Ikulu, Mwambieni Rais mlioyaona jana na leo. Msifiche!!

Mzee Mapenzi

Senior Member
Jan 9, 2019
122
439
Ukiachana na wale wapiga zumari ambao kwao kila kitu ni sawa; jana na leo hata wao wameshindwa kuelewa wafanye nini. Wanaojitahidi kupiga zumari, mlio wake ni matusi na si hoja.

Ikulu ni taasisi kubwa. Inapima mengi yalioko nje ya kuta zao. Nawakumbusha tu, maoni ya wananchi jana na leo, kwenye vichwa mbalimbali vya habari ziliendelea Ikulu, kuna lugha moja tu iliozungumzwa!

Hakuna aliezungumza lugha tata, hakuna aliefunika kombe! Wote wamesema kauli moja tu "RAIS UNAFICHA UFISADI, RAIS HUPENDI ANAEONA MAOVU".

Wala msimwambie hizo ni kauli za wapinzani waliolipa vijana kuyasema hayo. Bali mwambieni hali halisi mliyoona. Na hiyo si ishara nzuri kwa taifa.

Msisingizie upinzani. Hakuna hela ya kuwalipa watu wote hao kuyasema hayo.

Mwambieni, Asad umemfanya awe ufunguo wa bongo za watanzania waliolala kwenye nyumba zenye vitasa vibovu, ambao mwanzo hawakuona kasoro ya vitasa walivyofungiwa.

Mwambieni ukweli.
 
Katika historia ya nchi hii, hakuna utawala ulio/unaoongoza kwa "UFISADI" kama huu. Utashika "REKODI KITAIFA" na haitakuja kuvunjwa milele.

Pia wamwambie haiwezekani mtu mmoja kuwazidi "AKILI NA MAARIFA" raia zaidi ya millioni 60. Ipo siku watapata "UHURU" wa kuongea na kuweka wazi madudu ya utawala huu (pindi utawala huu utakapo fikia mwisho wake).
 
Nimemsikiliza sana MtuPori, yaani yeye ni vijembe tuu utadhani Mange Kimambi?
We umesha mnyang'anya cheo MTU kisheria au kimakosa sii unyamaze basi! Vijembe vijembe wakikujibu unaanza kuwa mbogo! Sasa hivi tuna mfano mbaya sana juu ya hiki cheo kikuu.

Bahati mbaya wasaidizi wa Rais hawakumkumbusha kuwa CAG sio Accounting Officer wa ofisi ya ukaguzi ndio sababu akajikuta anamtupia Madongo kwa tabia ya baadhi ya wakaguzi kuomba posho ubalozini pia akamuelekeze CAG mpya akafanye reshuffle wakati sio majukumu yake

CAG sio Accounting officer
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa

CAG aache kutafuta huruma ya Wananchi yeye sio wa kwanza kushika hicho cheo,kila Mtanzania mwenye sifa alistahili kuwa CAG
 
Huna ulijualo wewe kuku wa maziwa! Usijifanye unazijua Sana Sheria za kazi ilihali hujui lolote! Je, aliomba kustaafu kwa hiyari? Kama hakuomba kwanini mlazimishe kustaafu ilihali umri wake kisheria inampa nafasi? Kisha unabwata tu kwa ajili ya buku saba! Aibu.
 
Kazi ya CAG ni mkataba wa miaka mitano

Miaka mitano imeisha kama unampenda sana mwajiri awe mkaguzi wa familia yako

Back
Top Bottom