Iko wapi haki ya wana-udom | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Iko wapi haki ya wana-udom

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by buhange, Nov 29, 2011.

 1. buhange

  buhange JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 494
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Habari wana-JF

  Kwa kumbukumbu za haraka haraka ni kwamba pesa
  ( LOAN) zinazotowa na serikali kupitia HESLB kwa wanavyuo vya elimu ya juu ni kwa masharti ya kurudishwa baadae na wahusika(wanavyuo)

  Sasa utaratibu mpya ulioanzishwa na bodi wa kuvipa-mandate Vyuo husika kuweka pesa kwa wanafunzi imeongeza uvivu,uzembe na hata ubadhirifu ktk Loan offices kwa baadhi ya Vyuo. Mathalani, Continuing students ktk vyuo vingi vikiwemo UD na UDOM wamekuwa wakilalamika kutopewa Mikopo yao mpaka leo tangu vyuo vimefunguliwa, wakiuliza sehemu husika(Loan office) utasikia Una-Incomplete mara Matokeo ya kozi yako tulichelewa kuyatuma bodi ya mikopo na wakikuhurumia sana watakwambia swala lako lipo ktk mchakato.

  Hali ni tofauti zaidi ktk chuo kikuu cha Dodoma, maana kwa taarifa tuu ni kwamba baadhi ya wanafunzi ktk kozi kadhaa hawana hata matumaini ya kupata hizo pesa zao ktk SEMESTER hii. Vijana wanaishi ktk maisha ya kutisha na kusikitisha kama siyo kukatisha tamaa kabisa.

  UDOM swala la BATCH ndilo lilotawala, utasikia vijana hawa wakifarijiana kwa maneno kama "JINA LANGU LIPO BATCH YA 14, LABDA ITATOKA WIKI IJAYO". Utakuta kijana huyu anazungumza maneno haya akiwa hana hata uhakika wa kupata kipande cha mkate ktk siku husika. Inatisha sana ndugu wana-JF

  Sasa, hata hizo BATCH zitolewapo na wanafunzi wenye bahati ya mtende kupata fursa ya kusaini kwa ajili ya kuhakiki akaunti zao, hali huwa tofauti ktk kuwekewa hizo pesa. Mathalani, UNAWEZA KUSAINI LEO TAR.29/11 ILA UKAKAA WIKI TATU BILA PESA KUINGIA KTK AKAUNTI YAKO, Sasa Management na Loan Office UDOM wapo kwa ajili ya nini, bila ya hawa wanafunzi wanaowanyanyasa Leo hii kwa majibu ya kukatisha tamaa wao Wafanyakazi wangekuwepo kwenye hizo Office wanazolingia na viti vya kuzunguka? HUU NI UPUMBAVU NA UDHARIMU MKUBWA SANA

  SOCIAL SCIENCE ni mfano wa wahanga wa swala hili, takribani 51% ya wanafunzi wa SOCIAL SCIENCE hawajapewa pesa zao, Sasa hawa watu

  1.Wanakula na kunywa nini?
  2.Wanaandika na kusoma kwa kutumia nini?
  3. Kuna mwanafunzi kuelewa kipindi akiwa hana uhakika wa kula baada ya kipindi?
  4.Taifa linaandaa wasomi wa aina gani au wanaandaa MAKOMANDOO, MA-MAFIA NA WAZAMIAJI?

  Naomba Umma uelewe wazi kwamba ktk hali kama hii MIGOMO, FUJO NA HATA MAANDAMANO itabaki kuwa suruhu yetu ktk kutatua matatizo yetu, mpaka hapo Serikali watakapo elewa nini hasa tunamaanisha.

  POSHO ZA WABUNGE HAZITOLEWI KWA BATCH WALA HAZICHELEWESHWI, MAFUTA YA (SU) NA (DFP) ZA SERIKALI HAYAKOSEKANI ILA MIKOPO YA WANAFUNZI TUU... HAIWEZEKANI.
   
 2. s

  semako Senior Member

  #2
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda Mahumu ndo sababu
   
 3. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  ndio msome kwa bidii hata mie nimepita huko huko hadi leo hii, tulilala njaa siku nyingine ila leo twakula kuku na heniken baada ya kusota chuo , hivyo nashauri vijana msome na muwe wazalendo acheni kupenda starehe za mapema bila kufanya kazi
   
 4. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  He! ulichelewa wapi kuwa mbunge?mbona wapo hata wa STD 7tu!
   
 5. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2011
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Khah! Kula ni starehe au ni basic need? PhD hapo umechemka
   
 6. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Nyie Wanafiki kweli nyie,wacha mpate jeuri yenu...nyie si ndo mlimchangia JK mamilioni ya kuchukua form za kugombea Urais?wacha mle majani
   
 7. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  kujikwaa sio kuanguaka,wanajutia kosa lao sa hzi.
   
 8. dwight

  dwight JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wenzao tulipogoma,hadi vyuo vikafungwa kwa miezi kadhaa walitucheka wakadai eti wao watapendwa ktk soko la ajira,mara kwa mara ungesikia mara JK,sijui Pinda kaenda UDOM.
   
 9. nziriye

  nziriye JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 960
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  that is Udom bwana Chuo cha wenye njiiiii
  :lol:
   
 10. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Af hii issue mbona huwa MNAIPOTOSHA sana?! Mnataka kuniambia chuo chote ni wana CCM?! Mi Nime GRADUATE hapo UDOM na si MWANACHAMA wa CCM, kipindi kile sikusikia watu wanapita kuomba michango kwa ajili ya kumchangia JK..Wale inawezekana walikuwa WANACHAMA wa CCM pale UDOM ndo WALIOCHANGIA ila si wana UDOM wote...Naomba nieleweke MSIPENDE KUPOTOSHA UMMA...
   
 11. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  naijua Udom zaidi ya unavoijua..sipotoshi kijana..nasema nachokijua,ku graduate udom haimanishi unaijua sana...chuo cha kata kile kwa ajil ya degree za vodafasta,mtaishia kukichangia chama tu.
   
 12. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtaishia hivyohivyo.. Af ni dhambi kuichangia CCM!? Kwani ni lazima Kila mtu awe UPINZANI!?..Ok ni cha kata na vodafasta,.ila cha ajabu tupo makazini...mi nimesema ninachokijua na we unasema ulichokisia au kusimuliwa,..na kwa bahati mbaya nilikuwa waziri pale so kila kilichokuwa kinaendelea nakijua..Sijui hao waliomaliza vyuo vya taifa wanapata issue gani xtra zaidi ya Udom..hivi na wakimaliza chuo huwa wanaajiriwa moja kwa moja et??? Ili niwashauri wanasoma UDOM waache waanze kwny VYUO vyenu hivyo vya maana ili wasije HANGAIKA kupata KAZI?!
   
 13. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Inategemea na kaz uliyo nayo!hunidanganyi kuhusu Udoso...nimefanya research ya kutosha..na nlikuwa natazama mchango wa serikali za wanafunz ktk kuzuia migomo ya elimu ya Juu Tz..nimepta zaid ya vyuo 15 Tz nzima..na hicho chako cha kata kikiwemo...nkapata Dodoso za uongozi kuanzia Mtu anaitwa Malimi,Maratho,Singo mpaka takataka nyngne na serikali zao,ni aina ya viranja s rais wala mawaziri...ata HP wangu pale Kibaha Secondary amewashnda....hakuna kitu pale..tena unajiaibisha kusema umekuwa kama kiranja ktk chuo cha kata...kwa product ya Udom Taifa linaenda kuwa na wasomi hafifu
   
 14. dwight

  dwight JF-Expert Member

  #14
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Anaesema UDOM ni chuo kikuu ajitazame mara mbilimbili,twafahamu ni chuo cha majaribio sawa na shule za kata.
  Kuna tofauti kubwa kati ya wahitimu Udom na vyuo vingine katika mambo mengi km mtazamo,uelewa,umahiri ktk kazi nk.
   
 15. K

  KWETU PAZURI Senior Member

  #15
  Dec 4, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 161
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  u must be related 2 David Cameron
   
 16. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #16
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Narudia tena mtaishia hivyohivyo?! Kumbe unaiponda UDOSO kisa ya hicho ki-research chako kwa nini walikuwa wanashindwa kuzuia MIGOMO?! We ulikuja kufanya research mi nilikuwa kwenye system..nina doubt ka ulienda kufanya reseach ila ulienda kutembelea washkj.Hao wakn Ambrose na Singo walikuwa ni Marais wa collage ya Social Sciences na sio UDOM.. Af soma post yangu vizuri, nilichosema mi nimegraduate pale na nilikuwa Waziri, So vitu vingi nilivyokuwa vinaendelea navijua..Ningekuona wa maana ka ungekuja na sababu kwa nini elimu ya pale mbovu..
  1.Kwa nini wazuie migomo ka watu wanasababu za kugoma!?
  2. Kuhusu products za UDOM kuwa hafifu, huwezi kutoa conclusion kwa chuo ambacho kimetoa products mara mbili na product moja tu ndo ipo kwenye soko la ajira
  3. Kwa bahati mbaya sijasikia muajiriwa toka UDOM amekuwa fired kisa kashindwa kafanya kazi...
  4. Nyie mliotoka kwenye vyuo vya maana mmefanya issue gani kwa taifa hadi leo hii
  5. Graduates wa hivyo vyuo vyenu vya taifa mbona wapo wa kutosha huko mitaani imekuwaje hawana kazi hadi leo?!
  6. Unataka kuniambia Marketing, Accounting au Sociology jinsi inavyofundishwa UDSM, MU. SUA ni tofauti na UDOM?!
  NB:- Swala la uwezo wa kufikiri ka unavyodai hausababishwi na chuo bali ni juhudi za mtu binafsi na misingi aliojengewa toka mwanzo, manaake hamna sehemu inayofundisha mtu jinsi ya kufikiri,.KWANI HUYU RAIS WENU KASOMA CHUO GANI!? Si regret kwa kusoma pale but naji proud sababu nilichokitalajia nimekipata tena +ve
   
 17. K

  KWETU PAZURI Senior Member

  #17
  Dec 4, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 161
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  asante kwa kumjibu huyu kenge
   
 18. Engager

  Engager JF-Expert Member

  #18
  Dec 5, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  ukilinganisha mawazo haya na ya huyo anayejiita sijui ngaliba dume, oviously utagundua ngaliba ni mropokaji (speaks without facts) halafu naye anajihesabu anauwezo mkubwa wa kufikiri, kaaz kwelikwel....lol.
   
 19. buhange

  buhange JF-Expert Member

  #19
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 494
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  NGALIBA JIKE! lenye MADUME 20.Mmmmh! pole sana kaka.
  ila siwezi kukulaumu sana maana kila mtu anahaki ya kutoa maoni, inamaana uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo ktk kuponda hii jamii ya wana UDOM? Kweli nchi hii bado inamzigo mkubwa wa kuelimisha UMMA wake! sikutalajia kama watu kama wewe waweza kufikia hatua ya KU-COMMENT vitu bila hata kushirikisha BRAIN zao, Pole sana ndugu. Mmmmmh! endelea kutoa pumba zako. maana it seems kama uko half way minded... go on...
   
 20. buhange

  buhange JF-Expert Member

  #20
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 494
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Mmmmh! pole sana kaka.
  ila siwezi kukulaumu sana maana kila mtu anahaki ya kutoa maoni, inamaana uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo? Kweli nchi hii bado inamzigo mkubwa wa kuelimisha UMMA wake! sikutalajia kama watu kama wewe waweza kufikia hatua ya KU-COMMENT vitu bila hata kushirikisha BRAIN yako, Pole sana ndugu. Mmmmmh! endelea kutoa pumba zako. maana it seems kama uko half way minded... go on...
   
Loading...