Ikulu mpya ya Chamwino yaiva, kuzinduliwa Mei 2022

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa Ikulu mpya ya Chamwino uliofikia 91% ambayo itazinduliwa rasmi na kukabidhiwa kwa watanzania mwezi wa tano mwaka huu.

Ikulu ya Chamwino inaongoza kwa ukubwa wa eneo Duniani kote.
RIP Magufuli hata Chadema watafaidi siku moja wakishinda urais.

View attachment 2084978
"....itazinduliwa rasmi na kukabidhiwa kwa watanzania mwezi wa tano mwaka huu...." Hii sentensi inabeba maneno mazito sana ukiitafakari kwa kina.
 
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa Ikulu mpya ya Chamwino uliofikia 91% ambayo itazinduliwa rasmi na kukabidhiwa kwa watanzania mwezi wa tano mwaka huu.

Ikulu ya Chamwino inaongoza kwa ukubwa wa eneo Duniani kote.
RIP Magufuli hata Chadema watafaidi siku moja wakishinda urais.

View attachment 2084978
Awamu ya Sita ina tatizo kwenye kukamilisha miradi. Kuanzia hapo asilimia 91 inaweza kuchukua miaka miwili kufikia asilimia 100.

Mfano ni ile stendi ya Magufuli - Mbezi juu na SGR.
 
Raisi naye ahamie Dodoma, Dar watuachie wenye pesa zetu tuendelee kupiga na kula raha
 
Haitaongeza chochote kwenye uchumi wa nchi au wa mwananchi. Ni fahari ya macho na matumizi mabaya ya pesa ya umma. Hakukuwa na haja kabisa ya msururu mkubwa wa majengo kama ilivyofanyika.

Rais hata kama angezaa kama simbilisi, nina uhakika hatahitaji hata 20% ya hayo majengo.
Omba uwe rais utaujua utamu wake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom