Ijumaa ya kesho ni siku ya kimataifa ya Quds

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,175
2,000
Mamilioni ya wapenda haki kote duniani kesho watajitokeza katika pembe mbalimbali za ulimwengu kwa ajili ya kushiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yenye lengo la kutangaza himaya na uungaji mkono kwa taifa madhulumu la Palestina.
Maandamano ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Quds yanatarajiwa kuwa ya aina yake hasa kutokana na mazingira yanayotawala hivi sasa katika ulimwengu wa Kiislamu kwa upande mmoja na kushadidi jinai na ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhlumu wa Palestina kwa upande wa pili.
Nchini Yemen kamati ya maandalizi ya Siku ya Kimataifa ya Quds imewataka wananchi wa nchi hiyo ambao kwa sasa wanakabiliwa na hujuma na mashambulio ya kinyama ya Saudi Arabia kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya Quds ili kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi madhulumu wa Palestina.
Nchini Tanzania, Waislamu wa nchi hiyo na wapenda haki wanatarajiwa kuungana na Waislamu pamoja na wapenda haki wenzao wa Ukanda wa Afrika Mashriki kama Kenya, Burundi, Uganda na kwingineko kushiriki katika maandamano ya kesho ya Siku ya Kimataifa ya Quds. Aidha maeneo ya bara Ulaya pia yanatarajiwa kushuhudia maandamano ya Siku ya kimataifa ya Quds hapo kesho.
Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani ilitangazwa na hayati Imam Ruhullah Khomeini muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds na kuwataka Waislamu kote duniani kushiriki katika maandamano ya siku hiyo ili kuonesha hasira zao dhidi ya siasa za kibaguzi za Israel huko Palestina na kutangaza kwa sauti moja himaya yao kwa wananchi wa Palestina.
 

Jodeo

JF-Expert Member
Mar 10, 2015
1,184
2,000
Inabidi mwende mkawatoe waisrael kwenye hiyo ardhi. Siyo kuongelea pembeni. Kitakachowatokea mtatusimulia

By the way, utakieni amani Yerusalem
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom