Ikulu kuna nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu kuna nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msharika, Jun 20, 2010.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jamani wapendwa wana JF wenzangu, Nimedata? within one month 3 cars within predent's office related to him straight have been involved in scandals of tyres and dirty fuel. Who is iresponsible to that? who has to be punished? How is president supposed to react to this for his security?

  Ikulu yakanusha Rais kupata ajali

  20th June 2010


  Ikulu imekanusha na kufafanua juu ya taarifa iliyotolewa na gazeti moja la kila siku (sio Nipashe) lililoripoti kuwa Rais Jakaya Kikwete amenusurika katika ajali baada ya gari lake kupasuka tairi wakati msafara wake ukipita hifadhi ya Katavi.

  Taarifa iliyotolewa na Mwandishi wa habari msaidizi wa Rais, Premi Kibanga, ilisema taarifa hizo si za kweli na kufafanua kuwa wakati msafara wa Rais ukipita katika hifadhi ya Katavi kutoka Namanyere kwenda Sumbawanga, jiwe lilinasa kwenye rim ya gari na kuanza kusababisha sauti isiyo ya kawaida hali iliyolazimu dereva wa gari ya Rais kusimama na kumhamisha Rais kwenye gari ya ziada ambayo siku zote huwa kwenye msafara kwa ajili ya dharura.

  Alisema baada ya hatua hiyo msafara uliendelea na mafundi wa Ikulu walibaki nyuma kushughulikia hitilafu ambayo iligundulika kuwa kwenye tairi ya nyuma upande wa kushoto ili kutoa jiwe lililonasa kwenye rim na kusababisha mlio usio wa kawaida.

  Kibanga alisema wakati shughuli hiyo ikiendelea walifika maofisa wa Polisi kutoka Mpanda ili kulinda gari la Rais na walikuta mafundi wakiwa katika shughuli ya kurudishia tairi ambayo ilitolewa kwa ajili ya kutoa jiwe kwenye rim na wala haikuwa pancha kama ilivyoelezwa kwenye taarifa hiyo.

  "Napenda kusisitiza kuwa katika hali hiyo hakukuwa na hatari yoyote ya kuweza kuelezewa kuwa Rais amenusurika ajali. Hiyo ni dua mbaya kwa mtu yeyote usiyemtakia au kumtakia mema kwa hali yoyote ile na wala si ustaarabu na heshima kwa kiongozi wako mkuu wa nchi.

  Sio kila tukio lolote la kupata pancha au kupata hitilafu ya gari linaweza kuelezewa katika hali kama ilivyoelezewa katika taarifa hiyo ya gazeti la Mtanzania hadi kuleta taharuki na kujengea watu na jamii nzima hofu isiyo na msingi," alisema. Alisisitiza umuhimu wa waandishi wote kupata taarifa za ufafanuzi na za udhibitisho kutoka kwa watu walio na mamlaka ya kufanya kazi hiyo na wala sio kutoka kwa mtu yeyote aliyeyoko serikalini ama Ikulu.

  Alisema ni wajibu wa mwandishi wa habari yeyote aliye makini kupata ufafanuzi wa taarifa zozote alizonazo. "Nasikitika kwamba hakuna mwandishi yeyote aliyenitafuta ili nimpe ufafanuzi wa jambo hili, kwa sababu mimi ndiye niliyekupo kwenye msafara wa Rais.

  Hili ndiyo jukumu kubwa na la msingi kwa mwandishi au chombo chochote cha habari ili kuondoa mkanganyiko wa maelezo ama taarifa ya matukio muhimu mahali popote."


  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. kussy

  kussy JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2010
  Joined: Jun 15, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  this is serious! but msafara wa rais huwa unakimbia mno, tuombe lisije likatokea baya lolote, msafara wa rais unatakiwa UPUNGUZE MWENDO
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wewe Premi Kbanga..usitufanye sisi hatujui magari...jiwe ninanasaje kwenye rim ya gari lenye tairi moja moja nyuma?ingekuwa double tyres ningeelewa...
   
 4. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2010
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,586
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Sitaki kusema kuwa msemaji wa ikulu ni muongo ila naomba tuangalie ukweli huu halafu tuamue.

