Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Rais wa JMT, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Machi, 2017 amepokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2016.
Katika kukabidhi ripoti hiyo CAG ameshauri hatua zichukuliwe kukabiliana na mapungufu ikiwemo kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za umma katika Madini, kuiepusha TANESCO kununua umeme wa gharama kubwa, matumizi mabaya ya misamaha ya kodi na kuongeza mashine za kutoa risiti(EFD).
Rais amemuagiza CAG kufanya ukaguzi wa kina katika sekta ya madini na kubaini mianya yote ambayo inasababisha nchi kukosa mapato makubwa hususan misamaha ya kodi, mikataba na ulipaji wa kodi.
Pia rais ameamuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuitisha kikao cha pamoja kitakachomkutanisha CAG na Mawaziri wote, Makatibu Wakuu wa wizara zote, Gavana wa Benki Kuu na Wakuu wa taasisi za umma ili kila mmoja aambiwe hali ya hesabu katika taasisi yake na kuchukua hatua ili makosa yasijirudie.