Ikiwa kubana matumizi ni kufuta posho kwa watumishi wa umma, futeni na posho za askari

Hivi unaelewa majukumu ya Majeshi yetu?
Unamlinganisha Mwanajeshi na Daktari!!!
Acha kabisa Masihara.
Viongozi wote wa Kisiasa wanapata Jeuri ya kutoa Matamko kwa sababu ya Jeshi.

Mkuu hakuna cha umuhimu wowote, kila mtu ni muhimu.... Askari hazalishi, je nani anamlipa mshahara, tunawalipa mshahara ili mtulinde tukiwa tunafanya kazi, kazi ya askari ni kutulinda na kuhakikisha kuna usalama ili tuzalishe kwa amani naye familia yake iende choo... ni kama baunsa tu club au bar anawalinda wanaofanya starehe ili yeye alipwe mshahara na huu ndio ukweli....
 
Kuwa askari sio kwamba ni kitu special sana, kila mtu akihitaji kuwa askari anaweza kuwa. kila binadamu huwa anamatakwa yake, kunawaliocchagua kuwa maengineer, madaktari, walimu, mafundi, wezi, wauza unga, mabaharia nk, vilevile kuna waliochagua kuwa maaskari wakijua kabisa kuna hizo risk zote sasa wafanye kazi ya kupambana na hizo risk maana ndio kazi walizochagua na kuzipenda... Kama ulipenda kuwa askari hilo ni chaguo binafsi timiza majukumu ya uaskari...

Naomba nikupinge ijapokuwa naheshimu sana maoni yako.
Sio kweli kwamba kila mtu anaweza kuwa Askari,engeneer,Daktari,Mwalimu,Fundi,Mwizi,Muuza Unga,Baharia nk.
Kila kazi ina vigezo vyake vya kuingilia.Mfano,Mimi nilitamani sana kuwa Daktari lakini nimeishia kwenye uhasibu.
 
Utaumia na stress ndugu yangu.
Serikali inachofanya ni sahihi kabisa.
Wanajeshi ni watu muhimu sana kwa ustawi wa Taifa kwa hiyo lazima walipwe Posho nono.
Napendekeza waongezewe.
Kama unaona malipo yao hayastahili,fungua kesi Mahakamani na utoe hizo hoja zako za kuchekesha walionuna.
Kwanu umesikia mie nataka kushindana au tambo? Hoja ilikuwa ni wewe kuona kundi moja muhimu dhidi ya jingine na si kutaka kutambishiana posho coz kwangu hazina tija ila nitaendelea kusisistiza hakuna kundi muhimu zaid ya jingine makundi yote ni muhimu na ndio maana hata huyo mwanajeshi anamtegeme amwana sayansi mbunifu na fundi wa silaha ili yeye akamilishe jukumu lake, ila kama unadhani tunashindana hapa na kujifanya hutaki kushindwa wakati ukweli umesha uona ni hiyari ya moyo wako hatulazimishani wa kutambiana hapa ila tunaelweshana na ni hiyari kuelewa ama kuto elewa .
 
hakuna tofauti ya umuhimu kati ya wanajeshi na watu wengine,, Kazi ya mwanajeshi ni kulinda usalama na nchi hiyo ndio kazi yake kifupi hazalishi, JE NANI ANAMLIPA MSHAHARA?????????? ili familia ya huyo Mwanajeshi iende choo lazima wengine wafanye kazi na kuzalisha kwa bidii ili yeye alipwe mashahara sasa nani muhimu hapo?? Jeshi ni Majukumu ambayo mhusika aliyapenda kuwa nayo kama ambavyo wengine walipenda kuwa maengineer nk..
 
Mkuu hakuna cha umuhimu wowote, kila mtu ni muhimu.... Askari hazalishi, je nani anamlipa mshahara, tunawalipa mshahara ili mtulinde tukiwa tunafanya kazi, kazi ya askari ni kutulinda na kuhakikisha kuna usalama ili tuzalishe kwa amani naye familia yake iende choo... ni kama baunsa tu club au bar anawalinda wanaofanya starehe ili yeye alipwe mshahara na huu ndio ukweli....

Kuanzia zamani,Jasiri na M-babe ndie hufaidi zaidi.
Huu ndio ukweli ambao watu hawapendi kuuongea.
Mwenye Nguvu hufaidi sana.Hii ni Sheria ya asili.
Majeshi yetu ndio msuli wa Serikali kwa hiyo lazima yalipwe vizuri.
 
Hivi unaelewa majukumu ya Majeshi yetu?
Unamlinganisha Mwanajeshi na Daktari!!!
Acha kabisa Masihara.
Viongozi wote wa Kisiasa wanapata Jeuri ya kutoa Matamko kwa sababu ya Jeshi.
Hakuna kazi ngumu kama kubishana na shabiki anaye jibu kimazoea kuliko mjenga hoja anaye tumia uhalisia.
 
Naomba nikupinge ijapokuwa naheshimu sana maoni yako.
Sio kweli kwamba kila mtu anaweza kuwa Askari,engeneer,Daktari,Mwalimu,Fundi,Mwizi,Muuza Unga,Baharia nk.
Kila kazi ina vigezo vyake vya kuingilia.Mfano,Mimi nilitamani sana kuwa Daktari lakini nimeishia kwenye uhasibu.

Mkuu ungependa kweli kuwa daktari sidhani kama ungeshindwa kama ungeweka nguvu na kuwa na resources za kukufikisha huko..., vilevile mtu yeyote akipenda kuwa askari na uaskari ukawa ndio hobby yake hawezi kushindwa kuwa ni swala la kupanga na maamuzi tu....
 
Kwanu umesikia mie nataka kushindana au tambo? Hoja ilikuwa ni wewe kuona kundi moja muhimu dhidi ya jingine na si kutaka kutambishiana posho coz kwangu hazina tija ila nitaendelea kusisistiza hakuna kundi muhimu zaid ya jingine makundi yote ni muhimu na ndio maana hata huyo mwanajeshi anamtegeme amwana sayansi mbunifu na fundi wa silaha ili yeye akamilishe jukumu lake, ila kama unadhani tunashindana hapa na kujifanya hutaki kushindwa wakati ukweli umesha uona ni hiyari ya moyo wako hatulazimishani wa kutambiana hapa ila tunaelweshana na ni hiyari kuelewa ama kuto elewa .

Mimi naongelea uhalisia wewe unaongelea nadharia.
Hayo unayoongea yanaongelewa sana na watetezi wa haki za binadamu.
Siku zote mwenye nguvu ndie mwenye haki.
 
Hakuna kazi ngumu kama kubishana na shabiki anaye jibu kimazoea kuliko mjenga hoja anaye tumia uhalisia.

Mimi naamini Mtu aliyekariri bila kuelewa ndio mgumu sana kumwelewesha.
Hapa hatubishani bali tunaongea uhalisia.
Wewe huelewi hata kwa nini Majeshi yetu pamoja na watu wenye Nyadhifa kubwakubwa wanalipwa Posho nono.
Umekariri tu Usawa wa binadamu.
 
Mkuu ungependa kweli kuwa daktari sidhani kama ungeshindwa kama ungeweka nguvu na kuwa na resources za kukufikisha huko..., vilevile mtu yeyote akipenda kuwa askari na uaskari ukawa ndio hobby yake hawezi kushindwa kuwa ni swala la kupanga na maamuzi tu....

Nimekwambia kila fani ina vigezo vyake na sio wote wanaoweza kuvifikia.

Mfano;Ili uwe Mwanajeshi lazima usiwe na Kilema chochote.Tayari hiyo imeshamuondoa kilema wa kidole anayetaka kuwa Mwanajeshi.
 
hakuna wafanya kaz wehu kama sekta ya elimu,nadhan n idara ya mwisho kwa kulipwa mishahara mibov na ndio kwanza wanaongoza kufanya kaz kama mchwa na ndio wanaongoza kusimama mistarin kupga kura na kuandikisha senza! mwl hana posho wala night semina zenyewe kwa manati wkt mwingne mpaka namwonea huruma mke wangu nataman nimwambie aache kaz lkn naogopa atasema namnyanyapaa make n kada ambayo mfanyakaz huwa haeshmiwi mtaani. na sasa anabanwa mpaka kona hakuna twishen ijapo awal nilikuwa namwona mke wangu ilejion anapata watoto kama mia hv mkonon akija na tsh 100 ilikuwa inamboost lkn saiz ukimwambia anatetemeka kisa ku2mbuliwa. kwa ujumla mwl hakustahl kulipwa hela mbuz kama hyo ambayo mm naipata ndan ya wiki moja,lkn kada ya afya,jesh,tra,pccb,bandari hawa watu wanamishahara kufuru wkt elim n zile2 isipokuwa kda ya ulinz na usalama hapo n nguvu na sio elimu.
Mwambie mkeo aache hyo kazi unayo iita ni ya kipumbavu then aende huko unakoona wewe wanalipwa mishahara hyo ya kufuru.
 
The higher the risks the higher the rewards.Ujinga hauondoki kwa kumchukia mwenye akili, umasikini hauondoki kwa kumchukia tajiri, kuhesabu dhambi za mwenzio hakukufanyi wewe kuwa mtakatifu":- Mchungaji PeterMsigwa
 
Kuna majeshi hayana maaana mfano kuna kesi nyingi sana polisi wanatuhumumiwa kushiriki, kupora, na kutoa au kuvujisha siri za ma informers wao bado unataka niamin kuwa wanafanya kazi nzuri?? Na kustahili posho za ongezeko kila mwaka ?? Sikiliza bossy , hakuna anayektaa posho kabisa kwa askar tatizo ni posho ambazo haziendani na uhalisia ikiwa unaweka posho kwa asilimia 90% kwa majeshi halafu tasnia zingine 0.00%_ hapo ni tatizo , wapewe posho lakin sio kwa mkupuo wa staili ile ya jk bhana #!!!#
Chuki yako binafsi usituambukize sisi. Hivi masuala yako ya kesi yamekujaje kwenye mjadala wa posho? Mbali na hayo posho zilizokatazwa na PM unazijua au ndio ulimbukeni wetu walio wengi? Posho ambazo PM amekataza sio zilizopo kisheria,zile za kisheria zipo kama kawaida wewe pambana na hali yako,if you can't fight them join them
 
Wakuu mi bado napata shida hivi hawa askari mnaosema mambo yao safi mbona sioni utofauti nawaona maisha yao magumu hawana hata uhakika wa kesho au ni kuanzia lini hayo mahela watajazwa?
 
Mimi naamini Mtu aliyekariri bila kuelewa ndio mgumu sana kumwelewesha.
Hapa hatubishani bali tunaongea uhalisia.
Wewe huelewi hata kwa nini Majeshi yetu pamoja na watu wenye Nyadhifa kubwakubwa wanalipwa Posho nono.
Umekariri tu Usawa wa binadamu.
Mh kazi unayo sababu hadi sasa hujajua nasimamia kipi nadhan unachanganya mambo.
 
Mimi naamini Mtu aliyekariri bila kuelewa ndio mgumu sana kumwelewesha.
Hapa hatubishani bali tunaongea uhalisia.
Wewe huelewi hata kwa nini Majeshi yetu pamoja na watu wenye Nyadhifa kubwakubwa wanalipwa Posho nono.
Umekariri tu Usawa wa binadamu.
Hujajua nasimamia nini na hilo ndilo tatizo kuu
 
Hakuna kazi ngumu kuliko nyingine bwana mdogo unacho kiongea wewe kipo kihisia zaid ya uhalisia na kwa maana hiyo huwezi aminisha jamii kwamba uaskari ndio kazi ngumu zaid wakati inatumia mwili zaid kuliko akili na ina utaalamu kidogo tatizo mnaongelea kukesha mnasahahu kwamba wana shift kama ambavyo Doctor ana shift , mnadanganya watu hapa eti 24hrs zawapi? Kila kazi ni muhimu kwa nafasi yake maana hata huyo askari anamtegemea daktari pia.

Mi nadhani tatizo kubwa sio kwa askari kulipo posho bali kujua kwa nini wanalipwa hizo posho.
Kwa nini hao wengine wasilipwe posho na ufaham mdogo wa wananchi juu ya kazi za majeshi yetu nalo ni tatizo kubwa ndio maana hata wanasiasa wanatumia sana haya majeshi jasa polisi kujitafutia umaarufu kwa jamii .
Ni rahisi sana mtu kusimama na kurukaruka kama maharage yanayoanza kuchemka na kuanza kusema kuwa askari hawana umuhimu wowote kwenye jamii na kusema hata polisi au jeshi likifutwa hakuna shida mana eti hawajasoma.
Huu ni imbukeni mkubwa.
Watu wanaropoka tu juu ya majeshi yetu kwa sababu haijatokea siku moja wakafanya mgomo halafu vibaka na wavuta bangi wahamie kwenye nyumba za wale wanaojiona ni watumishi bora na kuwabaka mabinti wao na wake zao na mama zao na kisha wawaibie kila wanachoona kinawafaa ndipo watu watagundua umuhimu wa kile serikali inachofanya ili kuimarisha majeshi yetu na kuwapo askari motisha.
Kuna wasimi uchwara wanasahau kuwa kwenye majeshi yetu kumesheheni wasomi wa kila namna na watu wenye taaluma za kila aina;
Kuanzia mabaunsa ,mainjinia madaktari,walimu,wahasibu, wanasiasa, wanasaikolojia, wataalam wa kivita, marubani ,wataalam wa Mawasiliano , wataalam wa computer, wanasheria,na wajanja wa kila namna.
Kwa kifupi tu ni kuwa majeshi ndizo taasisi zilizojitosheleza na zinauwezo wa kuwahudumia wananchi katika sekta zote.

Na ninazidi kumshauri Mh.Rais aimarishe sana majeshi yetu kabla ya kuanza kushughulika na jambo lolote. Huwezi kupambana na rushwa au uhalifu wowote bila kuwa na majeshi imara.
Huwezi kujitegemea kama nchi bila kuwa na majeshi imara.
Hatuwezi kulinda uhuru wetu bila kuwa na majeshi imara.
Hatuwezi kusambaza madawa na pesa za mishahara kwenye mabenki bila kuwa na majeshi imara.
Hatuwezi kuwa na wakulima na wafugaji wanaoishi kwa amani bila kuwa na majeshi imara.
Hatuwezi kuwa na maendeleo yanayotokana na vipato halali bila kuwa na taasisi imara za kiulinzi.
Mahakama zinaheshimika kwa sababu ya kuwepo kwa dola lenye majeshi.
Hatuwezi kuwa na Rais anayeheshimika ndani na nje ya nchi bila kuwa na taasisi imara za majeshi.
Wake au waume za watu hawawezi kuwa salama kwenye ndoa zao kama sio kuwa na kitu kinachoitwa nguvu ya kipolisi ya kumkamata mtu anapojaribu kutumia mabavu kumpora mke wa mtu.
Kila mtu mwenye maguvu anajitahidi kuwa mstarabu kwa sababu ya kuogopa kitu nguvu ya kipolisi jeshi. Kila mtu anamhofia mwenzake na heshimu utu wa mtu mwingine kwa sababu ya kuwepo kwa kitu jeshi. Kila taifa linaheshimu mipaka na rasilimali za nchi nyingine kwa sababu ya kuwepo kwa nguvu za majeshi.

Taifa lolote lenye majeshi lelemama yanaishia kugawanyika na kupigana wenyewe kwa wenyewe.

Majeshi yetu yanasheria zake za kiutumishi tofauti na sekta nyingine. Na mara nyingine sheria hizo zimekuwa zikiwaumiza sana kimaslahi hasa wakati wa kustafu.
Ni rahisi sana kumwona askari polisi mwenye elimu ya form 4 akiwa analipwa mshahara chini ya sh.laki tano huku akiwa ametumikia taifa kwa miaka zaidi ya 25.Jambo ambalo ni nadra kulikuta kwenye sekta nyingine. Matokeo yake askari huyo anastaafua akiwa ametumikia taifa kwa miaka 30 huku akiwa na miaka 55 na kupewa kiinua mgongo nusu ya mtumishi aliyeko kwenye sekta nyingine.

Kwa hiyo kulinganisha maslahi ya watumishi wa idara nyingine na ya majeshi ni uchochezi.
Hivi ingekuaje kama CDF na IGP wangekuwa wanalipwa kama Ma MD wa mashirika ya umma.?Ukweli ni kwamba kila mmoja anaongozwa na sheria zake.

