Ikulu mbona hamjibu tuhuma hii?

Ikulu mbona hamjibu tuhuma hii?

Hawawezi kujinu wakati ni ukweli..... Lowassa kashasema wakijubu tu anamwaga data
 
Natamani sana wajibu ili pachimbike...ila sidhani kama watajibu watakaa tu kimya na kuja na mkakati mwingine wa kubadilisha upepo...maccm yanajua udhaifu wa watanzania na wanajua sana kucheza na akili za watanzania....kinachotakiwa hapa ni ukawa kujipanga kukabiliana na lolote...hata kama ni kumleta aliyesemekana amekufa na wamlete tu...tunachotaka ni maccm yatoke madarakani kwanza mengine tutayaweka sawa baadae kidogo...
 
Ikuru twambieni Richmond mlivuna ngapi?lowasa ameishasema
 
Mkuu mbona sijaona cha maana cha kujibu kwenye hili andiko lako jepesi na halina maana.
 
Lowasa akimleta Balali pia Ikuru hamtajibu upepo utapita tu
 
Balali akiletwa Ikulu mtakaa kimya?Upepo utapita tu
 
Imekuwa kawaida ya wasemaji wa ikulu kujibu haraka haraka tuhuma zinazotolewa juu ya watumishi wa ikulu hasa rais kikwete.
Majuzi tumemsikia EL akidai kuwa mamlaka ya juu yake (rais) indiyo iliidhinisha mkataba wa richmond kusainiwa licha ya kutiliwa shaka na wataalam. Swali ni kitu gani kinamzuia salva na wenzake kuliongelea hili (kukanusha) kama ilivyo kawaida yao? Tafakari!

Kwani Vasco dagama Wa bagamoyo yupo?
 
Vasco dagama yuko safarini kuelekea Tanga hajafika ofisini mwezi wa nne sasa

Anakula bata za mwisho Ila rai yangu ipo siku bata zake atazilipa km sio yy jamii yake

Nothing goes for free
 
Ikulu haina muda wa kupoteza kujibizana na Lowasa,nyie mmeshamchukua endeleeni nae na kila anachosema mnasikiliza,pesa ni sabuni ya roho acha kabisa
 
nimeona kwenye gazeti la raia mwema kuwa Kikwete atahojiwa. nayasubiri kwa hamu sana hayo mahojiano, nadhani ni kesho au j'tano kama sikosei.
 
Imekuwa kawaida ya wasemaji wa ikulu kujibu haraka haraka tuhuma zinazotolewa juu ya watumishi wa ikulu hasa rais kikwete.
Majuzi tumemsikia EL akidai kuwa mamlaka ya juu yake (rais) indiyo iliidhinisha mkataba wa richmond kusainiwa licha ya kutiliwa shaka na wataalam. Swali ni kitu gani kinamzuia salva na wenzake kuliongelea hili (kukanusha) kama ilivyo kawaida yao? Tafakari!

Hawawezi kuthubutu kuujibu kwani utamweka rehani Bosi wake JK, kumbuka Tundu Lissu aliongea nini wakati wa issue ya escrow ikijadiliwa bungeni juu ya mkataba wa IPTL, JK ana scandal nyingi kuhusiana na mikataba ya umeme kwa vile yeye wakati mikataba hiyo inasainiwa katika vipindi tofauti alikuwa Waziri wa Nishati na Madini kisha Waziri wa Fedha na Escrow amekuja kuitetea akiwa rais. Jamaa anajua sana kuwabambikia mizigo wenzake kumbe yeye ndiye mhusika mkuu. Nakumbuka wakati vyombo vya habari vikianza kudodosa issue ya Richmond kuna wakati JK alikuwa akitoa ufafanuzi sana juu ya kinachoendelea hadi gazeti moja liliandika kichwa cha habari kifutacho nanukuu ' HIVI KIKWETE AMEKUWA MSEMAJI WA RICHMOND'? Mwanzoni mwa issue ya Richmond jamaa alikuwa anaitetea ile mbaya.
 
Back
Top Bottom