IKULU: Rais Magufuli amuapisha balozi Mlowola na kupokea ripoti ya TAKUKURU

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,980
Karibu!

Up dates;
Balozi Valentino Mlowola anakula kiapo sasa mbele Rais Magufuli.
Na sasa anakula kiapo cha uadilifu mbele ya jaji Nsekela.

Ukumbi umesheheni viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu viongozi wa Idara na taasisi za serikali bila kusahau viongozi wa dini.

Wageni wakuu ni pamoja na Makamu wa Rais mama Samia, PM Kassim Majaliwa, Jaji mkuu Prof Juma na CS Kijazi.
Bado sijamuona Spika wala Naibu wake.

Sasa Mkurugenzi mkuu wa Takukuru nchini Diwani Athumani anawasilisha ripoti ya utekelezaji ya mwaka ya Takukuru

Diwani anamshukuru Rais Magufuli kwa namna anavyoisimamia vita dhidi ya Rushwa.
Sasa anaanza kuwasilisha ripoti ambayo ameigawanya katika sehemu ( vitabu) vinne!

Matangazo mubashara yamekatika!

Matangazo yamerudi lakini Diwani Athumani alishamaliza uwasilishaji wake sasa waziri Kabudi anatoa salamu zake na anamshukuru Rais Magufuli kwa kufungua ubalozi Havana Cuba ambako balozi Mlowola anaenda kuhudumu!

-------------

HOTUBA YA KAMISHNA MKUU TAKUKURU,DIWANI ATHUMAN

Kwa mwaka 2017/18 utekelezaji wa malengo ya TAKUKURU umefanikiwa kwa 87.4%. Kwa mwaka 2017/18 TAKUKURU imeokoa kiasi cha Tsh. Bilioni 70.3 kulinganisha na Tsh. Bilioni 14.6 zilizookolewa kwa mwaka 2016/17

TAKUKURU imeongeza kasi ya kufungua kesi ambapo imefungua kesi 495 kwa mwaka 2017/18 ikilinganishwa na kesi 435 kwa mwaka 2016/17. Aidha, Kurugenzi ya uchunguzi imechunguza na kukamilisha majalada 906 ambapo 699 kati yake yalihusu hongo

Kwa sasa tunacho Kitengo maalum kinachotafutilia na kutaifisha mali zilizopatikana kwa njia ya rushwa. Lengo ni kuwaondolewa Watuhumiwa tamaa ya kuiba fedha za umma kwani mali walizoiba ipo siku zitatifishwa na kurudishwa Serikalini

Kupitia Kitengo hicho kwa mwaka 2016 hadi 2018 Serikali imeokoa zaidi ya Bilioni 14.69, kutaifisha nyumba 7 na Magari 4. Tumeweka zuio la mali zikiwemo akaunti za benki zenye fedha zaidi ya Bilioni 20, Nyumba 26, Viwanja 47, magari 61 na mashamba 13

TAKUKURU inavyanzo vingi vya taarifa za rushwa ila vilivyozoeleka ni pamoja na Taarifa ya CAG, hoja zitolewazo Bungeni, taarifa za yombo vya habari. Pia, Wananchi kupitia mitandao ya kijamii, Wananchi kuwasilisha barua au kupiga simu au kufika ofisini


HOTUBA YA RAIS MAGUFULI

Hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu ulinieleza kuna mtu ameingiza magari zaidi ya 94 bila kulipa kodi. Lakini alikingiwa kifua kweli na watu wengi kweli, ila nakupongeza sana mmeanza vizuri

Sikukuchagua wewe Kamishna wa Polisi kuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU kwa bahati mbaya, ukishindwa kukamta mtu kwa sheria za TAKUKURU tumia za Polisi. Pia huyu ni Mtumishi wa TISS, najua mlikuwa hamjui ila haina shida kusema cheo chake kwa nafasi aliyonayo sasa

Sasa kwa vile wewe ni mtumishi wa TISS mtu wa TISS akifanya makosa pia mkamate. Pia, Msaidizi ni kuweka Mwanajeshi Bregedia Jenarali ili akila rushwa Mwanajeshi pia mnamkamata

Kwenye sherehe moja kule Airport nilizungumza kuwa ndege ya Serikali ipelekwe ATCL ili ibebe wananchi, siku viongozi tukitaka kupanda tunapanda hiyo. Wakanambia eti kuchorwa twiga na kupaka rangi za ATCL haiwezi kufanyika Tanzania, zikatafutwa nchi tatu

Sitaki kuzitaja nchi hizo, mimi nikasema tafuta watu hapa hapa Tanzania. Wakanyamaza wakadhani nitasahau. Nikaambiwa siku moja ndege inaondoka, eti Wameshalipa hiyo nchi 60% ya gharama nadhani gharama ni Milioni 200. Na wanaosindikiza walikuwa wamelipwa

:Wanaosindikiza ndege hiyo kupkwa rangi wapo hadi ‘Air hostesses’ eti waende kule kusubiri ndege ikipakwa rangi. Nikasema ndege ikiondoka na hao walioisindikiza wanaondoka. Haikuondoka na leo au kesho ndege inakamilia kupakwa rangi ikiwa imegharimu Milioni 5

Hongereni sana Kamishna Diwani na Bregedia Jenerali kwa kufanya kazi nzuri sana sana. Fedha mlizookoa zitatumika kununulia madawa au kupeleka watoto shule na shighuli nyingine za kijamii

Mnafanya vizuri, tumeona hata Watu wakubwa waliodhani hawawezi kushikwa wamefikishwa mahakamani. Tena rushwa za wakubwa ni mbaya zaidi, za wadogo unaweza mwambia rudisha wewe akarudisha akiogopa kwenda gerezani

TAKUKURU ni chombo kilichobaki kinachotisha, sasa mkakitumie vizuri katika kutenda haki. Katika uchunguzi mfanye vizuri, msionee mtu ili msije baadaye mkajibebea dhambi za bure. Katendeni haki

Gavana anajua watu walikuwa wanaenda kuchukua pesa BoT kwa ajili ya zile Bureau De Change lakini hawasemi kiasi gani wameuza. Wala hakuna uhusiano kwamba wamelipa kiasi gani au ripoti na walikuwa wanatumia Bureau moja kumuuzia mtu wao

Walikuwa wanamuuzia mtu wao kwa rate hata ya 1400 halafu wanchukua hiyo quotation kwamba exchange rate ya Tsh imepanda juu. Ile ni kusumbua uchumi wa nchi. Nikamwambia Gavana kafanye kazi huko, haikutokea tena kuzungumza kuwa exchange rate ni 2400

Nikimuuliza Gavana wewe kweli huna Dola huko, anasema ninazo nyingi mno. Fedha zipo hata za ziada zipo. Nchi inaweza kuishi hata zaidi ya miezi mitano bila kukusanya hela yoyote

Yote ni kwa sababu Bureau De Change zilikuwa zinafunguliwa kama uyoga na ndio zilikuwa vichochoro. Zinachukuliwa fedha zinakwenda nje! Mtu anapigiwa simu toka nchi fulani anasema mtu anakuja na dhahabu weka dhahabu huko, fedha tunaweka huku. Wizi wa ajabu

TAKUKURU si lazima kesi zote za kwenda mahakamani zipitie kwa DPP, kuna kifungu kwenye sheria zenu kinaruhusu kumpeleka mtu mahakamani moja kwa moja. Zile ambazo lazima kwa DPP sawa, na uzuri wewe una vifungu vingi tumia hata vya Polisi

Mimi nakupongeza Balozi Mlowola nenda kafanye kazi, usichelewe kuondoka eti unaaga aga. Nimeshaona hawa Mabalozi nikiwateua kila siku wapo kwenye ofisi wanakwenda kuaga

Nimemteua balozi wa Zambia, sifahamu kama ameshaondoka. Penyewe ni Zambia tu hapo kila siku anaaga. Anaaga mara kwa Waziri mkuu, mara sijui ofisi gani, sasa ataanga mpaka kwa Wakuu wa mikoa na akimaliza kuaga na ubalozi hakuna
 
One man show on all television channel...

Hakika watanzania walijikoroga kumpa hicho kiti...

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani jamaa kodi zetu anachofanya ni kumtajirisha Mengi ndio maana credibility ya ITV inashuka sana sasa maana wanafanya biashara na mtu asiyekubalika kwa jamii....

Jamaa ni dicteta mambo anayoyafanya ndio Putin alikuwa akiyafanya miaka ya nyuma hv baada ya kuingia madarakan ...

Ana kila sifa ya kuwa dicteta...
 
Yaani jamaa kodi zetu anachofanya ni kumtajirisha Mengi ndio maana credibility ya ITV inashuka sana sasa maana wanafanya biashara na mtu asiyekubalika kwa jamii....

Jamaa ni dicteta mambo anayoyafanya ndio Putin alikuwa akiyafanya miaka ya nyuma hv baada ya kuingia madarakan ...

Ana kila sifa ya kuwa dicteta...
Hahahahahah mtasema sana lakini watanzania asilimia 90 wapo nyuma ya Rais..nyinyi mko labda asilimia 10 au 5.. hamna impact yoyote. Bwabwajeni mkichoka mkakungute miguu mkojoe mlale
 
Achana na chaguo la Mungu wewwew jinga...watanzania waliomba kwa Mungu wapatiwe a tough guy. Na huyu ndie tuliyekuwa tukimwomba Mungu..acheni Mungu aitwe Mungu wajameni
Jina lako lina akisi kushindwa maana ni mnara ulio jengwa kumjaribu mungu na haukufanikiwa ila kwa komenti yako naiunga mkono isipokuwa usipende kumshirikisha mungu kwa kila kitu
Imeandikwa usilitaje jina la bwana wako bure


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom