Nobunaga
JF-Expert Member
- Mar 22, 2019
- 1,169
- 4,986
Kwa mujibu wa Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Mama Anna Makinda ametoa tangazo kwamba siku ya sensa, tarehe 23/08/2022 ambayo itakuwa Jumanne, haitakuwa siku ya mapumziko. Haya ni maajabu.
Kwa mujibu wa historia ya sensa za miongo miwili iliyopita, inaonesha ili kuwapata watu wote majumbani basi sensa zilifanyika siku za mapumziko yaani Jumamosi na Jumapili.
Mwaka 2002 sensa ilianza kufanyika usiku wa tarehe 24 kuamkia 25 Agosti ambayo ilikuwa ni Jumamosi kuamkia Jumapili. Mwaka 2012 sensa ilifanyika tarehe 26 Agosti ambayo ilikuwa Jumapili.
Cha kushangaza sensa ya mwaka huu 2022, tarehe iliyopangwa ni 23 Agosti ambayo itaangukia siku ya Jumanne, siku ambayo ni ya kazi, na wanasema hakutakuwa na mapumziko.
Hapa bila hata ya kutumia akili za rocket science hawatapata data zote kwa siku hiyo maana wengi watakuwa makazini, na hata wale watakaowakuta majumbani watakuwa na data nusunusu maana wengi watakuwa watoto na wafanyakazi wa majumbani ambao wanajua majina tuu, huenda hata wasijue nyumba wanayoishi ni ya wazazi wao ama ni ya kupanga.
Kwa jinsi nilivyosikia hii sensa inahitaji data nyingi mpaka viwanja na nyumba anazomiliki mtu, namba za NIDA, taarifa za walemavu, taarifa za vifo vya wazazi, taarifa za vifo vitokanavyo na uzazi, nk basi tutegemee hii sensa kuchukua zaidi ya wiki sababu ya kutopatikana kwa watu watakaotoa data zote kwa siku moja.