku 60 kama walivyosema wenyewe, maneno yalianza kuzagaa miongoni mwa wananchi, vyombo vya habari na hata baadhi ya wabunge, hivyo Lowassa akahisi kuwa kazi aliyokuwa ameisimamia kwa nguvu zote amechemsha na hivyo kutoa maelekezo mapya.

Katika maelekezo hayo, Lowassa kwa barua yake kwenda kwa Waziri Msahaba alisema: “Kama unavyofahamu yapo maneno mengi sana yanasemwa kuhusu uwezo wa kampuni tajwa (yaani Richmond) kuagiza Gas Turbines kama alivyopewa mkataba na Tanesco baada ya kushinda zabuni Yameandikiwa pia kwenye Gazeti la Thisday la jana (20.09.06).

“Inawezekana hivi vikawa ni vita vya kibiashara. Lakini kwa sababu ya meneno hayo yanasemwa na watu wengi na tofauti ni vizuri UKAJIRIDHISHA kwamba kampuni hii itaweza kutekeleza kazi hiyo. Kama utaona shaka lolote ni vizuri
kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu mapema ili tuweze kuchukua hatua zinazopasa mara moja.”

Aidha, Lowassa akijua kwamba kuna jambo linazidi kuumuka juu ya Richmond, katika barua hiyo ya Septemba 21, 2006 alijipa moyo akisema: “Kwa upande mwingine kwa kuwa malipo yake ni kwa L/C hawezi kupata nafasi ya ‘kuturusha’. Ila unachoweza kufanya ni kuweka utaratibu wa
kumfuatilia kwa karibu ili kuhakikisha kwamba analeta ‘turbines’ hizo zenye kiwango na kwa wakati. Napenda kupata taarifa za ufuatiliaji wa suala hili kila siku; bila kukosa.”

Ushiriki wa Lowassa haukuishia kwenye barua hiyo aliyoandika na kuisaini mwenyewe Septemba
21, 2006 tu; bali ushiriki wake mwingine unaonekana katika waraka wa Waziri Msabaha,
aliyegeuzwa karani katika mchakato mzima huo,
kwenda kwa Mwenyekiti wa bodi ya Tanesco, Balozi Flugence Kazaura.

Dk. Msabaha anamtaarifu Balozi Kazaura kuwa suala la kushughulikia mashine za umeme wa kukodi limekwisha kushughulikiwa na Waziri Mkuu Lowassa.

Katika barua hiyo ambayo pia Nipashe ilifanikiwa kuiona ya Aprili 12, 2006 inasema ifuatavyo:

“Nadhani hatukuelewana vizuri. Suala la kushughulikia gas turbines za kukodisha lilishashughulikiwa na Mhe. Waziri Mkuu, ambaye aliunda Kamati ya wataalam watatu – KM-
Hazina, KM Nishati na AG. Nia ni kuliondoa suala zima kwenye mikono ya Menejimenti ya Tanesco
ambayo imeshindwa kulishughulikia kwa ufanisi.”

Kwa barua hiyo, si tu kwamba Dk. Msahaba aliweka wazi msimamo wa Lowassa katika suala zima la ukodishaji wa mitambo hiyo, bali pia alionyesha jinsi ilikuwa imekubalika kuwaweka pembeni Tanesco ambao walikuwa ni wataalam wa mitambo hiyo kuliko mtu mwingine yeyote kwenye masuala ya uzalishaji umeme.

“Waache Kamati iliyoteuliwa kufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na BODI yako na wataalam wa Tanesco kwa kadri watakavyoona inafaa. Pasiwe tena na picha kama vile Menejimenti ya Tanesco imerejeshewa kazi hiyo, maana huko kutakuwa ni kukiuka maagizo ya Mhe. Waziri Mkuu,” kwa kauli
hiyo ni dhahiri Lowassa alikuwa ndiye anayejua mwelekeo wa kile alichokuwa anakitaka.

Mikono ya Lowassa katika sakata la Richmond haipo tu kwenye kumwagiza Dk. Msabaha na Kamati ya Makatibu pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini pia inaonekana jinsi alivyobariki mapendekezo ya Timu ya Majadilino ya Serikali (GNT) iliyojadiliana na Richmond.

Kwa mujibu wa barua nyingine ya Waziri Msabaha ambayo pia Nipashe imefanikiwa kuiona ya Juni 17, 2006 siku sita tu kabla ya mkataba wa Richmond kusainiwa inaonyesha alivyoelezwa hatua kwa hatua za majadiliano baina ya GNT na Richamond na jinsi utekelezaji wa mkataba utakavyokuwa.

Katika barua hiyo, Lowassa alielezwa gharama za kuleta mitambo hiyo na mpangilio mzima wa kuileta kwa awamu tatu, kwa kuonyesha alivyokuwa amelipa suala hilo kipaumbele, Juni 21, 2006 Lowassa kupitia kwa Katibu wake,
aliyetambulika kama B. Olekuyan, alimtaarifu Katibu wa Waziri wa Nishati na Madini majibu ya bosi wake.

Majibu yalisema ifuatavyo:
“Mheshimwa Waziri Mkuu amekubali mapandekezo na ushauri wa Mheshimiwa Waziri. Tafadhali mjulishe.”

Kwa kasi ya ajabu, siku hiyo hiyo, Dk. Msabaha akiwa anafanyia kazi majibu ya Lowassa, alimwagiza Katibu Mkuu wake, Arthur Mwakapugi, hatua za kuchukua juu mkataba wa Richmond.

“Serikali imekubali mapandekezo ya Wizara kuwa Tanesco iagizwe kuingia mkataba wa kuleta Gas
Turbines za kukodisha za jumla ya MW 105.6 na kampuni ya Richmond kwa mtiririko uliopendekezwa katika makubaliano kati ya Kampuni ya Richmond ya Marekani na GNT,”
ilisema barua hiyo na kuongeza kuwa:

“Iagize Tanesco iingie mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya umeme wa kukodisha haraka iwezekanavyo. Nakuletea kibali kilichotolewa kutoka kwa Ofisi ya Mhe. Waziri Mkuu kwa kumbukumbu za Wizara.”

Mwakapugi naye kwa kasi kama ya Waziri Msabaha, siku hiyo hiyo, aliagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco aagize Tanesco waingie
mkataba na Richmond. Mkataba ambao kwa mujibu wa kumbukumbu za Kamati Teule ya
Bunge iliyochunguza mchakato wa mkataba wa Richmond, ulisainiwa usiku kwa haraka hizo hizo siku mbili baadaye.

Mikono ya Lowassa pia ilionekana kwenye mkataba wa Richmond kama waraka wa ndani wa Waziri Msabaha kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara akieleza kuwa Waziri Mkuu ameamrisha Richmond wapewe dili nyingine ya kuzalisha
megawati 40 za umeme.

Waraka huo wa Julai 13, 2006 baada ya kusainiwa kwa mkataba wa Richmond na Tanesco, unasema:

“Nimezungumza tena na Mheshimiwa Waziri Mkuu leo juu ya bei ya mitambo ya Aggreko. Msimamo ni uleule niliokueleza awali na ameagiza tuulize Richmond kama anaweza kutoa 40 MW kwa bei isiyozidi ile ile ya 4.99 cents per kwh na kama tunaweza kuipata basi achukuliwe Richmond.”

Kwa maelekezo ya Lowassa, Msabaha katika barua hiyo kwa Katibu Mkuu alisema: “Nimempigia simu Mohamed Gire wa kampuni ya
Richmond juu ya upatikanaji wa hizo MW 40. Gire amekubali kuwa anaweza kutoa MW 40 za ziada ifikapo Septemba na kwa bei hiyo ya USD cents 4.99 @ kwh. Amesema hatahitaji majadiliano
mapya. Inatosha kama ataandikiwa barua tu ya nyongeza MW 40.”

Kwa mtiririko mzima wa kusakwa kwa Richmond, hakuna hata hatua moja ambayo Lowassa anaweza kudai hakuhusika katika mchakato
mzima, na kama vile Dk. Msabaha alikuwa anajua kitakachotokea wakati wote alionyesha kwamba
alikuwa akifanyia kazi maelekezo ya bosi wake, yaani Lowassa.

Kuna habari kwamba wakati Serikali itakapowasilisha ripoti ya utekelezaji wa maazimo ya Bunge juu ya Richmond, hoja ya kutaka
kusafishwa kwa Lowassa itaibuka ikilenga kuionyesha kwamba alionewa na Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza mchakato wa mkataba wa Richmond na Tanesco.