  1. Ni kweli kuwa mawe yanakwama kati ya tairi za gari na kusababisha kelele zisizoza kawaida.
  2. Nijuavyo mimi magari ya msafara wa rais ni single tyres.
  3. katika gairi ya double tyres kama lori mara nyingi ikitokea kukwama jiwe huwa linagongwa na nyundo na kutoka.
  Sasa tuambiwee kukwama katika tairi hilo jiwe lilikwamia wapi.Tuone habarika kina kuondoa mashaka.
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mwenzake wa malawi mpaka alihama ikulu maana ilikuwa ina mauza uza kila siku....ye anang'ang'ania tu
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  well said
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hawa jamaa wanakanusha kila kitu...Sasa wakikubali kuwa msafara ulikwama kutokana na hitilafu ya gari kutakuwa na shida gani, si cha maana waeleze kitu cha ukweli?...Siasa hadi kwenye mambo ya kiufundi namna hii?..bahati mbaya ufundi huu hata vijana wanaojipaka oil magerejini kwa makusudi wanajua kwamba jiwe haliwezi kunasa kwenye single tyre!
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Ukiona explanation inazaa maswali mengi kuliko majibu una kila sababu ya ku suspect cover up.

  Halafu huyu msemaji/ muandishi wa rais ama hajui au anajifanya hajui swala zima la freedom of speech na uhuru wa waandishi kupata habari zao kutoka sehemu tofauti.Naelewa kwamba waandishi wetu ni muhimu wapate habari za upande wa wasemaji rasmi na kama hawakufanya hata jitihada za kupata upande huu hili si zuri (chances are wamejaribu na kuwa frustrated au hata wangejaribu wangekuwa frustrated, but still this is not an excuse). Lakini kusema waandishi wapate habari kutoka vyanzo rasmi tu ni kutoelewa concept nzima ya uhuru wa habari. Huwezi kuniambia mimi muandishi wa habari niko Mpanda, nakuta mafundi wanabadili tairi gari la rais, eti nisiwaulize habari mafundi, nianze kumtafuta msemaji wa rais, hata huyo msemaji wa rais atapata a technical breakdown kutoka kwa mafundi.

  Halafu kuna utamaduni katika wasemaji wa serikali kuwa na cover up, ku minimize effects za tragedies etc, ndiyo maana ukisoma magazeti yanayoelewa biashara ya habari utakuta kama information imetoka kwa a government mouthpiece wanakuwekea hiyo fact kama caveat, kama unajua kusoma between the lines uweze, utakuta watu wanakwambia "the government owned daily said...kwa nini wasiseme "the newspaper said..." wanajua kwamba information zinazotoka serikalini mara nyingi ni suspect, especially kwa nchi kama Tanzania ambapo watu wa Ikulu wanafanya coverup kuhusu magari bila hata ya kujua kwamba cover up ina holes, gari ya tairi moja haiwezi kupata hilo tatizo kwa mujibu wa wanaojuwa mambo haya.


  Si mtuambie tu kuna watu hawampendi rais mpaka Ikulu wanamfanyia hujuma? Mara wamuwekee mafuta mabaya, mara tairi etc.

  Ian Fleming alisema, once is happenstance, twice could be coincidence, but thrice is definitely by design.

  This is the third time this is happenning, with three points you can even draw a perfect circle, nothing less than definite design.
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hii niliyo bold imenichekesha sana ..dahh ngoja niende zangu bar kuangalia mpira mie haya mambo ya JK na watu wake yanaweza kukuvunja mbavu kwa kucheka..nakumbuka alipoaanguka Mwanza daktari wake akatoa taarifa eti rais hana ukimwi.....
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,912
  Trophy Points: 280
  Anatakiwa ajenge mazingira mazuri ya kidemokrasia nchini na ndani ya chama chake kwasababu mambo yameshabadilika...hata mwalimu naye alikuwa kwenye misuko suko mithili ya hii hivyo ulinzi wake na yeye mwenyewe alikuwa very cautios,na kipindi hicho ilikuwa wakati wa chama kimoja...Sasa yeye hajiulizi?

  Kwanza hata wakati wa mwalimu kulikuwa na mafisadi na ufisadi ulikuwepo,lakini siri hazikufichuliwa kama ilivyo sasa kwasababu kulikuwa hakuna sababu za kisiasa kufanya hivyo,na pia zilikuwa ni siri za Taifa na kuzifichua ni kama uhaini...wakati huu kuna kila sababu za kisiasa za kufanya hivyo lakini mazingira hayaruhusu,bado mazingira ni kama ya chama kimoja kwa kiasi kikubwa na asipobadilisha mazingira lazima atakuwa hatarini zaidi....Na kama hataki kubadili mazingira basi ajiuzulu wengine wafanye hivyo,kipindi hiki si kama zamani....Mwalimu alianza lakini wengine badala ya kuendeleza kadri muda unavyozidi kwenda,wao wanarudi kinyume nyume na kufanya yale ambayo hata mwalimu mwenyewe hakuthubutu kuyafanya....Haya yanayomtokea sidhani kama ni mambo ya kawaida,kuna unrest ya hali ya juu ndani kwa ndani,na kama hawezi kufanya mabadiliko ya kweli ni bora ajing'atukie zake tu kama mwalimu ambaye aliruhusu vyma vingi kimachale machale na kuruhusu vyama vingi licha ya kutokutaka kufanya hivyo under his watch, kuliko kuendesha nchi kwenye mazingira kama haya ambapo wengi tunaona kama nchi imeshauzwa na wao hata hawajali....Pia asiwazuie wenzake kugombea eti ili amalize awamu ya pili,isue si mtu kumaliza awamu,issue hapa ni unawafanyia nini wananchi na unalifanyia nini Taifa?!

  Waliyoyafanya mtandao mwaka 2005,hawawezi kuyafanya this 2010 halafu eti nchi ikaendelea kuwa na amani,asome alama za nyakati na abadilike accordingly,akicheza smart card atafanya hivyo,wananchi wana taarifa zaidi nyakati hizi kuhusu ufisadi na wanataka mabadilko lakini mazingira hayaruhusu,kama kuna wanamtandao ndani ya chama,basi pia kuna wazalendo ambao nao hivi majuzi tu wamenyimwa haki yao kuhusiana na ccj?!badilika Mh Rais acha kubandika pamba masikioni,mengi mabaya yenye mtiririko kama huu tumeona yanatokea...akiwa king'ang'anizi mi simo.
   
 11. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :embarrassed:
   
 12. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  It's not easy kuwa msemaji wa Raisi JK right now.!!
   
 13. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,797
  Likes Received: 20,754
  Trophy Points: 280
  wandugu,JIWE LINAWEZA KUNASA KWENYE GARI YA SINGLE TYRE.ishawahi kunitokea na ilibidi niende kwa fundi ndio nikajua ni jiwe.lilikuwa linasababisha very deafening screaching noise.
  Jiwe linaweza kunasa katikati ya BREAK DISC na METAL COVER ya break disc, ambayo iko on the inside of the break disc.
  Ukiangalia mpangilio ni tairi nje,inafuata break disc,then cover ya disc iko upande wa ndani wa disc SIO ULE WENYE STUD ZA KUSHIKILIA TAIRI.
  Natumaini nimeeleweka.
  NB:jiwe lenyewe ni size ndogo(kokoto).
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,912
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo ndugu Mbeba maboksi unatuambia kuwa wasemaji wamekosea kutaja rims na badala yake wangetaja "Break disk na metal cover?"
  Yani wangesema jiwe limenasa kwenye break disk and not the rim.....Is that what you're implying?
  Kuhusu huo mpangilio wa tairi bado sijauelewa moja kwa moja,ntashukuru kwa ufafanuzi zaidi.
   
 15. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #15
  Jun 20, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,797
  Likes Received: 20,754
  Trophy Points: 280
  Nilichojaribu kuonyesha ni POSSIBILITY YA JIWE KUNASA KWENYE SINGLE TYRE.kuhusu kilichotokea kwa gari ya MH.RAIS NO COMMENT.
  Mpangilio huo nina maana ukiangalia tairi ya gari.....nje kabisa ni tairi lenyewe,then inafuata break disc(ambayo imeunganishwa na chuma kinachoshikilia tairi)....upande wa ndani wa disc ndio una metal cover
   
 16. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #16
  Jun 20, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kigogo unasemaje?? say it again!!! mwenzetu una redio na television binafsi? Mbona sisi hatukusikia hilo la UKIMWI??
   
 17. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,912
  Trophy Points: 280
  Ok mkuu,shukran kwa maelezo yako,ni wazi wanachosema hao watu wa ikulu si kweli unless tuna uhakika kwamba jiwe lilinasa kwenye brake disc na si kwenye rim....Na kama tukipata taarifa zaidi zenye kuonyesha aina ya tairi ya gari hilo la Rais,basi tunaweza ku analyze more kwasababu naona hoja yako imejijenga zaidi kwenye two tyres vs single tyre na si rim vs brake disc....Tusubiri more info kama zipo...Otherwise hakuna "ukawaida" kwenye issue hii.
  Hata hivyo uko right na wao wangeweza kuwa right kama wangesema jiwe hilo ama kokoto,lilinasa kwenye brake pads na si kwenye rim....Kuna mjadala kama huu uko kwenye forum ya Toyota Tacoma....Na kuna mchangiaji alisema haya.....
  Mjadala huo uko hapa.....http://www.tacomaworld.com/forum/2nd-gen-tacomas/70000-can-stone-something-get-lodged-between-disc-pad-funny-noise.html

  Hivyo kuna uwezekano wa jiwe kunasa btn a disc and a brake pad,how does that constitute to a rim is beyond ma imagination.
   
 18. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,797
  Likes Received: 20,754
  Trophy Points: 280
  mkuu,kwani huyo aliesema jiwe limenasa alisema ni btn rim na nini??au alisema jiwe lilinasa kwenye tairi ila watu hapa ndio wanarukia kuwa haiwezekani just bcoz wamezoea jiwe kunasa kwenye double wheeled trucks/buses.msibishe vitu kwa sababu hamjawahi kuona au kusikia.
  IT IS POSSIBLE JIWE KUNASA KWENYE GARI YA TAIRI MOJA.
   
 19. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,797
  Likes Received: 20,754
  Trophy Points: 280
  jiwe kunasa btn brake disc na pads sijasema,narudia nilichosema it is possible jiwe kunasa kwa single wheeled car.hio inatokea btn brake disc na metal cover(kaangalie gari yako kama ina disc brakes).hio forum uliyoangalia ni ya madereva kama mwingine yeyote sio wataalamu hivyo hamna jipya hapo.na jiwe kunasa kwenye rim siwezi kukanusha au kukubali mpaka nijue ni gari gani,ina rims inch ngapi,tairi yake ni 250-60-zr20 or what,ni original rims or pimped.so msijjaji kwa experience za magari yenu au kwasababu hamjasikia au haijawatokea.
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,912
  Trophy Points: 280
  Unaniambia mimi "msibishe" na nimekuwekea link after research hapa kwamba it is possible?Hao wasemaji wa ikulu wamesema jiwe lilinasa kwenye rim na wewe ni msemaji wa nani unayedai lilinasa kwenye brake disc?Ama unanunua kesi?

  Watu wanaodai kuhusu tairi mbili vs moja ni hao ambao hawakusikia mambo ya uwezekano wa kunasa btn brake pad and disc,wao wameambiwa ni kwenye rims na ndio nimewawekea hiyo link hapo juu kuonyesha uwezekano huo,otherwise acha kuchachawa,hao wasemaji wa ikulu ndo wenye kuhitaji kurekebisha statement yao ya "kunasa kwenye rim" ama unataka kusema brake pad na disc navyo ni rims?
  Swali la "Huyo aliyesema" si la kuelekezwa kwangu,kama hufuatilii si kosa langu,na pia waliodai kuwa single tire nayo haiwezi kutokewa na mambo kama haya wako right based on this statement.....


  Sasa kujishebedua kutamsaidia nani?
   
Loading...