Ili taifa lolote liwe kubwa na lenye uhakika wa watu wake kulala na kuamka asubuhi ni lazima tuwekeze sana kwenye ulinzi kwanza.
Marekani inatawala dunia kwa sababu ya kuwa na ulinzi imara sana. Mataifa yote yaliyoendelea sana yaliwekeza sana kwenye ulizi.
Ulinzi ukiwepo kila mtu atakua na uwezo wa kuwekeza na kujitafutia kipato chake halali.

Ni bora hata haya majeshi yapewe kila idara wazisimamie kijeshi ili kuleta maendeleo ya haraka halafu wananchi wawe huru kula maisha kwa amani bila kuhofia kitu chochote.

Mh. Rais ameliona hilo na sasa ni wakati wa kuboresha zaidi majeshi yetu.
Askari anaporisk maisha yake awe na uhakika wa kuiacha familia yake angalau kwenye nyumba yake endapo atapoteza maisha kwa kupigania mali za watu wengine ziwe salama.
Askari anapambana gari la mtu lisiibiwe wakati yeye hana hata bajaji. Huu ni uzalendo mkubwa.
Askari anapambana pesa za watu zisiiibiwe benki wakati yeye hana akiba benki.
Huu ni uzalendo mkubwa.
Askari hawana sikukuu wala hawana muda mwingi wa kukaa na familia zao majumbani hata wakati wa usiku.
Ukizunguka mitaani utawaona muda wote wapo kazini utadhani kuwa wapo wengi sana kumbe ni wachache ila hawana muda wa kupumzika zaidi ya kubadili majukumu.Waende kukamata,wachukue maelezo, watafute mashahidi,wapeleke mahakamani, walinde mabenki,wakinde viongozi,walinde majaji, walinde vituo vyao, wasindikize pesa ,walinde mikutano ya wanasiasa, wachukiwe na kulaumiwa na wananchi , wafanye kazi za doria usiku n.k. n.k.
Kama kunamtu anayefikiri kuwa kazi ya uaskari ni nyepesi yenye maslahi mazuri labda tu ajiulize ni kwa nini huko hakuna wahindi,waarabu na watoto wa mawaziri au watoto wa matajiri?

Watumishi wengine wajenge hoja za kwa nini walipwe posho kama askari na sio kusema kuwa posho za askari zifutwe.

Mwisho ningeomba Mh. Rais aimarishe zaidi uchumi wa nchi hasa kilimo kupitia majeshi yetu.
Ardhi yote yenye uwezekano wa kufanya kilimo cha umwagiliaji basi ikabidhiwe kwene jeshi laagereza na JKT ili chakula kizalidhwe kwa wingi sana na wananchi wapate chakula kwa bei nafuu na kwa wingi.

Watanzania wanataka maendeleo ya haraka na unafuu wa maisha sio mashindano ya kugombania posho kwa watu wanashindana kufanya vikao maofisini badala ya kazi.
 
Hana uwezo huo tutampindua, Askari posho zetu ni zaidi ya mshahara na hawezi punguza ata mia. ....Anatuogopa kama stima ....kwani umesikia kuna askari hewa aliyefukuzwa kazi. .??
Hahahaha du mkuu hapo umenena jamaa anajua kbsa kwa watumishi wengne tofauti majeshi hawaslimian kbsa sasa rafiki zake lazima wawe wake jamaa wanao simama nyuma yake coz akibeep tu jamaa wamampgia
 
Mkuu hakuna cha umuhimu wowote, kila mtu ni muhimu.... Askari hazalishi, je nani anamlipa mshahara, tunawalipa mshahara ili mtulinde tukiwa tunafanya kazi, kazi ya askari ni kutulinda na kuhakikisha kuna usalama ili tuzalishe kwa amani naye familia yake iende choo... ni kama baunsa tu club au bar anawalinda wanaofanya starehe ili yeye alipwe mshahara na huu ndio ukweli....
Usiongee kitu kama hukijui sawasawa, haiwezekani kuainisha majukumu yote ya vyombo vya ulinzi na usalama kama matangazo ya biashara kwa sababu za kiusalama.Ukitaka kufahamu zaid tafuta wasemaji wa vyombo husika wakueleweshe na sio kuropoka.
 
Back
Top Bottom