Hawawezi kuthubutu kuujibu kwani utamweka rehani Bosi wake JK, kumbuka Tundu Lissu aliongea nini wakati wa issue ya escrow ikijadiliwa bungeni juu ya mkataba wa IPTL, JK ana scandal nyingi kuhusiana na mikataba ya umeme kwa vile yeye wakati mikataba hiyo inasainiwa katika vipindi tofauti alikuwa Waziri wa Nishati na Madini kisha Waziri wa Fedha na Escrow amekuja kuitetea akiwa rais. Jamaa anajua sana kuwabambikia mizigo wenzake kumbe yeye ndiye mhusika mkuu. Nakumbuka wakati vyombo vya habari vikianza kudodosa issue ya Richmond kuna wakati JK alikuwa akitoa ufafanuzi sana juu ya kinachoendelea hadi gazeti moja liliandika kichwa cha habari kifutacho nanukuu ' HIVI KIKWETE AMEKUWA MSEMAJI WA RICHMOND'? Mwanzoni mwa issue ya Richmond jamaa alikuwa anaitetea ile mbaya.