Ikulu: Rais hajaidhinisha posho za wabunge!

Ikulu: Rais hajaidhinisha posho za wabunge!

Status
Not open for further replies.
Hii serikali sasa!!Rais anasema hili, Premier anazungumza opposite, Spiker yeye anasema na kutenda INVERSE na hao wote wawili. Nasikitika kusema Tanzania tunajiendesha tu wenyewe, HATUNA SERIKALI
 
Mi naona hapo wanacheza mchezo wa kuigiza, itakuwa ni kweli JK kesha saini siamini kama Pinda anaweza kuropoka kwa hilo na kuwaaminisha wabunge . Alternatively, inaweza kuwa ni mchezo kati ya Pinda na JK ila waone reaction ya wananchi wakati huo huo wakiwapoza wabunge! Lakini pia mi niko skeptical na authenticity ya hiyo taarifa ya Ikulu, ni ya kweli au Invisible ameitunga tu kwa sababu jinsi ilivyokuwa presented mtu yeyote anaweza kufanya hivyo!
 
Serikali inaendeshwa kishikaji, bora hata wasingekanusha!
 
KIKWETE AACHE UNAFIKI, YEYE NDIYE ALIYEMRUHUSU MIZENGO PINDA KUBARIKI ONGeZEKO LA POSHO, BASI KAMA HAKUBARIKI HIZO POSHO ATOE TAMKO LA KUZIFUTA. NA SIO KULALAMIKA.
 
Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi.

ati nini??
 
Inasikitisha sana kuona kwamba hata Rais wetu hana msimamo. Anapinga posho aseme wazi na ajenge mfumo mpya wa malipo kwa viongozi wa serikali na taasisi zake. Kwa nini anakuwa msanii ktk kila hoja muhimu kama hii kiasi kwamba wabunge wanajiamulia vitu wapendavyo kwa kuogopana.

Hakika alinishangaza sana ati alikubali kuweka saini muswada kwa kuhofia maamuzi yaliyokwisha pitishwa na bunge wana CCM wenzake hali yeye binafsi anakubaliana kimsingi na Upinzani. Hii inaonyesha wazi udhaifu wake na sitegemi lolote la maana maadam miaka 6 ya utawala wake umekuwa na vioja vingi kuliko utawala bora.
 
What's going on ??

Madam speaker, ZIMEBARIKIWA na zimeanza kutumika, JK and Pinda were around and none of them bothered to clear,clarify or vet the statement .........

Katibu wa bunge: hazijabarikiwa.........speaker makinda didn't comment further but PM brushed this off as a mere misunderstanding between people who should literally not contradict each other as they come from same office....this was an eye opener I dare say....


pm Pinda: ZIMEBARIKIWA Na rais ........

IKULU: hazijabarikiwa


NSIANDE: :A S embarassed::canada::biggrin:
 
Inawezekana Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imekuwa HACKED? Maana hawachelewi kuikana hii taarifa kesho!
 
Sababu za kutembea kifua mbele na kujiita Mtanzania mbele ya raia wa nchi nyingine zinazidi kuyeyuka siku hadi siku. Hii yote inaletwa na utendaji wa viongozi wetu tuliowachagua kuongoza serikali. Haiwezekani huyu aseme hivi yule vile
 
Kama hii taharifa ni ya ukweli basi Waziri Pinda apime kwa mapana na achukue hatua. Hii inatosha kumpa picha halisi ya mambo huko jikoni.
 
jamani huo ni usanii wa jk, anamwingiza pinda mjinii, huenda alimwambia posho atapitisha. Sasa pinda kaingia mkenge, si mnajua mabo ya richmond alimpa go ahead lowassa, mwisho wa siku akakaa pembeni jamaa akala sulubu ya bunge halafu akasema kapata ajali ya kisiasa!
 
nawasiwasi hi nchi tunapoelekea kwa kweli yaani Zito yuko informed zaidi ya Pinda waziri mkuu? poor jk nchi inamshinda hi amebaki kuongoza kwa matukio
 
sishangai kwa nini baadhi ya wanasiaasa kama kina DR N"GWANDU ,na wengine walisema kufanya kazi chini ya Kikwete ni bora kulima shambani......unafanyaje kazi na mtu ambaye siku zote anapenda kuwatega wenzake waingie shimoni ili yeye aonekane mzuri...

RAIS GANI HAJIAMINI.....??? ANAOGOPA SANA KUFANYA MAAMUZI..?? HUU UAMUZI WA POSHO NI YEYE ALIYEMPA RUHUSA WAZIRI MKUU PINDA KUWA ....ASAINI ONGEZEKO HILO......KUMBE ALIKUWA ANAPIMA MAJI ANAONA WATU WANALALAMIKA ...ANAKIMBILIA KUMRUKA ..

NI HUYO HUYO ALIMRUKA PINDA KWENYE SAKATA LA JAIRO........NA HATA KATIBU MKUU KIONGOZI AMBAYE KILA SIKU HURIPOTI KWA RAIS ....HATA OFISI ZAO ZIPO KARIBU..ALIPOMSAFISHA JAIRO ....ALIPOONA MALALAMIKO YA WATU AKAKIMBIA KUMKANA ..AKASEMA ALIKUWA HAJAPEWA TAARIFA ..ANGEKAATAA..!!

NI RAIS HUYU HUYU ...ALIYEMKATALIA LOWASSA KUVUNJA MKATABA WA DOWANS ..ALIPOONA MAMBO YANAHARIBIKA ..AKAMRUKA!!!!

MIMI NAONA TATIZO KUBWA LA NCHI SASA HATUNA RAIS AMBAYE ANA MSIMAMO WA KUTOSHA KUFANYA WAFUASI WAKE WAJIAMINI....RAIS ANAYEJIAMINI...YUPO TAYARI KWA MATOKEO YEYOTE YA MAAMUZI YANAYOTEKELEZWA NA WAFUASI WAKE AMBAYO AMEYABARIKI.....NA HATA MAMBO YAKIHARIBIKA HUWA TAYARI KUWATETEA ...HII ITAFANYA WAJIAMINI..

NAAMINI HILI LA MGOMO ...KAULI YA PINDA ILIKUWA NA BARAKA ZA RAIS ..LAKINI MAMBO YANAPOELEKEA KUHARIBIKA ATAMKANA....SASA WASAIDIZI WAKE WATAOMBA AWE ANAWAPA MAAGIZO KWA MAANDISHI AU WATAMREKODI.......

ITAFIKA MAHALI WATAMUACHIA KAZI!!
 
Wa bunge wa chadema walipo sema waziri mkuu ni muongo watu wakabisha sasa ikulu inamkana live
haya tusubiri kwenye kipindi cha majibu ya fasta bungeni
 
Taarifa hyo inaeleza Rais anaona umuhimu wa kuongeza maslahi ya wabunge, lakini amewataka watumie utu na wafikirie tena juu ya maombi yao na amewaagiza kutumia mkutano unaoendelea kufanya hivyo.
Source: Itv Habari ya saa 2 usiku leo.
 
Katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku kurugenzi ya habari yasema kuwa rais kikwete hajabariki posho za wabunge.hivi mtoto wa mkulima ni nani alimtuma kusema kuwa rais kabariki posho za wabunge.pole mtoto wa mkulíma umekuwa mbuzi wa kafara.bora tu urudi katavi ukafuge kuku.jamani hii iko vp?
 
Atoe kauli inayoeleweka, kauli thabit, KAULI ya kiume, mbona anababaika?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom