Ikiwa wananchi watajitokeza kwa wingi kutoa maoni yao, watapata KATIBA wanayotaka

Calipso

JF-Expert Member
Mar 25, 2009
284
15
Leo katika harakati zangu za kimaisha nimebahatika kukutana na mmoja ya wajumbe wa Tume ya Katiba,kwa kuwa tunajuana na tunafahamiana uzuri, Tukasalimiana na kuulizana hali na baada ya salam nikampa pongezi za kuchaguliwa kwake kuwa Mjumbe wa Tume hiyo,ndipo yalipoanza hayo mazungumzo,baada ya kuongea nae sana,nikaona kuna haja ya Point hizi niziwakilishe kwenu ili tupeane mawazo:

  1. Anasema hakuna lisilowezekana
  2. Anasema Nguvu ya wananchi wenyewe ndio itakayoamua,lkn amenisisitizia kuwa wananchi wajitokeze kwa wingi na watoe lile wanalolitaka
  3. Anasema kwa jinsi Tume ilivyoundwa na utaratibu mzima basi mawazo ya wananchi ndio yatakayosikilizwa
  4. Anasema hakuna mtu atakaeweza kuchafua maoni ya wananchi,hapo ni baada ya mimi kumuuliza kuwa Vidudu mtu kama Mwinyi na wengine hawawezi kufanya wanachokita wao?
  5. Anasema maamuzi ya Mwisho yatakuwa ni ya wenyewe wananchi
  6. Anasema zanzibar nao wanaweza wakajadili wanachokita na maamuzi yao yataheshimiwa lkn wajitokeze kutoa maoni yao na waungane wawe wamoja,hapo napo nilimuuliza suala la kiuchokozi.

Nimeona haya machache niyalete kwenu,tumeongea mengi sana lkn mengine tuyaache,isipokuwa mwisho nilimwambia pamoja na yote hayo mimi CCM Siwaamini hata kidogo
 
Back
Top Bottom