Poleni na mihangaiko,
Nimekaa na kuwaza,Tukilala tunafunga milango,je tunajisitirije tukilala?ikitokea ukafa ukiwa usingizini,yaani ulale usiamke mtu au watu watakao kukuta kwa mara ya kwanza watakukuta na hali ipi?Hasa watu wa mikoa ya joto!
Sijawahi kuvuta bangi hata siku moja wala sigara ya kawaida,mirungi na powder situmii,imagine umekufa ukiwa usingizini!Marehemu babaangu alikufa Usingizini so inaweza kutokea hata kwangu au kwako!NAONA mkuu bange unavuta msokoto ule mkubwa,,zamani kijiweni tulikuwa tunauita famtom,,,si mchezo
Wazee wa dar."...Hasa watu wa mikoa ya joto!"
Kivipi yaani mkuu, sijakupata hapo
anhaa lakini wakifa si wameshakufa..au unataka kumaanisha nini? Baridi/joto how?Kwa sababu ya baridi watu kama wa arusha wanalala na nguo na je wa Daresaalam!
inategemea na ulivyojifunika wakati wa kulala au pengine hujajifunika kote... au we unazungumzia kujisitiri na nguoUkifa usingizini imagine unakutwa na mtu wa kwanza ukiwa na hali gani?umejisitiri kiasi gani/
Me naona aibu nikifa usingizini nikiwa uchi,bora kuungua,kuzama baharini au kugongwa na gari,maana yake ni kwamba nitakuwa nimetoka najielewa maana nimetoka nyumbani!Ukishakufa si ndo ushakufa?
why uumize kichwa kujiuliza vitu nje ya uwezo wako?
una uhakika utakufa ndani ya nyumba?
au utakutwa maiti nzima?
unajuaje utaungua usipatikane hata majivu?
au ajali ya boti au meli maiti yako isipatikane?
Unajiuliza hayo tu mbona mengine hujiulizi?
Ukiwa unatibiwa unajitambua na ndio maana unakuwa na Dr wako,imagine huwezi kusema hapo hapana wanakukuta watu wa5 duh!Mbona ukiumwa doctor nesi Na anayekuuguza wanaona kila sehemu ya mwili wako Na kesho unaonana nao,sembuse umekufa!