SOURCE: NIPASHE
Home
 
Hivi kweli ukawa mmekosa mtu mpaka mpokee mtu ambaye nyie wenyewe mlikuwa mstari Wa mbele kusema ni Fisadi Tena mkazunguka nchi nzima mnisema wananchi wasimchague...leo hii mnamuona msafi eti sababu mnaichukia ccm...hata mfanye nini Lowasa hawezi kumfikia magufuli kwa utendaji,kupendwa na wananchi na kwa sifa safi!!mnamshauri vibaya waziri mstaafu na kufanya zaidi kuwa na mawazo....mwambieni ukweli sio kwamba anachukiwa Ila kwa Sasa Tanzania inamhitaji DK.MAGUFULI....na kingine,je akikosa huo urais nyie ukawa mtaendelea kumuheshimu au mtamdharau?
 
Hamjafanya kosa lolote, sasa kwa nini kuwa na wasiwasi, Mzee kashasema anaingia pale IKULU kuwaletea watanzania maendeleo na si kwenda kulipiza visasi.

Kuweni na amani tu mioyoni mwenu.
 
Mbeke

Mkuu, Sijui unataka nini hasa....hebu wasiliana na Mh. Gunini...T na Mh. Mge....T ndhani watakutatulia tatizo lako mana ke unasumbuliwa na homa Ya KIJANI na NJANO......
 
Last edited by a moderator:
Mleta Mada Hi I Tuhuma Za Ufisadi Kwa Rsis Mtalajiwa Zilishadunda.Uongo Mtupu.Wataznia Hawadanganyiki Me a Mate Ulale.
 
Alishauliza swali wanaosema ninaenda kulipa kisasi je wamenikosea nini?mbona mnahanya hanya?subirini msema kweli ni sanduku la kura,hakuna mtu mwenye hati miliki ya hii nchi,ESCROW ESCROW,home shopping center
 
Yaaah..! hili gazeti la 2009 lilifanya utafiti wa kina..wadau someni kwa umakini..hili ni Nipashe..
 
Lengo kuu la watanzania kwa sasa ni kuiondoa CCM kwanza.Mengine yatajadiliwa baadaye.

WatanZania wapi hao unaowaongela? Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 CCM ilikubaliwa na WatanZania karibia asilima 80 (80%)! sasa sijui hao unaowaongeli ni wa wapi hao?
 
Lengo kuu la watanzania kwa sasa ni kuiondoa CCM kwanza.Mengine yatajadiliwa baadaye.

Umewahi kusikia usemi unaosema '' The past determines the future''..Lowassa anayo ''past'' na ni lazima hiyo ''past'' ita-determine ''future'' yake..atake asitake..hii ni kanuni ya maisha.
 
Yaaah..! hili gazeti la 2009 lilifanya utafiti wa kina..wadau someni kwa umakini..hili ni Nipashe..

Acha umbeya wewe ripoti ya Dr Mwakyembe haikusomwa yote unajua kilichokuwa ndani yake ni nini au unajitoa ufahamu kweli aliyewaloga bado yupo hai mumtafute.
 
mh MBONA lowasa mnamuogopa sana !mmeanza kutapatapa kama wafa maji. Na bado mtaibua mengi mwaka huu!
 
Mbeke

Mkuu tunakushukru kwa taarifa hii murua kabisa.Sisi watanzania tunajua kabisa mkataba wa richmond ulioingiwa na serikali ya ccm unatuumiza sana mpaka leo na inaweza kuwa ndiyo sababu ya umeme kuuzwa kwa bei ya juu na hivyo kutuongezea umasikini.Kitu ambacho hatujui mpaka sasa ni kwa nini serikali ya ccm imeshindwa kumkamata na kumfungulia mashitaka mtu aliyetusababishia hasara kubwa namna hii.Kigugumizi cha serikali ya ccm katika hili ni nini?Kutokana na kukosa majibu ya maswali haya tukafikia uamuzi kuwa-TATIZO LETU KAMA NCHI SI LOWASA ila ni CCM na MFUMO ilio ujenga.kwa hiyo tulichoamua kufanya kwa sasa NI KUNG'OA MZIZI CCM na hayo matawi yaani akina CHENGE sijui,Lowasa kama unavyotutapikia hapa na wengine yatakauka yenyewe.

USITUSUMBUE HAPA ULIPOFIKA WENZIO TUSHAPITA KITAMBO SANA
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom